Urafiki kati ya mwanaume na mwanamke yaani kaka na dada unawezekana?

Urafiki kati ya mwanaume na mwanamke yaani kaka na dada unawezekana?

Gaddaf i06

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2022
Posts
1,770
Reaction score
2,841
Kwa kuheshimu muda wako, ngoja niandike kwa ufupi sana.

Je, urafiki kati ya mwanaume na mwanamke tena mke wa mtu, unaojionyesha kwa code ya "Kaka" na "Dada" huwa upo kweli au kuna kitu kinafunikwa hapo?

Ndugu yangu, sina sababu ya kuelezea kilichofanya niulize swali hili hapa, lakini bila shaka umenielewa. kila nikilitafakari sana jambo hili, sipati jibu linaoridhisha nafsi yangu.

Wewe unasemaje?
 
Je, unadhani huyo mwanamke atachagua kusimama upande wa nani kati yako (mume) na huyo rafiki yake, ikiwa utaamua kuchukua hatua?

Je, huyo rafiki yake wa kiume ameoa kama wewe au bado ni mzurulaji tu?

Hayo ndio maswali ya msingi ukitaka kutatua huo ujinga.

ILA

Nasikitika kusema kuwa hauna mamlaka juu ya huyo mke wako, ni either wewe ndo unampenda sana na hauwezi kuwa mbogo mbele yake kwa kuhofia atakuacha, kiasi cha kushindwa kusimamia uanaume wako, kama ni hivyo basi hakuna kitu unaweza kufanya zaidi ya kukaza moyo.

Urafiki wa namna hiyo unaweza kuwepo ila kama hauridhishwi nao, kwanini usichukue hatua? Hasa kama huyo jamaa hana mke.
 
Binafsi naamini inawezekana kwa asilimia zilizo nyingi, ingawa hapo ili iwe hivyo mmoja wa marafiki anatakiwa awe anaongozwa na akili na sio hisia.

Lakini sioni haja ya kuwa na urafiki wa damu damu na jinsia kinzani nawe kwa sababu saa yoyote na muda wowote mnaweza mkaongea lugha nyingine.

Hili mimi binafsi nikiri nitaliweza kwa asilimia ndogo sana, kuna mvutano mkali sana baina ya me na ke kinachoweza kuleta ukinzani ni ule undugu wa damu.
 
Hakuna urafiki wa me na ke wenye mawasiliano ya ukaribu wa mara 4/7 kwa wiki ambayo yalishawahi kuwaacha salama wahusika, ke atatumia nafasi hiyo kujipatia vitu vidogovidogo km vocha na me atatumia mwanya huo kumkula then anajitoa na kuomba radhi "i didn't mean it, sorry, ni shetani tu"
 
Mkuu uwezekano ni mdogo Sana,popote anapokuwepo mwanamke na mwanaume ambao sio ndugu shetani huwa WA watatu wao

Kama huyo ni mkeo hakikisha unaweka mipaka Kati Yao, huo urafiki sio salama,na kibaya Zaidi wanaweza kutumia urafiki huo ambao wewe unautambua wakala tunda la Kati Kati.

Shtuka fasta mkuu!
 
Mmnh! Wakuu asanteni kwa michango yenu.

Kuna mtu hapo juu amesema kwamba huenda sina sauti. Hawa wanawake kuna muda huwa wanatest mitambo!! hebu ngoja niendelee kuhesabu kura za maoni kwanza.
 
Back
Top Bottom