Salaam wanaJF!
Katika kipindi kirefu sana kumekuwa na mjadala juu ya kuruhusu uraia wa nchi mbili 'dual citizenship' katika taifa letu. Mjadala huu umepamba moto sana haswa katika uongozi wa waziri Bernard Membe. Hata katika hotuba ya bajeti ya wizara mwaka 2011/2012, ndugu Membe alizungumzia na kusisitizia suala hili. Kabla sijaenda mbele zaidi, naomba niulize, hivi ni sahihi kwa suala hili kujadiliwa na wizara inayoongozwa na ndugu Membe? Suala linaluhusu uraia kwanini lijadiliwe na wizara ya mambi ya nje, badala ya wizara ya mambo ya ndani?!
Naendelea na mjadala. Mimi binafsi kama raia wa Tanzania sijaweza kuelewa hoja zote zinazotolewa katika kujustify dual citizenship. Hususani juu ya suala la kuongeza kuongeza uwekezaji kutoka na wanaoitwa watanzania walio nje. Hapa pia kuna maswali ya kujiuliza. Hivi mtanzania anatambulikaje? Kwa passport? Kwa kadi ya kupigia kura? Au? Kama mtu (alie na miaka zaidi ya 18) hana vyote hivi anaweza kutambulika kama mtanzania? Je, mtu aliekua na passport ya Tanzania, halafu akaikana kwa kuchukua passport ya nchi nyingine, huyu ataendelea kutambulika kama mtanzania au?
Kama nia kuongeza uwekezaji, kwani hao watanzania walio nje wanakatazwa kuja kuwekeza? Tena hao wanakua na added advantage kwavile wanaifahamu nchi kuliko wawekezaji ambao hawana trace ya utanzania. Tena wakija kama wageni ndio watapokelewa vizuri zaidi kuliko wakija kama wazawa, kutokana na hali ya urasimu uliopo katika suala la uwekezaji wa wazawa. Katika hili, bado sijaona hoja nzito.
Pia kuna suala la rasilimali watu. Kwamba kuna watanzania walio nje ya nchi ambao wana elimu na utaalamu wa mambo mbalimbali ambao pengine ni adimu au ungeweza kuongeza nguvu kazi katika taifa letu. Sawa. Je, hawezi kuja kama expatriates? Mbona tunao wengi tu katika sekta mbalimbali, kuanzia taasisi za elimu, mashirika ya umma, idara za serikali na taasisi za serikali na binafsi. Sasa hapa hao watanzania walio nje wanashindwa nini mpaka wapewe uraia mwingine?! Tena wakija kama expatriates watapata employment benefits nzuri zaidi kuliko wazawa. Hapa pia sijaona hoja nzito ya kupelekea uwepo wa dual citizenship.
Sasa kama hizo ndio hoja za Membe, napatwa na wasiwasi kama dual citizenship ipo kwa maslahi ya umma au maslahi ya watu binafsi (nimesikia ndugu Membe ana watoto aliowazaa nje ya nchi!)
Huu ni mtazamo wangu, kukosoana kwa manufaa ya kuelimishana kunakaribishwa.
Asante.
Kunamsemo usemao, asiyejua maana ni kam usiku wa giza, ndugu yangu huwezi kuwa huru san kwenye nchi ambayo ww c mzawa kisheria wacha kuwa ulizaliwaTZ ukakana uraia, ndugu zetu wapo nje wengi kwa kutafuta maslahi lkn wangependa wawekeze home kisheria kama wazawa na siyo expertrates kama ulivyo shauri, unasema labda Waziri anamaslahi yake juu ya watoto aliozaa nje, hayo si kweli ila Dual citizenship ni kwa faida ya Taifa lako na ww kwa ujumla, nimekutana na wengi wanaoombakurudi home kama raia ili waweze shiriki katika kujenga nch lkn bado maamuzi ya wabunge wengi wanafanana na ww kuwa hakuna haja watu hao warudi kama wa TZ, nashauri kuwa Membe afanye haraka sana mwaka huu usipite tena jambo hili liruhusiwe, na baada ya miaka 3 utajua uzuri wa jambo hili, wapo matajiri wakubwa sn nje wambao wangetaka waanzishe kampuni zao kama raia wala c wageni kwa manufaa ya vijana wa TZ,
Ukitoka nje ya nchi utajua maana ya jambo hili, lkn ukitoka nje ya mkoa hutaujua umuhimu wa jambo hili,
Nawkilisha.