Tanzania, kama taifa, kuamini kwamba tunawapenda watoto wetu, tunazidanganya nafasi zetu, ukweli hatuwapendi.
Kuna matukio mengi yenye kuthibitisha kuwa hatuwapendi watoto wetu, ama viongozi wa taifa hili hawawapendi watoto wa wanaowaongoza maana wao wa kuwazaa hawapitii mapito ya wale wanao waongoza.
Moja ya uthibitisho wa kutowapenda watoto ni uporaji wa viwanja vya michezo vya shule kwa kuvitumia kwenye shughuli zingine zisizohusiana na elimu na miongoni mwa viwanja hivyo ni pamoja na ule wa Shule ya Msingi Luanda Nzovwe jijini Mbeya.
Hivi sasa ndio uwanja wa mikutano ya kisiasa, mahubiri, maonyesho na matamasha mbali mbali, yote hayo yakifanyika hadi nyakati za masomo.
Hivyo pamoja na kuwanyima haki yao ya kutumia viwanja vyao kwa ajili ya michezo, huvuruga usikivu wao wawapo madarasani wakiendelea na masomo kutokana na kelele pamoja na watoto kutamani nao kuona yanayoendelea nje.
Rais Samia, ukiwa pia mama, ingilia kati kwa kuzuia huu unyanyasaji wa watoto.