Uraia Pacha Tanzania: Siasa ya Bernard Membe na hatma yake

Uraia Pacha Tanzania: Siasa ya Bernard Membe na hatma yake

Salaam wanaJF!

Katika kipindi kirefu sana kumekuwa na mjadala juu ya kuruhusu uraia wa nchi mbili 'dual citizenship' katika taifa letu. Mjadala huu umepamba moto sana haswa katika uongozi wa waziri Bernard Membe. Hata katika hotuba ya bajeti ya wizara mwaka 2011/2012, ndugu Membe alizungumzia na kusisitizia suala hili. Kabla sijaenda mbele zaidi, naomba niulize, hivi ni sahihi kwa suala hili kujadiliwa na wizara inayoongozwa na ndugu Membe? Suala linaluhusu uraia kwanini lijadiliwe na wizara ya mambi ya nje, badala ya wizara ya mambo ya ndani?!

Naendelea na mjadala. Mimi binafsi kama raia wa Tanzania sijaweza kuelewa hoja zote zinazotolewa katika kujustify dual citizenship. Hususani juu ya suala la kuongeza kuongeza uwekezaji kutoka na wanaoitwa watanzania walio nje. Hapa pia kuna maswali ya kujiuliza. Hivi mtanzania anatambulikaje? Kwa passport? Kwa kadi ya kupigia kura? Au? Kama mtu (alie na miaka zaidi ya 18) hana vyote hivi anaweza kutambulika kama mtanzania? Je, mtu aliekua na passport ya Tanzania, halafu akaikana kwa kuchukua passport ya nchi nyingine, huyu ataendelea kutambulika kama mtanzania au?

Kama nia kuongeza uwekezaji, kwani hao watanzania walio nje wanakatazwa kuja kuwekeza? Tena hao wanakua na added advantage kwavile wanaifahamu nchi kuliko wawekezaji ambao hawana trace ya utanzania. Tena wakija kama wageni ndio watapokelewa vizuri zaidi kuliko wakija kama wazawa, kutokana na hali ya urasimu uliopo katika suala la uwekezaji wa wazawa. Katika hili, bado sijaona hoja nzito.

Pia kuna suala la rasilimali watu. Kwamba kuna watanzania walio nje ya nchi ambao wana elimu na utaalamu wa mambo mbalimbali ambao pengine ni adimu au ungeweza kuongeza nguvu kazi katika taifa letu. Sawa. Je, hawezi kuja kama expatriates? Mbona tunao wengi tu katika sekta mbalimbali, kuanzia taasisi za elimu, mashirika ya umma, idara za serikali na taasisi za serikali na binafsi. Sasa hapa hao watanzania walio nje wanashindwa nini mpaka wapewe uraia mwingine?! Tena wakija kama expatriates watapata employment benefits nzuri zaidi kuliko wazawa. Hapa pia sijaona hoja nzito ya kupelekea uwepo wa dual citizenship.

Sasa kama hizo ndio hoja za Membe, napatwa na wasiwasi kama dual citizenship ipo kwa maslahi ya umma au maslahi ya watu binafsi (nimesikia ndugu Membe ana watoto aliowazaa nje ya nchi!)

Huu ni mtazamo wangu, kukosoana kwa manufaa ya kuelimishana kunakaribishwa.

Asante.

Kunamsemo usemao, asiyejua maana ni kam usiku wa giza, ndugu yangu huwezi kuwa huru san kwenye nchi ambayo ww c mzawa kisheria wacha kuwa ulizaliwaTZ ukakana uraia, ndugu zetu wapo nje wengi kwa kutafuta maslahi lkn wangependa wawekeze home kisheria kama wazawa na siyo expertrates kama ulivyo shauri, unasema labda Waziri anamaslahi yake juu ya watoto aliozaa nje, hayo si kweli ila Dual citizenship ni kwa faida ya Taifa lako na ww kwa ujumla, nimekutana na wengi wanaoombakurudi home kama raia ili waweze shiriki katika kujenga nch lkn bado maamuzi ya wabunge wengi wanafanana na ww kuwa hakuna haja watu hao warudi kama wa TZ, nashauri kuwa Membe afanye haraka sana mwaka huu usipite tena jambo hili liruhusiwe, na baada ya miaka 3 utajua uzuri wa jambo hili, wapo matajiri wakubwa sn nje wambao wangetaka waanzishe kampuni zao kama raia wala c wageni kwa manufaa ya vijana wa TZ,
Ukitoka nje ya nchi utajua maana ya jambo hili, lkn ukitoka nje ya mkoa hutaujua umuhimu wa jambo hili,
Nawkilisha.
 
