Uchaguzi 2020 Upinzani wakisusia Ubunge/Udiwani, nini kitatokea? Hasara au faida?

Uchaguzi 2020 Upinzani wakisusia Ubunge/Udiwani, nini kitatokea? Hasara au faida?

Habari wana JF,

Ni swali la kujiuliza.

Endapo ikatokea wapinzani wote nchini wakashauriana katika kikao chao kinachosadikikia kuwepo leo kuwa, wabunge na madiwani wao wote waliopata nafasi katika uchaguzi huu kususia na kutoingia sehemu zao za kazi Je, nini kiatokea?

Nini faida na Hasara za uamuzi wa aina io kwa Taifa kama taifa na watanzania kwa ujumla.

Je, kuna hasara gani au faida watazipata upinzani?

Je, faida au hasara zipi kwa chama tawala?

Nawasilisha kwa utiiiifu🙏
Kwani kususa wameanza Leo? Kuna siku walishafunga hadi plasta midomoni, kwa hiyo kawaida tu!
 
Akitokea mtu akawashauri Wapinzani waliochaguliwa wasuse, huyo atakuwa sio mzima, ni kichaa!. Na kama kuna mpinzani amechaguliwa na wananchi, halafu akatokea kichaa mmoja kumshawishi agomee, huyo mpinzani pia atakuwa sio mzima!.

Kwenye uchaguzi kazi ya chama ni kukudhamini tuu, lakini unachaguliwa na wananchi. Ukiisha chaguliwa wewe unakuwa ni mtumishi wa watu na sio wa chama.

Kama watu wamekuamini wakakuchagua, chama kikikuzuia ni kuwasaliti hao watu na ukikubali na wewe ni msaliti!.
P

Kipi bora abaki kuwafurahisha wananchi waliomchagua au aachie apatikane wa ccm ili yapatikane maendeleo kwa wananchi hao??
 
Upinzani Huzaliwa Hata Katika Watu 2 Mke na Mume hamwazi wala kuwa wamoja kwa yote..hivyo Humu humo Bunge la Chama Chetu watapasuka hilo mlijue kabisa..Kwani Lile Kundi la G 55 la akina Tuntemeke Sanga, Njelu Kasaka and Co Lilikua la Chadema au ACT??

Mtaona wao wenyewe kule wanageukana tena kwa Moto wa hatari...
 
Wewe Paskali ndio sio mzima, siku za nyuma ulikuwa na akili timamu lakini hivi sasa umebaki na kasha kwenye fuvu la uso wako,
aibu kubwa kwako lakini pia na kwa wale wanakuamini
 
Habari wana JF,

Ni swali la kujiuliza.

Endapo ikatokea wapinzani wote nchini wakashauriana katika kikao chao kinachosadikikia kuwepo leo kuwa, wabunge na madiwani wao wote waliopata nafasi katika uchaguzi huu kususia na kutoingia sehemu zao za kazi Je, nini kiatokea?

Nini faida na Hasara za uamuzi wa aina io kwa Taifa kama taifa na watanzania kwa ujumla.

Je, kuna hasara gani au faida watazipata upinzani?

Je, faida au hasara zipi kwa chama tawala?

Nawasilisha kwa utiiiifu[emoji120]
Bunge live litarudi, alfu , na Gwaji atawatia sana tu
 
Habari wana JF,

Ni swali la kujiuliza.

Endapo ikatokea wapinzani wote nchini wakashauriana katika kikao chao kinachosadikikia kuwepo leo kuwa, wabunge na madiwani wao wote waliopata nafasi katika uchaguzi huu kususia na kutoingia sehemu zao za kazi Je, nini kiatokea?

Nini faida na Hasara za uamuzi wa aina io kwa Taifa kama taifa na watanzania kwa ujumla.

Je, kuna hasara gani au faida watazipata upinzani?

Je, faida au hasara zipi kwa chama tawala?

Nawasilisha kwa utiiiifu🙏
ushaambiwa hakuna connections,km hakuna connections no maendeleo, ikiwepo conection maendeleo yatakuja hizo ndo faida na hasara zakenadhani umeelewa.
 
Hahahaha
Wasuse tu, hizo nafasi CCM watafurahia kuzijaza bila kupoteza muda, kwani walivyosusa 2019 uchaguzi wa serikali za mitaa kilitokea nini?

Maagizo yalishatolewa kwa Wananchi kuwa, mkinichanganyia tu Viongozi basi sahauni maendeleo. Sasa ni Diwani/Mbunge yupi atakaekubali kuwa kikwazo cha maendeleo kwenye eneo lake??

