Pre GE2025 Upinzani wanaweza sana kulalamika lakini hawana mipango mbadala kabisa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkuu upinzani wa africa una pitia changamoto nyingi sana , ikichangiwa kwa kiasi kikubwa na mifumo duni ya kikatiba na kisheria .

Nembo kubwa kabisa ya demokrasia ya kweli ni pamoja na vyama vya upinzani .

Katika kifungu cha 18 cha katiba yetu vyama vya Upinzani vinayo uhuru wa wa kujieleza na kukusanyika .

Je katika nchi yetu hili huwa linazingatiwa?

Hauoni kuwa kuna namna tunaenda tofauti na katiba yetu ili kuvibana hivi vyama ndio maana unaona kama wanaishia kulalamika?
 
Vyote Hivyo Huwa Wanaongea tu kama wehu hawaelezi wao kama wao wakipewa nchi watafanya nini ili mfano mfumuko wa bei usiwepo kitaalamu

Huongea kama wehu tu majukwaani
 
Vyote Hivyo Huwa Wanaongea tu kama wehu hawaelezi wao kama wao wakipewa nchi watafanya nini ili mtano mfumuko wa bei usiwepo kitaalamu

Huongea kama wehu tu makukwaani
Tatueni changamoto za wananchi mitaani wananchi wanapitia magumu , upinzani sio changamoto za wananchi.

Nyie mmejipa dhamana ya kutuongoza na kututatulia changamoto sasa kazi ni kwenu kupambania madhila mbalimbali yanayowakumba wananchi.
 
huko kwenye katiba ni mbali mno unaenda gentleman,

but ukiwa na vibrant and visionary opposition with principles and standards; kuchochea mabadiliko ya sheria au katiba ni suala la dakika sifuri tu kuliatain.....

lakini hii ya leo mnalalamikia jambo hili, halijaisha mnaliacha kesho mnalalamikia kingine, hamjapata matokeo yoyote mmehamia kulalamikie jingine with no alternative plans completely. hakuna mahali mtafika, hakuna hatua mtapiga, hamna kitu mtachochea kisaidie mwanainchi....

na hiyo dandia dandia kila kitu na kukifanya agenda, ina maanisha hamjui mnachotaka na wala jamjui mnapo taka kwenda, na hamjajipanga

my friend siasa ni kujipanga bana
 
Tatueni changamoto za wananchi mitaani wananchi wanapitia magumu , upinzani sio changamoto za wananchi.
Sema baadhi ya wananchi wanapitia changamoto sio wote

Mbowe na Lisu ni Wananchi Wana shida Gani za maisha wale .Ruzuku ya Chadema wanakula wao
 
Tatueni changamoto za wananchi mitaani wananchi wanapitia magumu , upinzani sio changamoto za wananchi.

Nyie mmejipa dhamana ya kutuongoza na kututatulia changamoto sasa kazi ni kwenu kupambania madhila mbalimbali yanayowakumba wananchi.
jukumu la kumchochea mwenye dhamana uongozi, aongeze bidii zaidi ktk kuwatumikia wanaibchi, na atishike kwamba akileta mzaha anaweza kukatatliwa na wanainchi huko mbeleni kwenye uchaguzi, ni upinzani madhubuti na altenative plans zao
 
Mkuu hiyo tabia ya kudandia dandia mambo mbona ni ya wa tanzania woteπŸ˜€πŸ˜€.

Mfano mzuri ni vitambulisho vya wafanya biashara wadogo wadogo , serikali ilikuja kwa kasi mno watu wakawa wanalipia 20 tu kwa sasa mradi huo umekufa wala hakuna maelezo yoyote ya kina yaliyotolewa .

Ndugu mheshimiwa nafikiri unalijua hilo vizuri .
 
jukumu la kumchochea mwenye dhamana uongozi, aongeze bidii zaidi ktk kuwatumikia wanaibchi, na atishike kwamba akileta mzaha anaweza kukatatliwa na wanainchi huko mbeleni kwenye uchaguzi, ni upinzani madhubuti na altenative plans zao
Hakuna upinzani madhubuti mbele ya mifumo duni ya kikatiba na sheria .
 
