SoC02 Upungufu wa nguvu za kiume na kuwahi kumaliza kwa mwanaume wakati wa tendo la ndoa

Stories of Change - 2022 Competition

Hosea Ben

Member
Joined
Sep 22, 2014
Posts
69
Reaction score
15
Upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo gani?

Upungufu wa nguvu za kiume ni tatizo ambalo linahusisha kukosa uwezo wa kusimamisha uume au kushindwa kudumisha uume ukiwa umesimama wakati wa kushiriki tendo la ndoa. Hili ni tatizo la kihisia na kimwili ambalo linaweza kuhusisha matatizo ya kisaikolojia na kiafya kwa mwanaume na kusababisha uume kukosa uwezo wa kusimama kikamilifu ili kushiriki tendo la ndoa na mwanamke. Hii ni ya kiafya ambapo kwa kawaida huwaathiri wanaume wenye umri mdogo hasa ikiwa wana hali ya kiafya inayosababisha kushindwa kusimamisha na kudumisha uume. Pia kuna mambo ya kisaikolojia amabyo yanaweza kuathiri uwezo wa mwanaume kusimamisha uume. Utafiti unaonyesha kuwa takribani 40% ya wanaume huathiriwa na ukosefu wa nguvu za kiume wakiwa na umri wa miaka 40 na karibu 70% ya wanaume huathiriwa wakiwa na umri wa miaka 70.

sababu za tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Katika hali nyingi; upungufu wa nguvu za kiume hutokea wakati mtiririko wa damu kwenye uume ni hafifu. Hali hii inahusishwa na matatizo ya kiafya yanayotokana na magonjwa kama vile kisukari, ugonjwa wa figo, uti wa mgongo, kiwewe, unene kupita kiasi.
sababu zingine ni pamoja na mambo ya kisaikolojia kama vile mfadhaiko, wasiwasi. Pia kuwa na kiwango cha chini cha homoni ume yaani testosterone hormone kunaweza kusababisha tatizo hilo.

Njia za kutatua tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

Zifuatazo ni baadhi ya njia ambazo hutumika kukabiliana na matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume;
Moja, Kupunguza msongo wa mawazo.

Mawazo na mfadhaiko hupunguza na kuzuia mtiririko wa damu kwenye uume na kusababisha uume kushindwa kusimama.

Pili, Kutibu magonjwa yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume mfano kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la damu au uzito kupita kiasi.

Tatu, Kuacha au kupunguza matumizi ya vilevi. Matumizi ya vilevi husababisha tatizo la nguvu za kiume.
Nne, Kufanya mazoezi ya viungo. Mazoezi ya viungo husafisha mishipa ya damu na kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenye uume.

Tano, Kula vyakula vinavyoongeza nguvu za kiume kwa haraka. Mfano; Ndizi mbivu; hii husaidia kujenga misuli ya mwilini na kutengeneza stamina ya tendo la ndoa. Tikitimaji; husaidia kuimarisha misuli ya mwili na mfumo wa fahamu kufanya kazi vizuri. Jitahidi kula vipande viwili au vitatu. Parachichi; hii huongeza uwezo wa kufanya tendo la ndoa na kuleta msisimko mkali wakati wa kufanya mapenzi. Pilipili; hii husaidia mzunguko mkubwa wa damu na kuleta hisia kali ya mapenzi.

Inaweza kuchanganywa kwenye chakula au kula hivyo hivyo. Maji ya kunywa; inatakiwa kunywa maji mengi kwa siku. Tangawizi; chemsha tangawizi na utumie kama chai asubuhi, mchana na jioni. Hii husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini na kuwezesha uume kupokea damu ya kutosha. Asali yenye mdalasini. Hii huongeza kinga ya mwili, nguvu za mwili na nguvu ya ubongo kwa pamoja.

Tatizo la kuwahi kumaliza wakati wa tendo la ndoa

Tatizo la kuwahi kumaliza kwa mwanaume wakati wa kufanya mapenzi ni hali ambayo inatokea kwa mwanaume kuwahi kumwga shahawa mara tu anapoanza kushiriki tendo la ndoa na mwanamke; hali hii inaweza kutokea kati ya sekunde thelathini (nusu dakika) na dakika tatu. hali hii humfanya mwanaume ashindwe kuthibiti kutoka kwa shahawa wakati wa tendo la ndo kwa sababu ile misuli inayomfanya mwanaume achelewe kumwaga huwa imeshalegea na haina uwezo tena wa kuthibiti shahawa kutoka mapema.

Njia za kuondoa au kutibu tatizo la kuwahi kumaliza wakati wa tendo la ndoa kwa mwanaume.
Misuli inayohusika na kusimama kwa uume na kuwahi kumaliza wakati wa tendo la ndoa inapokuwa dhaifu hukosa uwezo wa kuthibiti shahawa kutoka kabla ya wakati husika.

Wataalamu wa afya ya mapenzi wamethibitisha kuwa zoezi liitwalo "physiotherapy" yaani mazoezi yanayohusisha misuli ya uume ndiyo hurudisha uwezo wa nguvu za kiume za asili, zoezi hili halina madhara yoyote kiafya na linaweza kufanyika wakati wowote.

Jinsi ya kufanya zoezi hili: Ukiwa umekaa kuwa kama mtu aliyebanwa na mkojo halafu kuwa kama unabana mkojo usitoke kwa kuhesabu hadi mara 20 (sawa na sekunde20) halafu achia na bana tena. unaweza fanya zoezi hili hata kwa dakika 8 au 10 baadae unapumzika na kusubiri muda mwingine. Pia unapokuwa unakojoa usiachie mkojo wote kwa wakati mmoja badala yake achia kidogo kidogo kisha bana. unaweza kubana hata mara 3 au 4.

Faida ya zoezi hili husaidia mzunguko wa damu kuingia kwenye uume na kufanya uume utanuke na kuwa na nguvu zaidi. Pia inaifanya misuli ya uume kuwa imara na kuweza kuzuia shahawa kutoka mapema.

Mwisho, nina imani makala hii itakuwa msaada wa kutatua tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na kuwahi kumaliza wakati wa tendo la ndoa.
 
Upvote 5

Kegel nzur kiafya
 
Back
Top Bottom