HITIMISHO: Mfamasia atengeneze dawa kiwandani, ahifadhi dawa,atoe na kusambaza dawa. Si kazi yake kuchukua history na kubaini ugonjwa kisha atoe dawa. Atoe dawa kwa maelekezo ya daktari kama taratibu zinavyosema, Pharmacies ziuze dawa kwa vyeti vya madaktari. Awepo daktari au nesi katika Pharmacy yeyote ile ili wasaidie kutoa dawa moja kwa moja kwa wagonjwa, huu ndio wajibu wao. Hakuna tatizo lolote nesi au daktari kuuza dawa maana hakuna hoja ya msingi ya kuzuia hili. Hata mahospitali za Wilaya nyingi tu na vituo vya Afya nchini Tanzania Nurse assistants ndio dispensers na hawana mafunzo ya ADDO.
EeeeenHeeee Heeeee Heeeee!
Imenibidi leo nitoe kile kicheko changu cha kawaida baada ya kusoma kimakini hili andiko la huyu kijana ambaye bado ndio kaanza shughuli za kiutibabu. Bado ana ule msisimko wa sisi zaidi kuliko wao, kama vile Simba na yYanga; kumbe anayoyazungumzia ni maswala nyeti sana yanayohususu maisha ya mteja wao wote, ambaye kwa kweli ndiye BOSS wao wote, ambaye ni mgonjwa. Bila ya ushirikiano wa mgonjwa, huu usimba na uyanga kati yao hauna maana yoyote.
Baada ya kusoma, nimejiridhisha, hakuna mtu anayejiita "Profesa Patrick Koboro" mwenye 'credentials' za MD, MMED, MPH, MBA, PH.D., n.k..
Mtu huyo hayupo. Huyu anayeandika hapa ni kijana tu asiyekuwa na ufahamu wa muundo wa hizi taaluma za Udaktari na Ufamasia, na wala hajishughulishi kutaka kujua kwa nini muundo huo ulivyo kama ulivyo sasa, si kwa Tanzania pekee, bali duniani kote.
Tena, inawezekana sana hata asiwe mtu aliyehitimu na MD, inawezekana sana hata akawa ni clinical ofisa tu au mtu tu aliye na maslahi na hiyo ADDO, ambayo imemchanganya sana kiasi kwamba anasahau kuwa ADDO ni sehemu ndogo sana katika mpangilio wa huduma za afya hapa nchini.
Baada ya kugundua haya, sioni lazima ya kufafanua hatua kwa hatua yote aliyoyaandika, labda tu kwa ufupi nikazie haya yafuatayo.
Famasia na Udaktari ni taaluma mbili tofauti, lakini zinazotegemeana. Huwezi kusema Famasia inatokana na au ilikuwa tawi la utibabu, kwa hiyo ni lazima utegemee mzazi kwa uwepo wake.
Hao aliowataja kama waanzilishi wa taaluma hizo mbili, yeye kaamua kuwachukuwa wawe upande wake, lakini hataki kukubali kwamba walikuwa pande zote toka mwanzo kabla ya mgawanyo wa taaluma hizi.
Inafaa pia atambue kwamba tokea wakati huo, hadi sasa, pamekuwepo na mabadiliko makubwa sana, kiasi cha kwamba huwezi kuhusisha taaluma moja kuwa kisehemu cha taaluma nyingine, na mabadiliko ndiyo yanazidi kupamba moto wakati huu na haya maswala yanayojitokeza ya "individualized therapy" na maswala mazima ya Biotechnology inavyochukua nafasi yake. Hata huko kwenye utibabu kwenyewe, si swala tena la sisi ni madaktari. Watu wanajipambanua katika fani hiyo hiyo na kufanya vitu vya kipekee kabisa ambavyo wengine hawafanyi.
Kulilia kuwa sehemu ya kuuza madawa wakati huu, na kuacha kushughulikia kazi inayokuhusu ya kumhudumia mgonjwa katika utambuzi wa kinachomsibu mgonjwa, maana yake ni kwamba anatafuta kukimbia kazi anayotakiwa kuifanya kwa ufanisi na kwenda kufanya kazi ambayo hahusiani nayo kabisa.
Kama hapo mwanzo ilionekana kuwepo umuhimu wa kutenganisha majukumu ya udaktari na mambo ya kushughulika na dawa, iweje sasa wakati huu tena huyu kijana alilie kuongezewa majukumu zaidi, wakati hata yale aliyosomea bado hayamudu?
Weka 'focus' kwenye kazi yako uliyosomea, uifanye kwa ufanisi zaidi, hayo ya akina Famasia, himiza tu, na wao wafanye ya kwao kwa ufanisi
Ninakubaliana naye juu ya uozo mwingi uliopo huko ndani ya taaluma ya Famasia unaotakiwa kushughulikiwa na kunyooshwa, lakini siyo swala la kuleta tena tabaka jingine kwenye uozo huo huo. Hilo siyo suluhisho la tatizo hata kidogo.
2. Mara nyingi huwa sipendi kuandika magazeti marefu katika ukumbi huu. Kwa hiyo inanilazimu niishie hapa kwa sasa.
Ikilazimu, nitaweka bandiko jingine la mwendelezo wa hapa nilipoishia.