It's about time.
Lakini jamani kwanini suala hili linachukuliwa kama jambo dogo?kwanini tusiitishe mjadala wa kitaifa?KIKWETE TAFADHALI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
You're 100% right Mkuu, It is about time. Thank you Membe for your efforts and dedication about this issue.
Mkuu,
Kwa jinsi nilivyoelewa ni kuwa kutakuwa na muswada wa mabadiliko ya sheria bungeni kabla mwisho wa mwaka huu sio..au sijaelewa?
I don't understand exactly why some people were going off the deep about this issue. I don't see anything wrong with it so long as the laws clearly state the stipulations to be followed.
I don't think the people who opposed it were genuine. I somehow feel their opposition was fueled by envy. But I'm glad now the govt. finally has decided to come around on the issue and hopefully sign it into law.
I use the phone nokia6300 sorry 4that
Kuchanganua na kuweka vizuri misingi ya waTanzania wanaoishi, kununua na kutumia uraia wa nchi hizo na wakati huo huo kuendelea ku-retain uTanzania wao ni mradi/mpango fulani ambao tatizo lake ni.
1. Faida itayopatika ni moja tu: ambayo ni "greater good only kwa nchi nzima na maendeleo yake". Faida binafsi "personal gain" kwa MAFISADI ni finyu mno kiasi cha wao kutokuwa tempted kuichukua na kuifanikisha project hiyo.
2. Pindi ingekuwa hao wanaoitwa wahisani wana direct interest ya sisi kuendelea na uTanzania baada ya kuwa wameshakuuzia uraia wa nchi zao na kutuwekea masharti yao, basi wangeudhamini utekelezaji wa "project" hiyo. Hapo tena ungewaona MAFISADI wetu (MAWARIRI, MANAIBU WAZIRI, MAKATIBU WAKUU, WAKURUGENZI WA IDARA, nk, nk) wanagombaniana haki za kuendesha mradi huo. Kila wizara ingedai haki ya kuundesha mradi huo, Mambo ya ndani, Mambo ya nje, Utalii na masoko, nk, nk. As long as kama hao wahisani wangetoa bilioni tano (5 bil) kwa ajili ya mradi na wao wanajua kwamba gharama zake hazizidi bil2.2 mpaka bil 2.5, Kila mmoja angekuwa tayari kukosa usingizi katika kufanya safari na mikutano mfululizo, kusema uongo kweupeeee ilimradi tu at the end, 2.5bil-2.8bil watatia ndani katika account zao.
Kwa kifupi, ni mentality za KIFISADI walizonazo VIONGOZI wetu ndizo zinazozuia kutekeleza mradi huu. Utakuja tuuuu kufanywa pasipo na budi kufanywa, tena utatekelezwa kiuvivu na kwa gharama kubwa za kupindukia. Yaani watasema "POTELEA MBALI TUTAIBA TU HATA KAMA WANATUONA" na zitaibiwa pesa hivihivi kwa ukuritimba na corruption. Hili ndio tatizo kichwa/tatizo mama la nchi yetu TZ.
Ole wenu MAFISADI, kufeni kabisa kabla sisi hatujakamta nafasi mnazohodhi, mta face retrospective justice, judiciuosly na gharama mtalipia, mpende msipende. Hamna nyiyi haki ya kuishi kabisa ulimwenguni, seuze Tanzania. May Satan be your miserable mates in the Hell-fire.
faida hizo haters
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, amesema serikali itahakikisha sheria ya uraia wa nchi mbili inapitishwa kwa manufaa ya Watanzania na taifa na si vinginevyo.
Akizungumza na baadhi ya Watanzania waliokutana naye mjini New York wiki iliyopita katika hoteli ya Grand Hyatt, Waziri Membe alisema lengo la serikali ni kuwasaidia Watanzania na si kugawa uraia wa Tanzania kwa wageni wenye uraia wa nchi zao.
Alisema haingii akilini ni kwa nini Mtanzania wa kuzaliwa anyang'anywe uraia wa Tanzania kwa kuwa amechukua uraia wa nchi nyingine kutafuta faida za kielimu, ajira au hata matibabu.
Ni kwa nini tumuadhibu huyu Mtanzania wa kuzaliwa kwa kuwa tu amechukua uraia wa nchi nyingine ili apate elimu ama ajira na kusaidia ndugu zake waliobaki Tanzania? alihoji Waziri Membe.
Waziri alisisitiza kuwa sheria hiyo itakapopitishwa haitatoa mwanya kwa kila mtu kuuvamia uraia wa Tanzania bali itawalinda Watanzania wanaotaka kuchukua uraia wa nchi za nje kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.
Akitoa mfano mmojawapo bila kutaja majina ya wahusika, Waziri Membe alisema anaifahamu familia moja ya Watanzania ambayo ililazimika kuchukua uraia wa Kanada kwa sababu za matibabu, na kwamba kuwanyang'anya uraia watu hawa ni kuwaadhibu bila kujali uhai wao.
Alieleza kuwa familia hiyo ina watoto wawili ambao matibabu yao hugharimu dola 2,000 kwa kila mmoja kwa mwezi, na kwamba kwa kuchukua uraia wa Kanada, matibabu hayo yanakuwa bure. Alihoji je, ni haki kuwanyang'anya uraia wao wa Tanzania?
Akitoa mfano wa manufaa yanayopatikana Ghana, Waziri Membe aliwaambia Watanzania hao kwamba ni muhimu kwa Tanzania kutumia raia wake walioko nje kwa manufaa ya taifa na siyo kuwabagua.
Mwaka jana pekee wananchi wa Ghana walioko nje waliingiza dola bilioni 2.5 kwa njia mbalimbali halali, na akaongeza: Taifa dogo kama Komoro, mwaka jana lilipata dola milioni 89 kutoka kwa wananchi wake walioko Ufaransa pekee.
Akifafanua zaidi, Waziri Membe alisema wakati akiwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kipindi kisichofikia miaka miwili, Tanzania ilitoa uraia kwa wageni 101 na kushangaa ni kwa nini Watanzania wa kuzaliwa wapoteze uraia wao.
Waziri Membe aliwataka Watanzania kujenga umoja thabiti na kuwahakikishia kwamba serikali itakuwa pamoja nao ili kuleta maendeleo kwa taifa, na kwamba mawazo kuwa usalama wa taifa utakuwa hatarini si la jambo kuhofia iwapo sheria itatungwa vizuri.
Tanzania ina raia wake waliosambaa nchi mbalimbali duniani huku idadi kubwa ikiwa katika nchi za Kiarabu za Ghuba ambako wakati serikali ikiongeza ofisi moja ya Ubalozi nchini Oman miaka michache iliyopita ilikadiria kuwa kuna Watanzania laki tano.
Nchi nyingine ambazo Watanzania wanakadiriwa kuwa wengi ni za Marekani Kaskazini na Ulaya Magharibi ambako wako kwa maelfu, ambao wengi wao hukabiliwa pia na utata wa uraia wa watoto wao wanaozaliwa ugenini.
Mjadala wa suala la uraia wa nchi mbili umekuwa ukiendelea nchini katika siku za karibuni ambako kumeibuka kambi za wanaopinga kwa madai ya kulinda maslahi ya nchi na wanaounga mkono kwa madai hayo hayo ya kulinda maslahi ya nchi.