Haiwezekani mpaka wawe na uraia wa nchi mbili hapo ndipo wataweza kujakuwekeza kama mtanzania na wakati huo huo nchi anayoishi akaishi kama raia ili haweze kukopa pesa na kuja kuwekeza Tanzania. Vinginevyo tutaendelea kukumbatia wawekezaji wazungu ambao faida wanaipeleka kwao. Siku ya siku wanaondoka wakiwa matajiri ili hali walikuja masikini.

Mwenye uchungu wa nchi ni mwananchi

Hivi unafahamu kwamba kwa Tanzania ni rahisi kuwekeza ukiwa kama mgeni kuliko ukiwa kama mwenyeji?!
 
Mimi naunga mkono uraia wa nchi mbili lakini uwe na madaraja.

1😀araja la kwanza ni kwa raia wazawa au mmoja wa wazazi ni mzawa ( hawa ndio wawe na uwezo wa kumiliki ardhi)
2: Daraja la pili ni raia wasio wazawa ( hawa watakuwa wanaishi kama raia wengine, kupiga kura ila wasiruhusiwe kumiliki ardhi na kama anataka kumiliki ardhi basi haukane uraia wake wa asili.

Hii itasaidia sana kwa wazawa wasipoteze ardhi kama ilivyo sasa wazawa wengi hawamiliki ardhi
 
Kunamsemo usemao, asiyejua maana ni kam usiku wa giza, ndugu yangu huwezi kuwa huru sana kwenye nchi ambayo ww c mzawa kisheria wacha kuwa ulizaliwaTZ ukakana uraia, ndugu zetu wapo nje wengi kwa kutafuta maslahi lkn wangependa wawekeze home kisheria kama wazawa na siyo expertrates kama ulivyo shauri, unasema labda Waziri anamaslahi yake juu ya watoto aliozaa nje, hayo si kweli ila Dual citizenship ni kwa faida ya Taifa lako na ww kwa ujumla, nimekutana na wengi wanaoombakurudi home kama raia ili waweze shiriki katika kujenga nch lkn bado maamuzi ya wabunge wengi wanafanana na ww kuwa hakuna haja watu hao warudi kama wa TZ, nashauri kuwa Membe afanye haraka sana mwaka huu usipite tena jambo hili liruhusiwe, na baada ya miaka 3 utajua uzuri wa jambo hili, wapo matajiri wakubwa sn nje wambao wangetaka waanzishe kampuni zao kama raia wala c wageni kwa manufaa ya vijana wa TZ,
Ukitoka nje ya nchi utajua maana ya jambo hili, lkn ukitoka nje ya mkoa hutaujua umuhimu wa jambo hili,
Nawkilisha.

Chief, naona umekaa nje ya Tanzania kwa muda mrefu. Hali ni tofauti katika Tanzania ya sasa; kwani ni rahisi sana kuwekeza kama ukiwa ni mgeni - kwa maana sasa serikali inaimba wimbo wa uwekezaji katika mashamba makubwa, uchimbaji wa madini, gesi na mafuta; utafutaji wa gesi na mafuta n.k.

Hapo ndipo ninapotofautiana na enthusiasts wa uraia wa nchi mbili. Kwanini uakane uraia wako kama kweli una mapenzi ya dhati kwa taifa lako la asili?

Chief, hakuna anayewakataza kurudi hao unaowaita 'watanzania'; warudi tu kama kweli ni watanzania. Mbona wengi tu wameenda nje na kurudi kama watanzania?!?

Bado sijaona mtu akisema uzuri wa kuwa na uraia wa nchi mbili; mengi yanayosemwa bado yanaweza fanyika hata kama mtu akija kama mgeni. Pengine labda, nipe mfano wa nchi za hapa Afrika ambazo zimefaidika na uraia wa nchi mbili.

Sasa hao matajiri wakubwa sana, wanaweza pia kuanzisha kampuni zao wakiwa kama wageni na kulinufaisha taifa kwa njia ya utoaji wa ajira, ulipaji wa kodi na CSRs.
 
mh membe anataka kumficha nani hapa kwa uraia wa nchi mbili ,hutuoni mantiki ya kuwa na uraia wa nchi mbili uzalendo utakushinda na utasaliti upande mmoja
 
Mimi naunga mkono uraia wa nchi mbili lakini uwe na madaraja.

1:Daraja la kwanza ni kwa raia wazawa au mmoja wa wazazi ni mzawa ( hawa ndio wawe na uwezo wa kumiliki ardhi)
2: Daraja la pili ni raia wasio wazawa ( hawa watakuwa wanaishi kama raia wengine, kupiga kura ila wasiruhusiwe kumiliki ardhi na kama anataka kumiliki ardhi basi haukane uraia wake wa asili.

