Upotoshwaji unaoendelea kufanywa na baadhi ya Wafamasia kumpotosha Waziri wa Afya

MDs wapumbavu sana time for slavery is over
 
P
Prof ni wahuni tu waliokujibu, upo sawa kabisa Waziri fuata ushauri huu itakusaidia,
 
Mtoa mada yupo kwa ajili ya kuongea mambo ambayo hayajui..
Nani kakwambia mfamasia haruhusiwi kufanya drug administration?
Nenda nchi za Uganda / SA hata nje la bara letu..
Nani kakwambia Mfamasia hajui diagnosis..?
Ndio maana unaweza ukakutana na kituko cha daktari wa watoto wanaandika dose za ajabu kwa watoto na kuleta uharibifu kwenye figo.. Wao ni kuandika tuu dawa mchanganyiko zisizo endana..
Hivi wewe unajiita prof sijui kokoto..
Unaweza kumuandikia mtoto mchanga IV Gentamycin 80mg ...? Tena masiku ya kutosha?
Hao ni madaktari tena specialist?
Hivi hamuoni mnaaribu figo za watoto?
Mnakazana kuzunguka nchi nzima / Wizara ya Afya mnasema hakuna Malaria...
Juzi hapa Mtoto kaletwa Muhimbili kutoka Temeke Hospital na ambulance.. Just mnakazana na kusema hii sio malaria.. Ni degedege...
Hivi nyie mnataka kuuwa watu?
Mtoto temp ipo 38 haishuki.. Akila anatapika.. Anatetemeka.. Mnakazana na Carbamazepine na Paracetamol kisha mnamwambia mama yake akatafute huko nje dawa ya kuzuia kutapika...
Mnakimbilia kupima mRDT badala ya field stain kuprove parasite wa malaria...
...mRDT haiwezi kuonyesha malaria.. Na ikionyesha hiyo ni severe tena inaweza ikawa cerebral malaria. ...
Wewe prof.... Waambie wenzako.. Mtakuja kuendelea kuuwa watu kwa poor management.... Na kujidai nyie mnajua mambo wakati.. Au basi
 

Profesa upo sahihi Kabisa.

Endelea kupaza sauti
 
Professor nchi zingine wanafanyaje? eg Marekani, U.k n.k?
Tatizo la Tanzania linakwenda deep na ni very complicated! Huu mgangano umetokea kwa sababu ya hali mbaya ya uchumi kwa madaktari na mafamasia. Ni kwamba daktari kazi yake tu haiwezi kukidhi mahitaji yake ya maisha. Na mfamasia hivyo hivyo. Matokeo yake wanagongana kwenye kutafuta namna ya kutosheleza kipato. Chanzo cha haya ni nini? Uongozi wa nchi mbovu! Listen, suala la mfumo mbovu wa uongozi wa nchi yetu lina athari nyingi sana katika maisha yetu. Hata wafanye nini kujaribu kurekebisha, ukweli ni kwamba bila ku-deal na kiini cha tatizo i.e. mfumo na uongozi mbovu, ni bure.
 
Ujinga mtupu umeandika.


Wewe badala ya kujikita katika hoja, unatanguliza porojo ??.

Yaan Mtu kafanya, MD, MMED, alafu unainua pua yako , Et 'Hawana interaction na wagonjwa ?".


Hilo Bichwa lako, kafugie minyoo .
Anatomy
 

Sasa Kama MD alisoma kozi ya Microbialogy na namna ya kutumia Vifaa Kama Microscope ulitaka asiangalie vipimo Kama kuna uhaba wa lab Technician?

Unafikiri miaka mitano wanasomea vitu gani?
Yaan wasome vitu vingi Kwa miaka mingi alafu wasitumie maarifa waliyoyapotezea muda na pesa kisa kuna watu wengine wanaingiliana majukumu.

Muhimu; Tanzania kwenye sekta ya Afya bado kuna uhaba WA watenda kazi, kugawana majukumu ingefaa watendakazi wakishakuwa wengi
 

Huyu Jamaa atakuwa ni Daktari wa Mchongo na niabu kuwa na wasomi kama hawa na anachopigana nacho ni kitu ambacho hakiwezi kuja kutokea, sio kwa Tanzania tu, duniani kote.

Daktari anajua Dawa au anakariri Dawa ya kutibu ugonjwa?

Yaani nesi ndio atoe Dawa ? Huyu jamaa ipo shida kwenye akili yake. Usimamizi wa dawa duniani kote ni Mfamasia, mpaka kwenye Pharmacy na kuna nchi za watu Pharmacy inasomwa na Magenius, kama Mfamasia anaweza aka omit hicho kilichoandikwa kwenye cheti cha mgonjwa na kumshauri huyo unayemuita Dr dawa sahihi ya kumpatia mgonjwa.

Shida kubwa ya huyu Dr wa mchongo hajui majukumu ya Pharmacist ; Hivyo aelimishwe.

Ikija prescription kwanza inatakiwa ikaguliwe na pharmacist ndio iende despensing bay , Kama Pharmacist hajaridhika.... inarudi kwa huyo Dr with recommendations nini cha kuandika au kufanya....,dawa sio maembe kwamba utatoa kama roboti.

Ni aibu kubwa Dr kama huyu kuandika kitu kama hichi. Yaani katika maisha yake yote hajawahi kujua majukumu ya Pharmacist , Nesi na Dr .... ni aibu sana .Hawa ndio wanaoua wagonjwa maospitalini kwa kukosa weledi.

