Mbona jana ilani zimechambuliwa. Na sera ya wanawake imezinduliwa jana!! Mfano
1. devolution ili kuzipa mamlaka kadhaa serikali za majimbo/halmashauri kujiendesha.
2. Kuwekeza kwenye kampeni ya kuendeleza miji ili watu wasikimbilie mjini, na kupunguza regional disparities.
3. Kuhusisha zaidi sekta binafsi kwenye kusogeza uchumi mbele na serikali ibaki kma regulator tu. (Ikumbukwe agenda kuu ya chadema ni uchumi wa soko/market economy)
4. Kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kurahisisha access ya mitaji kwa graduates wasio na collaterals kuombea mkopo (Wamesema watasusha makato ya HESLB mpka 3%)
5. Kuongeza purchasing power ya wananchi kwa kupunguza mrundikano wa makato (target iwe 30% pekee ndio ikatwe kwenye mshahara/income ya mfanyakazi sio sasa ambapo inafika 48%+).
Summary tu ila ilani ilichambuliwa jana vizuri tu
Safi sana mgosi ngoja nami nigosoe.
1. Huwezi kufanya devolution kwa ajili ya kuruhusu serikali za mitaa kujiendesha.
hata hivyo serikali za mitaa kwa mfano zinajikusanyia mapato yake binafsi mbali ya ile nyongeza kutoka serikali kuu.
Kutokana na hivyo tumeona serikali nyingi za miataa zikijenga masuala kama masoko makuu na vituo vya mabasi.
Hiyo ni fedha inayokusanywa na serikali za miataa.
nafikiri wakumbuka Dodoma iliidizi kimapato Dar-es-salaam wakati fulani hata makonda akashangaa sana.
2. Uko sawa tunahitaji balance na nafikiri hiyo iko katika azma ya serikali pale ilipoamua kuwapatia wajasirimali kitambulisho na pia kuwasamehe kulipa kodi endapo mapato yao hayazidi milioni 4 kwa mwaka.
3. Ukisema "Market economy" wamaanisha kwamba kuwe na "unrestricted competition" kwenye uzalishaji na bei ya bidhaa masokoni na madukani.
Ukifanya hivyo utarudi kulekule kwenye wale wanaotaka kuingiza bidhaa zao nchini ambapo bidhaa zingine ni fake na hazikidhi ubira na zingine ni sumu.
4. tatizo la ajira lipo duniani kote hata huko USA na Ulaya hili tatizo ni kubwa sana maana vijana wa miaka 24 pia wanashia mitaani na kwa kuwa nchi hizi ni kubwa kiuchumi wana uwezo wa kuwaoat handouts hawa vijana.
hapa tatizo ni sekta binafsi kuwa tayari kuchangia uchumi wa nchi ukue kwa kbuni miradi, makampuni, viwanda na hta small workshops ili ajira au apprentiships ziweze kwasaidia hao graduates kupata uzoefu wa kazi na skills zinazohitajika.
Tatizo jingine ni kwamba vijana wanapotaka kuingia chuo kikuu wanapaswa kuangalia manufaa ya degree anayosomea sio kwa mfano mtu anaingia chuo anasomea uandishi wa habari wakati sekta hiyo ina high competetion.
Eneo kubwa ambalo bado lipo "untapped" ni kilimo, ugavi na uboharia au warehousing.
Serikali yoyote iwe CCM au Chadema ina budi kuwawezesha wakulima na hao graduates kuendesha sekta hiyo kisasa.
Lakini CCM inaye kijana Hussein Bashe ambae akiwa naibu wizara ya kilimo amejaribu sana kutengeneza mazingira ya kukiweka kilimo kiwe cha kisasa.
Tatizo kubwa sana la vijana wengi na ile "mentality" yetu waafrika ni kusoma ili uajiriwe au ujitegemee.
Huwezi kukaa tu utafuniwe kila kitu ni lazima uwe mjanja usome kozi ya kukusaidia kujitegemea na hata ukiomba mkopo benki kinaeleweka.
5. You are wrong, mimi wakati nikiwa ughaibuni nilikuwa nakatwa asilimia 20 ya mshahara wangu na baada ya hapo kuna VAT ya madukani, kuna makato ya kulipa pango, kuna kodi ya maendeleo yaani kodi ya manispaaa na ukimaliza makato hayo tusema wabakia na kiasi cha kufanya shopping, vinguo kidogo na "other miscellaneous".
Hata hivyo "purchasing power" sifahamu wazungumzia kwa wananchi wa aina gani kwani hata mradi wa umeme vijijini unakusudia kupunguza ukali wa maisha kwa kulipa elfu 27,000 tu .