Unataka wapinzani wakupe njia za kutatua matatizo yako ukiwa madarakani Kisha ufanikiwe sio?

Kwanini unataka wawaze kwa niaba yako wakati wewe unalipwa mshahara, umepewa ofisi ya kutumia kutatua haya matatizo na vi 8 juu umepewa?

Hebu wapisheni hapo ofisini alafu ndio uanze kuleta hizi nyuzi kuwa hawana mbadala
 
Hakuna upinzani madhubuti mbele ya mifumo duni ya kikatiba na sheria .
hakuna upinzani unaotengenezwa na katiba friend,

bali watu makini wenye nia ya kweli na maono, mipango na mikakati madhubuti ya kuleta mageuzi kwa wanainch...
 
actually,
hizi ndizo first class brain nyingi za upinzani Tanazania zilivyo

halafu ati anajitutumua kabisa kutaka kushika dola
 
Shida ya vyama baadhi Africa iko.hapo ndio maana kushika Dola Vigumu wanaficha solutions za matatizo ya nchi wanaongea kama wehu tu kusema Kuna shida hii na hii ila solution hawatoi.

Sasa wananchi watawalewa vipi sababi hizo shida hata wao wanazijua ila solution hawajui

Sasa upinzani ukiongea tu matatizo bila kueleza wao wakishika nchi wata solve vipi wananchi watawaona hopeless tu na hawatawapa kura

Kueleza tatizo lililopo hata bwege aweza hata kama sio mwanasiasa
 
hakuna upinzani unaotengenezwa na katiba friend,

bali watu makini wenye nia ya kweli na maono, mipango na mikakati madhubuti ya kuleta mageuzi kwa wanainch...
duhπŸ™Œ kwa hiyo mkuu katiba haiwezi kushape vyama vya upinzani?πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Mkuu mfano wapo watu wawili mmoja kashika kisu anataka kukata nyama ila ameshindwa, na mwingne yupo pembeni hana kisu ila ana nia ya kukata nyama , njia rahisi zaidi ya kuikata ile nyama ni ipi apo?
 
unajua maana ya upi
unajua maana ya upinzani lakini mzee? unataka upinzani unaosifia serikali? hiyo mipango hata wakiwa nayo wataitekeleza kivipi na hawana bajeti?
 
Umenena vema sana. Kuonesha udhaifu tu wa mwingine pasina kuonesha na kuuishi uwezo wako ni kumpa umaarufu mpinzani wako. Tuache au tupunguze kila mara kuongelea habari za CCM, tuwe na habari zetu mbadala na nzuri kuliko za CCM ili kulingaishwa na kukubalika na umma na kisha kuleta mabadiliko chanya.

Mathalani, natamani tuanze kuandaa sera na mikataba mbadala ya namna ya kufaidi rasilimali zetu asilia tofauti kabisa na ilivyo sasa.
 
unajua maana ya upi

unajua maana ya upinzani lakini mzee? unataka upinzani unaosifia serikali? hiyo mipango hata wakiwa nayo wataitekeleza kivipi na hawana bajeti?
upinzani Tz unatakiwa walau kua biti kama za mandonga vs mada maugo kabla ya kuingia ulingoni
 
upinzani Tz unatakiwa walau kua biti kama za mandonga vs mada maugo kabla ya kuingia ulingoni
sasa mbona mnakimbia hadi na mabx ya kura? mwaka 2020 kura zilipigwa siku 2 kabla haya yalifanyika pale office za ccm kinondoni mkwajuni na vijana walioshiriki walipewa wali na maharagwe na waliahidiwa tsh 5000 @ ambazo hawajawah kupewa . Hapo bado hakuna upinzani. Nilikuwepo kwenye jumba la maendeleo mjini kasulu kigoma watu walifungua kituo saa 9 usiku na kujaza kura kwenye masanduku zote kwa Magufuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…