Nimejaribu kusoma kwa utulivu lakini sijapata logic ya hoja yako...
"Threat" ya kitu huzuiwa kabla ya matokeo. Huwezi kusubiri athari/matokeo yatokee ndiyo useme kitu au mtu fulani ni "threat" na kuanza kupambana nacho/naye...
Unajua kilichotokea ktk uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019...?
Na unajua kilichotokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana 2020, au siyo?
Unatafsirije ujinga na uchafuzi huo kwa kuitazama kesi hii ya Bwana Freeman Mbowe?
Hii sasa ndiyo inakuja maana ya ile statement ya Advocate Kibatala aliyowaambia mawakili wa serikali/jamhuri kuwa, "wanatanguliza mkokoteni/toroli mbele ya punda au farasi...!"
Kwenye kesi hii, wale vijana sijui kina Bwire, Adamoo na Ling'wenya katika ni "chambo" tu lakini atakiwaye kuchinjwa hapo ni mwamba...!
Swali ni; WATAWEZA????