Upinzani wa Tanzania ni wa vimatukio, Rais Samia ameumaliza kisayansi

Uzuri wote tunakatwa tozo apo ndio utamu unapokuja
Tozo Ni kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu ,Taifa letu litajengwa kwa mikono yetu wenyewe, wajibu wa kujenga Taifa letu lipo katika mikono na mabega yetu watanzania
 


Samia yupo kisayansi zaidi, leo kafanya kitu kikubwa kule Kigoma lakini kimeanza na kumalizika kimya kimya tu.

Hakutakuwa na kishindo cha vyombo vya habari kuelezea mazingira ya uwekezaji yaliyowezeshwa leo hii huko Kigoma, suala la nishati ya umeme linakwenda kuufungua mazima ule mkoa.
 
Rais Samia Ni mchapa kazi Sana, Ni kiongozi aliyejitoa na kujitolea kuwatumikia watanzania kwa Dhati ya moyo wake na kwa nguvu zake zote, Ndio maana unaona muda wote yupo kazini kuwatumikia watanzania
 
Rais Samia Ni mchapa kazi Sana, Ni kiongozi aliyejitoa na kujitolea kuwatumikia watanzania kwa Dhati ya moyo wake na kwa nguvu zake zote, Ndio maana unaona muda wote yupo kazini kuwatumikia watanzania
Na wewe muda wote uko wapi na unafanya nini?
 
Na wewe muda wote uko wapi na unafanya nini?
Nipo shambani naandaa mashamba kwa ajili ya msimu mpya hasa baada ya Rais wetu kutupatia matumaini makubwa sisi wakulima kutokana na kushuka kwa Bei ya mbolea kulikotokana na uamuzi wake wakutoa Ruzuku ya mabillioni ya Fedha na uwepo wa soko la uhakika kwa mazao yetu
 
Mimi naongea ukweli, Kama hauamini angalia hata mitaani namna watu wasivyo na habari na muda na habari zenu
Sasa inakuwaje unapoteza muda wote kuandika hili gazeti hili wakati unajua kuwa huu upinzani haupo? Utakuwa umechanganyikiwa akili. Uchawa mbaya sana
 
Kama anakubalika, kwanini mnatumia nguvu kubwa hivyo kutuaminisha?
Wala hatutumii nguvu Bali tunaelezea Yale aliyoyafanya mh Rais wetu ndani ya muda mfupi tangia aapishwe kuwa Rais wetu na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama
 
Tangu asubuhi upo JF kusifia uozo muda wa kwenda shambani utaupata wapi?
 
Sasa inakuwaje unapoteza muda wote kuandika hili gazeti hili wakati unajua kuwa huu upinzani haupo? Utakuwa umechanganyikiwa akili. Uchawa mbaya sana
Vyama vipo Ila upinzani haupo kwa hiyo naandika kwa ajili ya vyama hivyo
 
Hicho ndio ulichofanya?
Mbona 90% ya bandiko lako unaongelea upinzani?
Mambo aliyoyafanya mh Rais wetu mpendwa nimeyaeleza Sana humu na nitaendelea kuyaelezea Sana tu maana mh Rais anafanya kazi kila siku na muda wote katika kuwatumikia watanzania wanyonge wasio na sauti

Ukienda kwa wakulima utaona na kukuta Alama za mh Rais wetu namna alivyo wasaidia wakulima wa nchi hii, utaona namna mbolea ilivyoshuka Bei baada ya kutoa Ruzuku ya mabillioni

Ukienda katika Elimu utaona namna alivyo Jenga shule nyingi mpya, ujenzi wa vyumba vya madarasa, utoaji wa Elimu bure Hadi kidato Cha sita, Hali hii imesaidia Sana wanafunzi Kuendelea na masomo yao na kupata Elimu bila shida hata Kama wametoka familia duni

Ukienda secta binafsi utaona namna mh Rais wetu mpendwa alivyoimarisha na Sasa inatoa mchango mkubwa katika uchumi wetu na hata fursa za ajira kwa vijana,lakini pia wawekezaji na uwekezaji umeongezeka Sana hapa nchini,bila kusahau mafuriko ya watalii yameongezeka kutokana na ubunifu wa mh Rais kupitia royal Tour,
 
Sasa kwann bado anazuia uhuru wa upinzani kufanya vikao?
 
Tangu asubuhi upo JF kusifia uozo muda wa kwenda shambani utaupata wapi?
Saizi Ni kiangazi kipindi Cha maandalizi ya msimu mpya wa kilimo mashambani, bila Shaka hata wewe upo humu tangia asubuhi ndio maana umeweza kuona waliopoo humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…