Uchaguzi 2020 Upinzani wasizuie wabunge wao kwenda kuapa na kuhudhuria Bunge

Wenye vinyongo ni wanyama na kuku wa cdm, na sio watu huru wa JMT. Imeisha hiyoooooooooooo
 
Kumbe kulitumimikia bunge ni kufaidi?
 
Wameshahudhuria tayari wa CUF , Chadema na ACT wazalendo
 
Yaani vyama vya upinzani vifanye jitiada zoote za kuimarisha demokrasia alafu siku ya mwisho chama tawala kinakuja kubaka demokrasia kwa kutengeneza matokea ya chaguzi kinacho yajua chenyewe, tena kwa mitutu ya bunduki na
toa ushihidi. Mimi nina ushahidi wa mambo yafuatayo ambao ninaweza kuudhibisha nikitakiwa kudhibitisha:

1. Siku ya kupiga kura nilikuta watu wachache sana kituoni, nilitumia dk 5 tu kupiga kura pamoja kwamba nilikwenda saa4 asubuhi. Hii ina maana kuwa watu hawakwenda kupiga kura.
2. Niliwaona wajumbe wa CCM wakipita nyumba kwa nyumba kuwahimiza wanachama wao kwenda kujiandikisha daftari la kupiga kura na kwenda kupiga kura siku ya kupiga kura, na hii ilifanyika nchi nzima.

3. Siku majina ya wapiga kura yalipobandikwa niliwaona wajumbe wakihakiki majina ya wanachama wao kama yapo kwenye orodha na kuwarahisishia kufahamu kituo watakacho kwenda kupigia kura.

Vitu kama hivi sikuviona kwa wapinzani, inawezekana kura ziliibwa lakini kama CCM wangekuwa na njia rahisi hivyo ya kupata kura basi wasingezunguuka nchi nzima kupiga kampeni, wazingetumia wasanii wengi kupiga kampeni, Rais Magufuli asingelezimika kupiga magoti kuomba kura na wajumbe wao wasinge hangaika kupita nyumba kwa nyumba kuomba kura.

Lazima tuambiane ukweli kama tunataka kupona. Viongozi wa upinzani ni wapiga dili, wangechaguliwa wao kwenye ubunge kelele zisingekuwa nyingi sana.
 
Mbona kama mnawa lazimisha si mlitaka kuwa peke yenu lakini
Unafahamu hao wabunge walitumia hela ngapi kwenye kampeni? chama kitawarudishia? je, wasipohudhuria vikao katiba itabadilishwa?
 
Nakubaliana asilimia 100 kwamba waende bungeni ni haki yao
Wabunge 19 ni wengi saana katika iboresha
Nakumbuka bunge la 2011
Walikua wanasaidia kwa kiwango kikubwa alikua mnyika, mdee, zito, wenje na wengine
Walikua hawafiki 10 lakini bunge lilikua la moto!
Waende na wachangie hoja..
 
Kwani lazima wawe wa CHADEMA?
si wachukue vyama vingine??

atakayeapishwa tunamvua uanachama, anapoteza sifa ya kuwa mbunge, tunasimamia misimamo yetu
 
Unafurahia mateso wanayofanyiwa wapinzani hapa nchini?
Hii nchi tuliyo wachiwa na baba wa taifa likiwa moja lililoshikamana leo hii mnaligawa vipande vipande kisa siasa!
Baba wa Taifa ndiye chanzo cha tatizo kwa kutuachia katiba ya aina hii, usimtaje kabisa unapoongelea masuala ya demokrasia nchini.
 
Kwani lazima wawe wa CHADEMA?
si wachukue vyama vingine??

atakayeapishwa tunamvua uanachama, anapoteza sifa ya kuwa mbunge, tunasimamia misimamo yetu
Unasahau hata Zitto alipofukuzwa na chadema aliendelea na ubunge wake hadi mwisho? atakuwa mbunge wa mahakama.

Lazima wabunge hao 19 watoke chadema kwa mujibu wa katiba na kanuni za uchaguzi. Chama kilichopata kura kwa kiasi fulani.
 
vituo hewa kibao kila kona ya nchi, kula feki kila mahali, kula tulizo piga yalikuwa maigizo ma sarakasi tuu
 

Hakuna haja ya kushiriki bunge ambalo wamesgasema uchaguzi wake uligubikwa na ukiukwaji wa kanuni na sheria za uchaguzi. Kama wameshasema huo uchaguzi haukuwa huru na wakatoa witu uchaguzi urudiwe kwanini sasa waingie huko bungeni tena
 
Kama wangechaguliwa Mbowe, Sugu na Msigwa bado wangekatazwa kwenda bungeni?

Wangekatazwa kwa wizi ule wa kule kupatikana mtaani zikiwa kwenye mabegi hata angeshinda nani huo haukuwa uchaguzi tuseme ukweli bila kumung’unya maneno
 
Unasahau hata Zitto alipofukuzwa na chadema aliendelea na ubunge wake hadi mwisho? atakuwa mbunge wa mahakama.

Lazima wabunge hao 19 watoke chadema kwa mujibu wa katiba na kanuni za uchaguzi. Chama kilichopata kura kwa kiasi fulani.
Good ila anapoteza sifa ya kuongoza Kamati za bunge,

unajua kwanini CCM wanang'ang'ania wabunge wa upinzani??
 
Baba wa Taifa ndiye chanzo cha tatizo kwa kutuachia katiba ya aina hii, usimtaje kabisa unapoongelea masuala ya demokrasia nchini.
Tatizo lako ni kutoangalia na kuelewa nini kimeandikwa
 

Hiyo hoja haina mantiki yoyote ile awamu hii serikali imeingilia moja kwa moja maamuzi ya tume ikiwa ni tangu kuchapishwa kwa ballot papers hadi sasa inaonekana ballot paper zilichapishwa kienyeji sana ndo maana zilikuwa zimezagaa mitaani kwenye mabegi haijulikani kampuni gani ilichapisha hata zile kula zilizopatikana polisi hawajatwambia upelezi wao umeonesha zilizoka wapi zile. Hii ni kasoro kubwa sana katika uchaguzi huu ambayo haijawahi tokea chaguzi za nyumba.
 
Ningekuelewa kama ungesema watafute pesa za kuwanunulia mawakala AK47 na Grenade za kujilinda wakati wanasimamia zoezi la kuhesabu kura vituoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…