Uchaguzi 2020 Upinzani wakisusia Ubunge/Udiwani, nini kitatokea? Hasara au faida?

Kwani kususa wameanza Leo? Kuna siku walishafunga hadi plasta midomoni, kwa hiyo kawaida tu!
 

Kipi bora abaki kuwafurahisha wananchi waliomchagua au aachie apatikane wa ccm ili yapatikane maendeleo kwa wananchi hao??
 
Upinzani Huzaliwa Hata Katika Watu 2 Mke na Mume hamwazi wala kuwa wamoja kwa yote..hivyo Humu humo Bunge la Chama Chetu watapasuka hilo mlijue kabisa..Kwani Lile Kundi la G 55 la akina Tuntemeke Sanga, Njelu Kasaka and Co Lilikua la Chadema au ACT??

Mtaona wao wenyewe kule wanageukana tena kwa Moto wa hatari...
 
Wewe Paskali ndio sio mzima, siku za nyuma ulikuwa na akili timamu lakini hivi sasa umebaki na kasha kwenye fuvu la uso wako,
aibu kubwa kwako lakini pia na kwa wale wanakuamini
 
Bunge live litarudi, alfu , na Gwaji atawatia sana tu
 
ushaambiwa hakuna connections,km hakuna connections no maendeleo, ikiwepo conection maendeleo yatakuja hizo ndo faida na hasara zakenadhani umeelewa.
 
Hahahaha
Wasuse tu, hizo nafasi CCM watafurahia kuzijaza bila kupoteza muda, kwani walivyosusa 2019 uchaguzi wa serikali za mitaa kilitokea nini?

Nimepata kitu
 
Umeandika kitu heavy sana sasa naanza kuelewa
 
🤣
 
ACT ndio chama kilichopata mafanikio makubwa zaidi kwenye huu uchaguzi. Idadi ya wabunge wake imeongezeka kwa 300%. Idadi ya kura zao zaUrais pia imeongezeka.

Zitto Kabwe ni mbinafsi tu. Kwa sababu yeye hajashinda basi anataka kuzuia wengine wasitumikie watu waliowachagua.

Nitashangaa sana wakimsikiliza.
 
Hakika watawaumiza wananchi waliowachagua
 
Vichaa ni wale wote wanaofahamu ukweli namna uchaguzi ulivyoendeshwa halafu wanakaa kimya.
Umemjibu vema sana huyu jamaa, anaezeeka vibaya na kusotea teuzi ili maisha yaende na hapo ni mwandishi wa habari,na mwanasheria think about it.Unafiki mtupu.
 


Endapo ikatokea wapinzani wote nchini wakashauriana katika kikao chao kinachosadikikia kuwepo leo kuwa, wabunge na madiwani wao wote waliopata nafasi katika uchaguzi huu kususia na kutoingia sehemu zao za kazi Je, nini kiatokea?

Jibu:
Kwa madiwani na wabunge itapelekea kurudiwa kwa uchaguzi kwa hizo sehemu ambazo nafasi zitatokea au kuachwa wazi. Hii haina tofauti na kama mbunge anapo kufa au kuacha nafasi yake.

Nini faida na Hasara za uamuzi wa aina io kwa Taifa kama taifa na watanzania kwa ujumla.

Jibu:
Hasara moja wapo ni kurudia kwa uchaguzi, na kutumia tena pesa. Pili, wateule wapya wanaweza kuto pedwa kwenye sehemu usika na kupelekea kudumaa kwa maendeleo. kama watu wakisusa kunaweza kudumaza maendeleo. Diwani au mbunge peke yake hawezi kuleta maendeleo sehemu usika. Tatu, kunaweza kuwa kulikuwa na kusudi kwanini mbunge au diwani hakuweza kupita kwa kura, inaweza kuwa labda hana uwezo wa uongozi na ni wizi, kama wata force au kumuweka kwa hila basi hiyo sehemu watu wanaweza pata matatizo.

Je, kuna hasara gani au faida watazipata upinzani?

jibu:
Hasara ni kubwa, wengi wao watakosa Ajira. Faida kwa upinzani ipo na ni kubwa, lakini sio rahisi kupimwa kwa Pesa. Wanaweza kutumia hili jambo kama mtaji wa siasa uko mbeleni.

Je, faida au hasara zipi kwa chama tawala?

Jibu:
Hasara ni kubwa kwa nchi. Siku zote watu kabla ya kufanya "Investment" au kukopesha, kuna vipimo wanaangalia. Kwa mfano, wanaweza kuangalia usalama ndani ya nchi, level ya corruption au matumizi mabaya ya jeshi.
Pili chama tawala kinaweza "kuvujisha" rasilimali za chi maana hakuna chama chochote ambacho kinaweza kupiga kelele tena, nadhani hujasahau issue Ya " Richmond". Kama unataka kujua hali itavyo kuwa unaweza kuangalia nchi kama China, North Korea au Rwanda. Serikali inaweza kuamka na kusema hakuna "Jamiiforums tena au wanaweza ku block Instagram, na hakuta kuwa na mtu mwenye uwezo wa kupiga kelele. Tatu wanaweza kubadilisha "Katiba" kuiweka vizuri ili iwe upanda wao.

Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…