Hii itasaidia sana kwa wazawa wasipoteze ardhi kama ilivyo sasa wazawa wengi hawamiliki ardhi

Wazawa ni kina nani? Watanzania wenye asili ya uafrika? Watanzania wenye asili ya uasia? Watanzania wenye asili ya Ulaya na Marekani?

Mjadala wa uraia wa nchi mbili umekuwepo katika kutaka kuwasaidia 'watanzania' walio nje waweze kupata fursa sawa na watanzania. Sasa unaposema kwamba tuwape uraia watu ambao ni raia wa nchi nyingine, huku wakiendelea kuushikilia uraia wa nchi zao za asili, hapa unataka nini?
 
....lazima kuwekwe utaratibu maalum wa kuchuja watu hawa. Kuna vikwazo mbali mbali ambavyo nchi nyingine wanatumia ili kutowapatia uraia wale ambao hawafikii vigezo vilivyowekwa. Kwa mfano ni lazima ujue kuzungumza/kuandika lugha ya nchi hiyo, ni lazima uwe umeishi katika nchi hiyo kwa kipindi cha muda fulani na katika muda huo ulikuwa na biashara zako za halali au ulikuwa umeajiriwa kihalali na unalipa kodi. Ni lazima uwe umeenda shule angalau una 1st degree. Kunakuwa na mitihani ya kuhakikisha unajua mambo mbali ya nchi kama vile historia na Jiographia ya nchi ambayo ni lazima upate pass marks ambazo zinatofautiana kati ya nchi na nchi.

Heko kwa maelezo hayo.
Sasa kwa mtazamo wako, na kwa serikali hii, unafikiri utaratibu kama huo utawezekana? Kama sasa tu, raia kutoka nje wanaweza kuja Tanzania bila visa hadi uwanja wa ndege ambapo ndipo uweza kuomba na kupewa visa, hilo unalolisema litawezekana? Pia raia wa kigeni wanakuja tu (hata wawekezaji) Tanzania bila hata ya kufahamu neno moja la kiswahili, hilo unalolisema litawezekana?


Na kuna kingunge mmoja sikumbuki kama ni Membe aliwahi kutamka siku za nyuma kwamba kama uDC utaruhusiwa basi kwanza wataanza kupewa Watanzania waliozaliwa Tanzania ambao wana uraia wa nchi nyingine na watoto wao waliozaliwa nje huku wakiangalia taratibu gani ziwekwe/zifuatwe ili kuwaruhusu wageni toka nchi tofauti kuomba kuwa raia wa Tanzania, lakini kama tujuavyo nchini mwetu hili la wageni litatawaliwa na rushwa ya hali ya juu.

Hapo ndipo panaponipa kigugumizi cha kukubaliana na sera ya uraia wa nchi mbili. Rushwa! Ufisadi! You name it!
Hakika mpaka pale serikali (iwe ya CCM ama CHADEMA) itakapoweka utaratibu ulio fanisi, utaratibu utakaozuia aina yoyote deals ambazo zitaenda kinyume na maslahi mazima ya taifa, basi nitaendelea kupinga suala la uraia wa nchi mbili daima.
 
Nafikiri watu wanaotaka uraia wa nchi mbili ururhusiwe wana hoja na wanaopinga wana hoja vilevile lakini sasa hivi tupo kwenye mchakato wa katiba mpya Membe ana haraka ya nini kuupigia debe uraia wa nchi mbili?
Pamoja na kukubali faida zinazoweza kuletwa na kuruhusu uraia wa nchi mbili lakini inabidi tuwe wakweli kuna wanasiasa,wafanyabiashara ambao tayari wanao uraia wa nchi mbili na watu hao wameutumia zaidi kuiba rasilimali za taifa na kujinufaisha binafsi ndio maana ukiwaambia watanzania wengi juu ya swala hilo hawawezi kukuelewa kwani tumekuwa tukitunga sheria na kuingia mikataba mbalimbali bila kuangalia mapungufu yake kwa hiyo badala ya kuupigia debe tuangalie namna gani tukiuruhusu utaweza kuinufahisha nchi yetu badala ya kusema India imenufaika kwani tumewasahau wakina Chavda walivyotufanya
 
Mkuu Nzi hakuna kinachoshindikana kama Serikali iliyopo madarakani ikiamua kusimamia utawala wa sheria bila kupindisha ili kuwakingia vifua wakosaji. Angalia wakosaji wa EPA, RADA, Nyumba za Serikali, Kiwira n.k. ambao kama Serikalia ingekuwa inasimamia ipasavyo utawala wa sheria wote wangekuwa Lupango wanacheza na mvua za miaka mingi.