Kilichofanyika safari hii ni sawa na Mwenyikiti wa kijiji kuwatangazia Wanakijiji wote washiriki kwenye maandalizi ya Sherehe itakayofanyika kijijini kwao.

Kila mwanakijiji alijitoa kwa hali na mali kufanikisha shughuli ile. Siku ya sherehe Wanakijiji wote walijumuika pamoja kwa furaha. Lakini cha ajabu ilipofika wakati wa chakula M/Kiti yule na Familia yake walijitenga na kuketi kivulini. Walikula na kunywa peke yao bila kuwajali waliohangaika ktk kufanikisha shughuli ile.

Akatokea Mwanafamilia mmoja akamuuliza Babake ni nini hii?? Mbona Wale Viongozi walikutangulia walikuwa hawfanyi ubaguzi huu?? Baba kajibu chakula hiki ni kitamu nisingependa kila mtu akile. Lakini Baba chakula hiki ni kingi na tulishirikiana ktk maandalizi iweje tuwatenge?

Baba akasema sikilizeni niwaambie, wale wote hawafai kwani wana uwezo mkubwa kuliko ninyi. Hata kwenye kula watakula haraka kuwashinda ninyi. Lkn Baba tuna rafiki zetu kule itakuaje?? Tutawachukua wachache kuja kuketi mezani baada ya ninyi kumaliza. Watakuja kula vilivyosaza.

Vipi kuhusu ushirikiano na wao hapa kijijini si watatutenga Baba?? Hapana kwani tumeoleana. Wako waliooa kwetu nasi tukaoa kwao. Hivyo wengi ni Wajomba.

Kama ndivyo kwanini basi Baba uliwaweka wale walinzi waliokuwa wakiwapiga ili wakae mbali na chakula?? Baba aliinamisha kichwa chini kwa aibu.
Nimepata kitu
 
Itakuwa vyema kama watajitoa na sio kususia kwa sababu:
1. Wakikubali matokeo katika majimbo waliyoshinda na kukataa katika yale waliyoshindwa wataonekana wanafiki.
2. Wataupa uhalali uchaguzi wote ambao wameishatangaza kuwa haukuwa wa haki.
3. Watawanyima fursa ya maendeleo wananchi wa majimbo yao maana wameishaambiwa kuwa ingawa siasa haina chama, hauwezi kupeleka chakula kwa jirani wakati watoto wako wanakufa njaa.
4. Watatoa uhalali kwa mabadiliko yeyote ya Katiba ambayo yatafanyika kwa kuonekana kama vyama zaidi ya viwili ( CCM na CUF) vimeshiriki.
5. Watabebeshwa lawama kwa matatizo yeyote yatakayotokea huko mbele kwa kuambiwa uwepo wao ndio umezuia hayo maendeleo.
6. Ukiona mtu aliyefanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa haupo kabisa anabadilika dakika ya mwisho na kukubembeleza mbakie katika uchache wenu fahamu hakutakii mema.
7. Kwa sababu mtu unagombea ubunge ili upate nafasi ya kuweza kuwasemea waliokuchagua bungeni, kama ukiona nafasi hii haitakuwepo, basi ni bora ujitoe. Wote tuliona jinsi wabunge wa upinzani walivyokuwa wakitendewa pamoja na kuwa idadi yao ilikuwa sio haba.
8. Siasa na kuwatetea wananchi sio lazima uwe bungeni tu. Hata nje ya bunge inawezekana tu.

Amandla....
Umeandika kitu heavy sana sasa naanza kuelewa
 
Kweli paskali uko sahihi hata Kama wajumbe siyo watu wazuri.
Jambo la kujadili hapa ni kwamba hao chadema wanaopaswa kususia ubunge wako wapi?
Au wanachama wote na viongozi wote wa chadema Tanzania nzima wanakaa kikao kumjadili mtu mmoja tu ajitoe ubunge? Wana akili kweli hao watu?
Tunajua Mbowe alikuwa anachukua sehemu ya mishahara ya wabunge na alikuwa anakusanya mabillion. Sasa anaona mbunge mmoja Hana faida nae Tena Sasa anataka kuanza wivu kwa huyu mwanamama eti ajitoe, akijitoa mmoja Ana effect gani? Wangekuwa 50 Mbowe angekubali kusikia wazo la kujitoa ili akose mishahara yao?
Katiba ya Chadema inalazimisha wabunge wa kuchaguliwa kutoa laki 5, viti maalum kutoa 1560000 kila mwezi kwa chama na Mbowe huwa anatumia anavyojua yeye. Bunge liliopita alishutumiwa kutafuna 8.9bilion mishahara ya wabunge.
Hiyo ndiyo saccos, ila nina uhakika wakimlazimisha kumtoa ubunge kupitia chadema atahamia CCM na atashinda maana watu wa nkansi walichagua mtu siyo chama.

