Upotoshaji wa Kauli ya Rais Ukomeshwe. Wizara ya Afya Toeni ufafanuzi

Gts,

Inasikitisha sana tena sana jamii inapoendelea kupotosha kauli ya Rais juu daktari aliyegeuka mkataba.

Wizara ya afya toeni ufafanuzi.

Inavyofahamika, ukiwa kazini halafu ukasomeshwa na Serikali huwa kuna mkataba wa kufanya kazi Serikalini kwa muda maalumu baada ya hapo mhusika huwa huru.

Hivyo tamko la Rais lipo sahihi.

Hebu tupate kwanza tafsiri ya "kusomeshwa na serikali" ni ipi...

Je, ina maana ya kupewa mkopo kwa 100% ndo tafsiri ya kusomeshwa na serikali?

Kama kwa "kukopeshwa" ina maana ya "kusomeshwa na serikali" inawezekanaje pesa hiyo uliyolipiwa na serikali ukasoma iwe ni "mkopo" na mnufaika alazimike kurudisha mkopo huo na wakati huo huo afungwe na masharti ya kufanya kazi ktk taasisi za serikali pekee?

HATA HIVYO;

Hii inawezekana tu kama hawa madaktari bingwa walilipiwa gharama zote za kusoma kwao kwa masharti ya mkataba kuwa watafanya kazi ktk hospitali za serikali pekee kwa muda fulani au ktk maisha yao ya kazi yote...

Kama kuna mkataba Wa namna hii, basi madaktari hao waliokimbia na kwenda kufanya kazi kwenye hospital za binafsi, wamekiuka mkataba. Serikali ina haki ya kuchukua hatua za kisheria....

Lakini kama walisoma kwa mikopo hii hii ya kawaida ya HESLB, basi hawafungwi na sharti lolote la kufanya kazi kwingine....!!
 
Huyu Dr nikwamba kasomeshwa na serikali au kapewa mkopo na serikali...mm nimmoja wa wanufaika wa mkopo ila sijawai saini mkataba kama huo....hebu anaejua atueleze hapa kuwa huyu Dr alipewa grant na serikali au mkopo 100% ambao nilazima aulipe awe serikalin au private
 
Mkuu uwe na heshima na mwenyekiti wetu, mbona nyie tunawaheshimu.
Mkuu kama huyo Daktari alimaliza muda wake kisheria nadhani yuko sahihi. Nilidhani unajua muda aliofanya kazi baada ya shule na kabla ya kuhama
 
Pumbavu kabisa, hiyo umeipata katika sheria au kanuni gani?

Mkataba wa kufanya kazi serikalini kwa miaka mitano ndipo muhusika awe huru ulikuwepo wakati inasomesha watu bure na kuajiri wahitimu wote. Hivi sasa watu wanalipa ada ama kwa fedha zao au mikopo.

Hivyo wizara haina majibu wala hoja ya kufafanua.
Kuna mkataba kwa madaktari walioajiliwa serikalini wanaojiendeleza na masters kupitia ufadhili wa serikali wakimaliza wanatakiwa kurudi kazini au kupangiwa kituo kingine Cha kazi kwa miaka 2.
 
Hebu tupate kwanza tafsiri ya "kusomeshwa na serikali" ni ipi...

Je, ina maana ya kupewa mkopo kwa 100% ndo tafsiri ya kusomeshwa na serikali?

Kama kwa "kukopeshwa" ina maana ya "kusomeshwa na serikali" inawezekanaje pesa hiyo uliyolipiwa na serikali ukasoma iwe ni "mkopo" na mnufaika alazimike kurudisha mkopo huo na wakati huo huo afungwe na masharti ya kufanya kazi ktk taasisi za serikali pekee?

HATA HIVYO;

Hii inawezekana tu kama hawa madaktari bingwa walilipiwa gharama zote za kusoma kwao kwa masharti ya mkataba kuwa watafanya kazi ktk hospitali za serikali pekee kwa muda fulani au ktk maisha yao ya kazi yote...

Kama kuna mkataba Wa namna hii, basi madaktari hao waliokimbia na kwenda kufanya kazi kwenye hospital za binafsi, wamekiuka mkataba. Serikali ina haki ya kuchukua hatua za kisheria....