Hakuna Dr au Nesi anaejua dawa zaidi ya famasia; famasia anaanza kukutengenezea wewe Dr dawa na kukuwekea magonjwa yatakayotibu na kuja kukuelekeza namna ya kutumia.... Wewe kazi yako ni final .... baada ya kujua mgonjwa anaumwa nini , chungulia dawa ya kumpa na wafamasia ndio wanaweka miongozo na dose za hizo dawa kuanzia tangu kiwandani. Yaani ni aibu kusoma andiko la huyu Dr wa mchongo.

Addo ni upuuzi , na haya mambo ya ADDO huyakuti kwenye developed country. Matumizi ya hovyo ya Dawa bila ya Ushauri wa famasia ikiwemo na hizo Addo yamesababisha nchi yetu kuwa na wagonjwa wengi mno wa figo, ini na kansa.

Kama ulikuwa hujui, ajali zinazotokea kwenye matumizi ya Dawa kwa Tanzania kwa kukosa ushauri wa famasia ni nyingi kuliko ajali za barabarani.


Kama unadhani kwamba mfamasia kazi yake ni kutoa dawa kwa mujibu wa cheti Kama vile unatoa biskuti, unatakiwa kurudi shule upya maana hujaelewa majukumu yako ya msingi na hii ndio tatizo la kuongezeka vyuo vya afya vingi ambavyo havina vigezo na vipo kibiashara matokeo yake ni kuzalisha jamii ya huyu dokta wa mchongo
 
Unachekesha sana.yani daktari aende kusoma addo? Hahahaa!! Siku moja nilimfelisha interview mtu mmoja kwa kishindwa kujibu swali langu.Tena hawa wauza madawa wanaumiza watanzania kwa kutoa wrong dose kwa wateja wao.eg : azithromycin kwa magonjwa ya kawaida ni only for three days!! Siku mmoja nilibishana na hawa wanaojiita dispensors bila kujua kuwa Mimi ni daktari
 
Muwe mnajitahidi kuficha ujinga wenu.


Kwa Maisha ya Watanzania walio wengi, ambao huishia kujitibia wenyewe Kwa kwenda kununua sawa bila kujua wanachoumwa.


Kumtoa Daktari , na kumwacha Mfamasia ,ni UJINGA ULIOPITILIZA.


Mimi hapa Kila siku lazima nipate SIMU za wafamasia wakinipa maelezo ya wateja wao na wakihitaji kujua Nidawa gani wawepe.


Mfamasia anajua Dawa, lkn Daktari anajua ni Dawa gan amwambie Mfamasia ampe Mgonjwa .
 
Professor kama upo serious anza na ushauri wa katiba mpya maana hii nchi imeoza sababu ya mifumo mibov

Wapo wengi mno wataalamu lakini MD wamekua wakiona kua wao ni muhim sana na wanaweza kila jambo.

KIKUBWA kaz zigawanywe kwa kila mwenye mamlaka husika na sio kujitoa ubeparii kwenye sector hii

Watu wa afya ttzo kubwa hatuelewani kabisaa,

Imani yangu wataalamu ni wengi ila ubepari ni mkubwa sana.
 

Tatizo Lenu watu wa Afya ni kujiona Bora mkidhani mnaakili kuliko Kada zingine kumbe sio kweli.

Siku zote watu wanaojiona Bora na wabaguzi hubaguana wao Kwa wao.

MD anamdharao CO
MD anamdhaeau Nesi
CO anamdharau Nesi
MD anamdharau Mfamasia

Kusoma yote sio kufanya majukumu yote,

Wanabaguana Kwa sababu ya akili ndogo ya kutotambua kila mmoja ananafasi yake
 
Mkishakuaga na na vielimu uchwara ,mnavimba sana.


Sasa hiyo IV Gentamicin 80mg, na Mtoa mada wapi na wapi???.


Ulivyo Mpuuzi,Et 'Tena specialist ?!!.


KIHALISIA, KATIKA AFYA, DAKTARI ni Mfamasia, ni mtu wa Labo .


DAKTARI HAMHITAJI MFAMASIA...MFAMASIA LAZIMA AMUHITAJI DAKTARI.
 
Nafikiri wewe ndiye huna akili kabisaaa.yani mfalmacia atoe dawa kwa mgonjwa? How? Amesomea wapi anatomy? My dear friend ,dawa siyo maharage aisee!! lini mfamacia amesomea ABCD ? Yani airway, breathing, circulation and drug! Unaweza kutoa dawa kwa mgonjwa akakuzimikia !sasa unajua utamsaidiaje? Nurse na dakatari wanajua namna ya kumsaidia mgonjwa after any side effect from the admistered drug!! Addo na mfamacia wanavijulia wapi? Kitu ambacho daktari hawezi ni kutengeneza dawa na siyo kutoa dawa!! Full stop.so daktari haitaji kusoma Ado au au full pharmacy. Madakatari na manesi wanasoma pharmacology
 
Broo Hawa Baraza la madaktari wajitathmini sana , hawaheshimu kaz za wenzao wengine HASa wafamasia .
 
Mimi taaluma yangu tofauti pamoja na hivyo nimeelewa kiasi... ila jambo moja nakuomba profesa.
Kule umeshindwa kueleza kwa kiswahili hadi umetumia kingereza rudi jielimishe lugha kisha ututolee kwa kiswahili. Ni ombi tu ukipenda. Ukipotezea pia sitakulaumu.
 
Mkishajiona sijui MD kazi kudharau fani nyingine....
Kama daktari hahitaji mfamasia basi awe anakaa na dawa chumbani kwake...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…