Kipigo Cha shoga mwizi mwaka huu wamekipata.
P
🤣
 
ACT ndio chama kilichopata mafanikio makubwa zaidi kwenye huu uchaguzi. Idadi ya wabunge wake imeongezeka kwa 300%. Idadi ya kura zao zaUrais pia imeongezeka.

Zitto Kabwe ni mbinafsi tu. Kwa sababu yeye hajashinda basi anataka kuzuia wengine wasitumikie watu waliowachagua.

Nitashangaa sana wakimsikiliza.
 
Hakika watawaumiza wananchi waliowachagua
 
Vichaa ni wale wote wanaofahamu ukweli namna uchaguzi ulivyoendeshwa halafu wanakaa kimya.
Umemjibu vema sana huyu jamaa, anaezeeka vibaya na kusotea teuzi ili maisha yaende na hapo ni mwandishi wa habari,na mwanasheria think about it.Unafiki mtupu.
 
Habari wana JF,

Ni swali la kujiuliza.

Endapo ikatokea wapinzani wote nchini wakashauriana katika kikao chao kinachosadikikia kuwepo leo kuwa, wabunge na madiwani wao wote waliopata nafasi katika uchaguzi huu kususia na kutoingia sehemu zao za kazi Je, nini kiatokea?

Nini faida na Hasara za uamuzi wa aina io kwa Taifa kama taifa na watanzania kwa ujumla.

Je, kuna hasara gani au faida watazipata upinzani?

Je, faida au hasara zipi kwa chama tawala?

Nawasilisha kwa utiiiifu🙏

Endapo ikatokea wapinzani wote nchini wakashauriana katika kikao chao kinachosadikikia kuwepo leo kuwa, wabunge na madiwani wao wote waliopata nafasi katika uchaguzi huu kususia na kutoingia sehemu zao za kazi Je, nini kiatokea?

Jibu:
Kwa madiwani na wabunge itapelekea kurudiwa kwa uchaguzi kwa hizo sehemu ambazo nafasi zitatokea au kuachwa wazi. Hii haina tofauti na kama mbunge anapo kufa au kuacha nafasi yake.

Nini faida na Hasara za uamuzi wa aina io kwa Taifa kama taifa na watanzania kwa ujumla.

Jibu:
Hasara moja wapo ni kurudia kwa uchaguzi, na kutumia tena pesa. Pili, wateule wapya wanaweza kuto pedwa kwenye sehemu usika na kupelekea kudumaa kwa maendeleo. kama watu wakisusa kunaweza kudumaza maendeleo. Diwani au mbunge peke yake hawezi kuleta maendeleo sehemu usika. Tatu, kunaweza kuwa kulikuwa na kusudi kwanini mbunge au diwani hakuweza kupita kwa kura, inaweza kuwa labda hana uwezo wa uongozi na ni wizi, kama wata force au kumuweka kwa hila basi hiyo sehemu watu wanaweza pata matatizo.

Je, kuna hasara gani au faida watazipata upinzani?

jibu:
Hasara ni kubwa, wengi wao watakosa Ajira. Faida kwa upinzani ipo na ni kubwa, lakini sio rahisi kupimwa kwa Pesa. Wanaweza kutumia hili jambo kama mtaji wa siasa uko mbeleni.

Je, faida au hasara zipi kwa chama tawala?

Jibu:
Hasara ni kubwa kwa nchi. Siku zote watu kabla ya kufanya "Investment" au kukopesha, kuna vipimo wanaangalia. Kwa mfano, wanaweza kuangalia usalama ndani ya nchi, level ya corruption au matumizi mabaya ya jeshi.
Pili chama tawala kinaweza "kuvujisha" rasilimali za chi maana hakuna chama chochote ambacho kinaweza kupiga kelele tena, nadhani hujasahau issue Ya " Richmond". Kama unataka kujua hali itavyo kuwa unaweza kuangalia nchi kama China, North Korea au Rwanda. Serikali inaweza kuamka na kusema hakuna "Jamiiforums tena au wanaweza ku block Instagram, na hakuta kuwa na mtu mwenye uwezo wa kupiga kelele. Tatu wanaweza kubadilisha "Katiba" kuiweka vizuri ili iwe upanda wao.

Asante
 
Back
Top Bottom