Wageni wanaoingia nchini kuja kuchukulia visa Airport kwangu mimi sioni tatizo lolote ikiwa tu Wafanyakazi wa uhamiaji ambao watakuwa katika Airports zetu na mipaka mingine ya nchi watalipwa mishahara na marupurupu mazuri yanayokidhi gharama za maisha na hivyo kutoshawishika kuchukua rushwa na hivyo kuruhusu watu kuingia nchini kinyemela na hivyo kuvunja sheria za nchi.

Serikali inakuwa na speed ya ajabu kila mara Wafanyakazi mbali mbali wanapoomba kuongezewa mishahara na marupurupu kutokuwa kauli yake potofu "Serikali haina uwezo" bila kuangalia athari kubwa inayosababishwa na mishahara kiduchu ambayo haikidhi hata gharama za wiki moja. Matokeo yake rushwa inashamiri kila mahali...mashuleni, mahospitalini, kwenye idara mbali mbali za Serikali ikiwemo uhamiaji, polisi n.k. na wakati huo huo Serikali ikidai inapambana na rushwa!!!! Utapambana vipi na rushwa bila kuangalia chanzo chake? ambacho ni watu kuwa na ujira mdogo na pia sheria za nchi kupindwa pale ambapo sheria hizo zinakiukwa?

Kwa maoni yangu sheria ya kuruhusu uDC haina matatizo yoyote ila kwa hii Serikali inayokurupuka katika maamuzi yake mbali mbali inaweza pia kukuurupuka kwenye hili na hivyo likajaa rushwa na ufisadi wa kutisha. Ni kweli kama sheria hazikuboreshwa mafisadi wanaweza kabisa kutumia sheria ya kuruhusu uDC kuendelea kuangamiza maslahi ya nchi lakini tukumbuke wakati huo huo ufisadi mkubwa uliofanyika nchini wa Rada, Kiwira, EPA, IPTL, Kigoda, Meremeta, Uuzwaji wa nyumba za Serikali, Ubinafsishaji wa mashirika ya umma, mikataba ya uchimaji wa madini, uuzwaji wa wanyama toka mbuga za Taifa n.k. umefanywa na wazawa ambao hawakuyajali kabisa maslahi ya nchi.




Heko kwa maelezo hayo.
Sasa kwa mtazamo wako, na kwa serikali hii, unafikiri utaratibu kama huo utawezekana? Kama sasa tu, raia kutoka nje wanaweza kuja Tanzania bila visa hadi uwanja wa ndege ambapo ndipo uweza kuomba na kupewa visa, hilo unalolisema litawezekana? Pia raia wa kigeni wanakuja tu (hata wawekezaji) Tanzania bila hata ya kufahamu neno moja la kiswahili, hilo unalolisema litawezekana?


Hapo ndipo panaponipa kigugumizi cha kukubaliana na sera ya uraia wa nchi mbili. Rushwa! Ufisadi! You name it!
Hakika mpaka pale serikali (iwe ya CCM ama CHADEMA) itakapoweka utaratibu ulio fanisi, utaratibu utakaozuia aina yoyote deals ambazo zitaenda kinyume na maslahi mazima ya taifa, basi nitaendelea kupinga suala la uraia wa nchi mbili daima.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hawezekani kuruhusu raia wa nchi yako wechukue uraia wa nchi nyingine na wakati huo huo raia wa nchi nchingine wasichukue uraia wa nchi yako. Huu ni ubaguzi
 
The right to dual citizenship in Tanzania is a must

Dual Citizenship is a status in which a person is concurently regarded as a citizen under the laws of more than one state. Dual citizens have two passports and live and travel freely within their native and naturalized contries without immigration constraints. The Tanzania citizenship is governed by the Citizenship Act, 1995. This Act proscribes the right to dual citizenship. S. 7(4) provides"Any Citizen of Tanzania shall cease to be a citizen if having attained the age of 18 years, he acquires the citizenshp of some country other than Tanzania by a voluntary act other than marriage".

The Tanzanian Constitution, 1977 unlike Constitutions of other countries eg Kenya and Uganda, is silent on the right to dual citizenship. Generally, citizenship in our Constitution is merely mentioned en passant.

A significant number of Tanzanians are now living abroad and are scattered all over the world. They are now commonly known as THE DIASPORA COMMUNITY. Mean estimate is putting the number of Tanzanians in Diaspora at 2Million. This group, thus, account for 5% of our total population. This is an important constituency which has to be represented in the new constitution, in my humble view.