Lakini kama walisoma kwa mikopo hii hii ya kawaida ya HESLB, basi hawafungwi na sharti lolote la kufanya kazi kwingine....!!
Kama ulienda kusoma ukiwa mtumishi wa umma, mkataba unakufunga na uko wazi. Muda wote unapokuwa shule kumbuka serikali inakulipa mshahara. Tatizo hatujui alikuwa ameshafanya kazi kwa muda gani baada ya shule
 
Kuna mkataba kwa madaktari walioajiliwa serikalini wanaojiendeleza na masters kupitia ufadhili wa serikali wakimaliza wanatakiwa kurudi kazini au kupangiwa kituo kingine Cha kazi kwa miaka 2.
Na pia kuna guarantee ambayo serikali inatakiwa kutoa kwa ye yote ambaye atajiendeleza kupitia ufadhili wa nchi nyingine au mashirika ya kimataifa.
 
Gts,

Inasikitisha sana tena sana jamii inapoendelea kupotosha kauli ya Rais juu daktari aliyegeuka mkataba.

Wizara ya afya toeni ufafanuzi.

Inavyofahamika, ukiwa kazini halafu ukasomeshwa na Serikali huwa kuna mkataba wa kufanya kazi Serikalini kwa muda maalumu baada ya hapo mhusika huwa huru.

Hivyo tamko la Rais lipo sahihi.
Sasa kama unafikiri Magufuli alieleweka kwanini unataka Wizara ifafanue?

Likilaza lenu mtalitetea mpaka mtaenda kaburini lenyewe lipo tu
 
Gts,

Inasikitisha sana tena sana jamii inapoendelea kupotosha kauli ya Rais juu daktari aliyegeuka mkataba.

Wizara ya afya toeni ufafanuzi.

Inavyofahamika, ukiwa kazini halafu ukasomeshwa na Serikali huwa kuna mkataba wa kufanya kazi Serikalini kwa muda maalumu baada ya hapo mhusika huwa huru.

Hivyo tamko la Rais lipo sahihi.
We umeona wapi huo mkataba ? Mkataba unasema kufanya kazi Tanzania miaka mitano , kwani private ni Burundi ?
 
Kama mikataba ya nyongeza za mishahara na kupanda madaraja kwa watumishi wa umma inavunjwa, daktari yeye ni nani hadi asivunje mkataba ambao unahusu maslahi yake na familia yake.
 
Kina mollel, ndugulile, gwajima, et al wao hawakusomeshwa na serikali? Mbona hawapo kwenye vituo vyao vya kazi? Au huko kwenye ukumbi wa binge ni hospitali? Acheni ubaguzi ninyi!
Hili swala linakuzwa sana na Chadema.

Mfano Dr Kigwangalla yeye alisomeshwa na WAMA ndio maana serikali haikushughulika naye.
 
Hivi wewe mataga hiyo hospital binafsi inahudumia fisi hadi mwenyekititi wako wa ccm anaagiza ifungwe???

Yani bora ukae kimya aisee.
gharama ya hospitali binafsi na ya serikali kwenye huduma za kibingwa zinafanana? acha uzwazwa...rais anatetea wanyonge wasio weza kumudu gharama za matibabu huko private
 
Ni kunguru maji tu ndiyo ataunga mkono maamuzi ya kuifunga hospital binafsi kwasababu daktari ameamua kuacha kazi serikalini na kwenda kwenda kwenye hiyo hospital binafsi.
 
gharama ya hospitali binafsi na ya serikali kwenye huduma za kibingwa zinafanana? acha uzwazwa...rais anatetea wanyonge wasio weza kumudu gharama za matibabu huko private
Mh! Kaka bora kukata kimya tu. Usiongee vitu usivyovijua. Nenda kafanyiwe upasuaji wa figo muhimbili Na Bugando au kCMC halafu ulete mrejesho Kama gharama ni tofauti.
Kikubwa Ni kuwa huko hospitali binafsi nako anahudumia raia. Hebu jiulize kea Nini Magufuli aliacha ualimu akaenda kwenda siasa, tena hata kwenye siasa mara kadhaa anapita bila kupongwa. Hilo sio suala kubwa kwa kuwa kote anahudumia raia. Kwa hiyo kwenda binafsi au serikali wote wanyonge wanahudumiwa.
 
Back
Top Bottom