Kwa miaka 5 vyama vya siasa vilipigwa marufuku kufanya siasa, kwahiyo mimi nilidhani mwaka huu na kipindi hiki cha kuruhusiwa kwa siasa wapinzani wangefanyakazi za kuvijenga vyama vyao kwa uchaguzi wa 2025 zaidi kuliko kushinda uchaguzi wa 2020. Nilitaraji wapinzani wangefahamu kuwa baada ya uchaguzi kupita siasa zitasimama tena hadi 2025, hivyo wangefanya kazi za kufungua matawi hadi kwenye vitongoji badala ya kujikita kwenye kuomba kura kwa watu ambao hawana uhakika kama walijiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na watapiga kura.
Inamaana kuwa kama Lissu angeshinda uchaguzi hii miradi ya reli, bwawa la umeme, kuhamia dodoma, meli, ndege, nk yote angeachana nayo kabisaaa. Huu ungekuwa upuuzi kwetu kwa kiwango cha lami. Maana sijawahikumsikia Lissu kwenye kampeni zake akisema atamalizia miradi hii ambayo tayari imeshatafuna hela zetu nyingi. Mimi hata kama simpendi JPM lakini napenda bwawa, dodoma iwe mji mkuu, reli ya kisasa, elimu bure, ndege, tembo wetu wasiuawe ovyo hata ikibidi kwa kuwaua hadharani wanaoua tembo. Sasa cdm walikuwa hawasemi kuhusu mambo hayo hata kidogo kwenye kampeni zao zaidi ya kulalamikia kila jambo hata yale mazuri.