Upotoshaji mkubwa sana unaoenezwa Mbowe amebambikiziwa kesi kwasababu ya mambo ya kisiasa

Upotoshaji mkubwa sana unaoenezwa Mbowe amebambikiziwa kesi kwasababu ya mambo ya kisiasa

Nauona upotoshaji mkubwa sana unaoenezwa mitandaoni na mitaani kuwa ndugu Mbowe amebambikiziwa kesi kwa sababu ya mambo ya kisiasa. Mi nadhani kama kweli ingekuwa hivyo basi alikuwa tishio awamu za nyuma kwani nakumbuka huko nyuma Chadema pekee kiliwai kuwa na wabunge 70 na ushee ambapo kisiasa unaweza sema chama na Mbowe ilikuwa threti kwa serikali na chama.

Leo hii tunaongea Chadema kinambunge 1 tu wa kuchaguliwa sawa na CUF. Mi nadhani Chadema kwa kuwa wamekuwa wakiupongeza sana huu muhimili wa mahakama nashauri watulie na kuiachia mahakama ifanye kazi yake na kuja na majibu kwani hapa Tanzania Mahakama ndiyo chombo pekee kinachotoa haki kwa mujibu wa katiba.

Na kwakuwa uko mwanzo Chadema walituaminisha kuwa mama Samia yuko safi, watulie kwani tulisha waamini hivyo kubadili gia kila mara si vizuri. Mi naamini kuwa mahakama itatenda haki na serikali haikurupukagi kama iliona viashiria vya uvunjifu wa amani haiwezi kukaa kimya kuacha kutulinda wananchi wake na mali zetu hivyo tusitoe povu mahakama itatenda haki kama ilivyotenda kwa Sabaya.
Ccm inawabunge wangapi wakuchaguliwa.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom