Uchaguzi 2020 Upinzani wakisusia Ubunge/Udiwani, nini kitatokea? Hasara au faida?

Uchaguzi 2020 Upinzani wakisusia Ubunge/Udiwani, nini kitatokea? Hasara au faida?

Joined
Mar 28, 2014
Posts
38
Reaction score
27
Habari wana JF,

Ni swali la kujiuliza.

Endapo ikatokea wapinzani wote nchini wakashauriana katika kikao chao kinachosadikikia kuwepo leo kuwa, wabunge na madiwani wao wote waliopata nafasi katika uchaguzi huu kususia na kutoingia sehemu zao za kazi Je, nini kiatokea?

Nini faida na Hasara za uamuzi wa aina io kwa Taifa kama taifa na watanzania kwa ujumla.

Je, kuna hasara gani au faida watazipata upinzani?

Je, faida au hasara zipi kwa chama tawala?

Nawasilisha kwa utiiiifu🙏
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Nikikumbuka zile ngebe za akina Lord deninning na kundi lake humu nacheka sana

Endelea kucheka na kufurahia Mkuu ,sisi ni Binadamu na Siku hazigandi ukija wakati wako wa kulia usistuke.
 
Litakua ni jambo sahihi sana kwao. Kama mtu mmoja tu amejiapiza mara kadhaa hadharani kutopeleka maendeleo maeneo ambako wananchi watachagua wagombea wa vyama vingine, kuna umuhimu gani wa kufanya kazi na mtu mbaguzi kama huyo?
 
Wasuse tu, hizo nafasi CCM watafurahia kuzijaza bila kupoteza muda, kwani walivyosusa 2019 uchaguzi wa serikali za mitaa kilitokea nini?

Hakuna kilicho tokea na Maisha yame songa unaonaje kwa Sababu CCM ni kila kitu hapa Tanzania kwa sasa pelekeni Hoja ili muibadili Katiba iwe ya Chama kimoja.Hakuna haja ya kupoteza Pesa kufanya Maigizo ,hakuna haja ya kuumiza wengine kwa kuwaua na kuwaachia vilema kisa ni Madaraka ambayo tayari mnayo.
 
Akitokea mtu akawashauri Wapinzani waliochaguliwa wasuse, huyo atakuwa sio mzima, ni kichaa!. Na kama kuna mpinzani amechaguliwa na wananchi, halafu akatokea kichaa mmoja kumshawishi agomee, huyo mpinzani pia atakuwa sio mzima!.

Kwenye uchaguzi kazi ya chama ni kukudhamini tuu, lakini unachaguliwa na wananchi. Ukiisha chaguliwa wewe unakuwa ni mtumishi wa watu na sio wa chama.

Kama watu wamekuamini wakakuchagua, chama kikikuzuia ni kuwasaliti hao watu na ukikubali na wewe ni msaliti!.
P
 
Akitokea mtu akawashauri Wapinzani waliochaguliwa wasuse, huyo atakuwa sio mzima, ni kichaa!. Na kama kuna mpinzani amechaguliwa na wananchi, halafu akatokea kichaa mmoja kumshawishi agomee, huyo mpinzani pia atakuwa sio mzima!.

Kwenye uchaguzi kazi ya chama ni kukudhamini tuu, lakini unachaguliwa na wananchi. Ukiisha chaguliwa wewe unakuwa ni mtumishi wa watu na sio wa chama.

Kama watu wamekuamini wakakuchagua, chama kikikuzuia ni kuwasaliti hao watu na ukikubali na wewe ni msaliti!.
P
Kichaa ni yule alieagiza asiowapenda wahujumiwe na wehu wakatekeleza.
 
Kiti kimoja cha ubunge!!! Aisee, na kelele zote hapa mtandaoni!!! Poleni sana.
Mkuu nenda taratibu bado mbele pana kona kali sana na Simba wametanda kila mahali na chini pana mto wenye mamba wengi sana sidhani kama mtavuka salama
 
Maagizo yalishatolewa kwa Wananchi kuwa, mkinichanganyia tu Viongozi basi sahauni maendeleo. Sasa ni Diwani/Mbunge yupi atakaekubali kuwa kikwazo cha maendeleo kwenye eneo lake??

Kilichofanyika safari hii ni sawa na Mwenyikiti wa kijiji kuwatangazia Wanakijiji wote washiriki kwenye maandalizi ya Sherehe itakayofanyika kijijini kwao.

Kila mwanakijiji alijitoa kwa hali na mali kufanikisha shughuli ile. Siku ya sherehe Wanakijiji wote walijumuika pamoja kwa furaha. Lakini cha ajabu ilipofika wakati wa chakula M/Kiti yule na Familia yake walijitenga na kuketi kivulini. Walikula na kunywa peke yao bila kuwajali waliohangaika ktk kufanikisha shughuli ile.

Akatokea Mwanafamilia mmoja akamuuliza Babake ni nini hii?? Mbona Wale Viongozi walikutangulia walikuwa hawfanyi ubaguzi huu?? Baba kajibu chakula hiki ni kitamu nisingependa kila mtu akile. Lakini Baba chakula hiki ni kingi na tulishirikiana ktk maandalizi iweje tuwatenge?

Baba akasema sikilizeni niwaambie, wale wote hawafai kwani wana uwezo mkubwa kuliko ninyi. Hata kwenye kula watakula haraka kuwashinda ninyi. Lkn Baba tuna rafiki zetu kule itakuaje?? Tutawachukua wachache kuja kuketi mezani baada ya ninyi kumaliza. Watakuja kula vilivyosaza.

Vipi kuhusu ushirikiano na wao hapa kijijini si watatutenga Baba?? Hapana kwani tumeoleana. Wako waliooa kwetu nasi tukaoa kwao. Hivyo wengi ni Wajomba.

Kama ndivyo kwanini basi Baba uliwaweka wale walinzi waliokuwa wakiwapiga ili wakae mbali na chakula?? Baba aliinamisha kichwa chini kwa aibu.
 
Kuna two antagonistic forces hapo. Ya kwanza ni kwamba wakikubali watakuwa wamehalalisha uchaguzi batili na watashiriki batili zote (mf kuondoa term limit) zitakazopitia bungeni ktk kipindi cha miaka 5 ijayo.

Force nyingine wakigoma, watakuwa wamewadharau wananchi na kutanguliza maslahi ya chama zaidi.

Kwahiyo kazi iliyo mbele ni kuchagua the lesser evil.
 
Back
Top Bottom