There are many factors obtaining in Tanzania which have contributed to the exodus of skilled talent. They include poor conditions of service, potential human rights abuses, nepotism and favoratism, disregard for local talent, scarcirty of jobs, poor salaries, limited access to education, the 2001 Zanzibar chaos etc.

African natives who are resident in industrialized nations have been prodding their home countries to provide for dual citizenship to make it possible to make them citizens of a second country. A lot of Tanzanians who are currently in the Diaspora have been agitating for the same. At the beginning, the issue of citizenship was resented but now it was beginning to be understood.

Tanzania has been benefitting from people living abroad through remittances. Apart from tha,t Tanzanians living abroad have different professions and are experienced in several sectors of the economy, hence they would make immense contribution if they came back to work here. Some of them command respect the world over hence if properly utilized they could greatly contribute to their mother country development.

The role of the Tanzanian Diaspora community has been, inter aia, to provide socio-economic support for some Tanzanians back home. Due to the extended family system, most of Tanzanians living abroad find themselves being regarded as crucial breadwinners of not only their immediate families but also their close family relatives.

They normally pay for most of the financial needs of their dependants back at home such as medical and education fees, accomodations rentals and social events such as religious gatherings, funerals, birthday and wedding parties.

In 2006, the Law Reform Commission of TZ under the Chairmanship of Judge A. Bahati recommended introduction of Dual Citizenship. The Commission stated that the issue deserved " a possitive and foward- looking consideration and that it was high time Tanzania adopted dual citizenship because in a globalized world, the country could not develop without interraction with other nations".

More importantly, many developing nations scuch as Ghana have made significant economic strides after allowing dual citizenship a few years ago.Furthermore, Hon. B. Member, Minister for Foreign Affairs, a distingushed Diplomat stated the following in the National Assembly when responding to a question from one Vicky Kamata (CCM)

"African countries have been benefitting from people living abroad through remittances. For the past year, a total of USD 40 Billion entered Africa through remittances out of which Tanzania received USD 250M.

We are creating a good environment that will enable Tanzanians living abroad work in the country. We recognize them and respect their contribution to the country economic development. In the newly launched 5 year develoment plan (2011-2015) the issue of Diaspora has been highlighted and given priority.

This dual citizenship issue will also be included in the Constitutional debate..."

Thus, in my view, Dual citizenship MUST be enshrined in our new Constitution.
Great Thinkers, hii imekaaje?
 
Anayo,kwani hujui kuwa huyu jamaa pia ni raia wa Afganistani?
Hapana! nu uraia wa Vatican (Makao makuu ya Ukatoliki) tu ndio ambao unaruhusiwa kuwa nao pamoja na waKitanzania!

Ni matabaka yaliyoasisiwa katika awamu ya kwanza.
 
When it comes down to "allegiance", to whom will the person with multiple uraia be pledged? Dual citizenship will confer facilities and privileges without obligations. Apart from marginal economic and social benefits, it can create ambiguous loyalties among people holding it.

What status will you confer to aid donors that give a lot of handouts to our government if you view the magnitude of aid they give?

How could someone be a citizen of two countries at the same time? I bet it could be undermining the notion of nationhood especially to a nascent country like TZ.

Assume the US is engaging into war with your second country(probably your mother country) and you are living in the US, what will you do in this situation or you will make it the Arab style, suicide bomber, which in turn will result to negative repercussions with your community living the US.

Giving reasons of remittances back home as justification to conferring dual citizenship is too vague a definition of granting the status to make any credible conclusion about its establishment.

If allowed, the decision will be based on narrow short term motivations and should be opposed.
 
When it came down to "allegiance", to whom will the person with multiple uraia be pledged? Dual citizenship will confer facilities and privileges without obligations. Apart from marginal economic and social benefits, it can create ambiguous loyalties among people holding it.
What status will you confer to aid donors that give a lot of handouts to our government if you view the magnitude of aid they give?
How could someone be a citizen of two countries at the same time? I bet it could be undermining the notion of nationhood especially to a nascent country like TZ.
Assume the US is engaging into war with your second country(probably your mother country) and you are living in the US, what will you do in this situation or you will make it the Arab style, suicide bomber, which in turn will result to negative repercussions with your community living the US.

Giving reasons of remittances back home as justification to conferring dual citizenship is too vague a definition of granting the status to make any credible conclusion about its establishment.

If allowed, the decision will be based on narrow short term motivations and should be opposed.

The poor mind sets, always ready to embrace the negatives...
 
Back
Top Bottom