inabidi tujiulize kwa nini uu mswada unashikiwa bango? nadhan serikali ina priority ktk kuletea wananchi wake maendeleo, je, muswada wa dual citizenship utaleta faida gani hadi upewe kipaumbele hadi membe akipita kila kona kuuhubiri kama jesus enzi zake!
je hao wageni(waliokua watanzania wakaukana utanzania ili wawe raia wa nchi zingine) sisi tunawajali kwa lipi maana walitukimbia ili wakaenjoy raha za majuu sasa leo wamesahau nini? kama ni kuja kuwekeza si kweli mpaka uwe na urai wa tanzania ili uwekeze, makaburu wa kule tanzanite one(mererani), barrick kule kanda ya ziwa, tbl, nmb etc ni watanzania?
watanzania siri ya dual citizenship ni kwamba wawekezaji wanataka waenjoy benefit za utanzania kununua ardhi, kuchimba madini na kutolipa kodi na mwisho wa siku maliasili zikiisha na umasikini ukiongezeka violences are inevitable kwa iyo ndio waweze kurudi makwao kwenye nchi zao za kweli, na ndio haohao atakua anaweka pesa zake nchi za ulaya, imagine tajiri awe na uraia wa uk na tz, pesa atakua anaweka ktk benki za nchi ipi? matunda yote atayopata kutoka tz ataenda kuyaenjoy wapi? tusidanganyike uu mswada unapigiwa debe na wb,imf na donors na utapita tu kwani serikali ishalazimishwa no turning back!
au serikali itueleze ni wageni wangapi waluiokua watanzania leo wanataka kuwa watanzania tena, na kwa sababu zipi?