jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,540
- 25,834
Baada ya chairman Mbowe kumtaka mh rais kufanya mchakato wa maridhiano, upinzani ghafla umegawanyika zaidi. Wako wana chadema wanaokubalina, na wako wasiokubaliana na hatua ya mwenyekiti wao kuomba maridhiano ya kitaifa.
Kuna wanachadema ambao wamechukizwa, na wengine wakiungana na Zitto kwenye kulaani uamuzi wa Freeman. Wengi wao wanajiuliza ni kwa vipi wasahau yale waliyofanyiwa? haswa wamekuwa wakimtaja Tundu Lissu.
kwa maoni yangu, maamuzi ya rais baada ya ushauri huo wa chairman Mbowe, yana umuhimu mkubwa sana kwenye mustakabali wa huko tunakoelekea kama Taifa. Ni wazi bado wale ambao ni radical bado watakuwepo, lakini hawatakuwa na ushawishi mkubwa endapo maridhiano yatakuwepo.
Kwasababu upande ambao ndugu Zitto yumo, sina shaka na Tundu Lissu pamoja na watanzania wengi tu wako upande huo. Kina Tundu Lissu wao ndo wamekuwa kama sadaka kwa wengine. Wao pamoja na maridhiano, wanataka “justice”. ”And justice delayed equals justice denied”
kusipokuwepo na maridhiano yanayohusisha pande zote, basi tutakuwa tumefungua ukurasa mpya kwenye siasa za Tanzania. Yani sasa kutakuwepo na Kundi la “radicals” kwenye upinzani, ambalo hapo awali halikuwa na wapenzi wengi.Radicals ni wale wenye misimamo mikali zaidi. Wale ambao wako tayari kupinga kwa njia za tofauti na maridhiano. Mfano maandamano, migomo nk.
Wamarekani weusi nao walitumia njia hizo kwa kupitia MLK ambaye alikuwa moderate, pamoja na Malcom X ambaye alikiwa radical. Tofauti zao ilipokuja kwenye kudai haki, wengi tunazifahamu. Martin Luther King yeye alipendelea maridhiano na njia za amani(maandamano ya amani nk), wakati Malcom yeye alisema ni haki by any means hata kwa mapigano.
Haya ni maoni yangu. Baada ya kuwasoma members wengi humu ambao hapo awali walikuwa na mtizamo unaofanana, na sasa hawakubaliani kutokana na kauli za Mbowe Vs Zitto. Nina imani kuwa baada ya hili “vumbi” kutulia, watapata wasaa wa kuona ni wapi waelekee. Pia kina wale wapambe wa rais ambao wanataabika sana. Wao wanasema Mbowe ameomba Poo! Na wanamshauri rais akazie hapo hapo aachane na mambo ya maridhiano! Hao ni kama mafisi tu. Wengi wanaomzunguka rais wanalinda matumbo yao tu by any means!
Tusubiri response ya Maghufuli, halafu na ya Lissu.