Mkuu Mchambuzi, hii ni thread ya ZZK, tukianza kujibu ya EL na Membe, hapa patakuwa hapatoshi!. Ziko thread 100 humu nimemzungumzia EL na kama 20 nimemzungumzia Membe, sifa kuu zao wote hao wawili watu wenye uwezo mkubwa sana kutupatia ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!. Hili naomba usilihoji zaidi!.Hawa ni aina mbili tofauti kabisa ya viongozi in character, experience and positions on issues; kutokana na hili, ni dhahiri kwamba iwapo wote watafikia hatua ya kuingia kwenye top five katika uchaguzi wa ndani CCM iwapo watagombea na hivyo kupata wasaa wa kujieleza mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa, tofauti hizi zitaonekana bayana kabisa kwani kwa mfano, kila mmoja atakuwa na msimamo tofauti kabisa juu ya wapi anadhamiria kuipeleka nchi yetu kimaendeleo, nini viwe vipambele vya sasa, muda wa kati na muda mrefu in terms of domestic issues and foreign policy kisiasa, kijamii na kiuchumi; kutokana na hili, ndugu Pasco, ningependa kujua, je:
1. Ni vigezo gani unavyotumia kujenga hoja kwamba best candidate ni Lowassa and Membe as the second best candidate?
2. Na kwa vile inaonyesha kwamba unaona Zitto pia can make a good presidential candidate, ni kigezo gani unatumia kujenga hoja yako, hasa ikizingatiwa kwamba Zitto, Membe na Lowassa ni aina tatu tofauti kabisa ya viongozi based on hoja yangu ya msingi hapo juu?
Kwa kuwa masikio unayo Zito, basi yasikie maneno hayo na uyazingatie.ni kweli kabisa,sio kosa mtu kutaka kuwa kiongozi wa nchi hii.lakini pia naona kama mh. zitto anapaswa akae chini atulie and ajifanyie tathimini mwentewe.binafsi zito ni mwakilishi mzuri wa wananchi andamekuwa akifanya vizuri kazi zake.chaajabu,ni njinsi jammii anayoiongoza ilivyokuwa na mtazamo hasi(-) kwake.mie namshauri zitto atulie maana jinsi siku zinavyoendelea,amekuwa akihusishwa na tuhuma kibao ambazo sio nzuri,ajiulize ni wapi anakosea maana asipotulia magamba watamtumia and mwisho wa kuwa tegemeo kwa wananchi utafika.zitto skando zimekuwa nyingi sana bana,utadhani msanii kumbe kiongozi na mwakilishi wa wananchi.
zito wa zamani anapotea anaelekea kuwa zito mambo leo.tafadhali mh.turejeshee yule zito mwenye uchungu na nchi hii anayefanya kazi yenye maslahi kwa wote.hivyo vya urais mie sitaki kuviongelea maana maamuzi yapo kwa wanachama wenzio.
Mkuu Nguruvi3, asante, nimekupata vilivyo!. Pia nimewafitisha wale wote ninaowapigia debeMkuu Pasco,
Kama umenisoma vema nimesimama katika hoja ya kuwa kutangaza nia ya urais si kosa. Ni haki kabisa na kwa namna yoyote ile inabaki kuwa haki ya mtu. Lakini usisahau kuwa kila kitu kina mipaka na taratibu. Sijui taratibu za CDM ila kwa mkakati wa kisiasa kuna mambo mtu anaweza kufanya na kubomoa hata kama amedhamiria kujenga.
Ninasimamia ukweli na wala sifungamani na ushabiki unazi au upenzi. Kwa hili sakata la Kigoma nimeweka wazikuwa video ipatikane ili tuitathmini na kufikia conclusion kadri ya kila mmoja wetu.
Maana yangu ni kuwa Zitto asihukumiwe kwa kauli za wengine. Tunachotaka hapa ni kuondoa unafiki na mimi nasema ikidhihirika vinginevyo tutawaambia wahusika wote bila haya wala soni.
Historia inaonyesha kuwa Zitto hajawahi kukemea ukabila, udini na umri. Anavyozidi kukaa kimya huku akifungamanishwa na makudi ya kina Kafulila inatupa picha na habari nyingine zaidi ya tuzijuazo.
Kwa vile msimamo wangu ni demokrasia ya kweli, natumaini watu wote wa vyama vyote watapewa fursa sawa katika kuwania nafasi za uongozi. Lakini sitakaa kimya hata siku moja kwa kiongozi anayetaka uongozi kwasababu ya kabila, dini, umri au jinsia. Huyu nitamkana hadharani bila aibu wala kificho.
Sikubaliani na dhana ya ujana au kubadalishana uongozi kwa misingi ya dini. Hatuchagui masheikh wala maaskofu.
Ninashangaa kuona India nchi iliyokuwa inamilikiwa na Hindu kwa miaka dhahari imevuka mipaka na kuweka kiongozi wa Ki-Singh, Mamohan Singh. Angalia jinsi nchi inavyopaa.
China hawana viongozi wa kiislam wala kikristo, angalia nchi inavyopaa.
Hata huko Marekani kuna viongozi katika bunge wadini zisizokuwa rasmi. Sisi tumeng'angania udini.
Ndipo ninaungana na Mkuu Mkandara kuwa zamu za uongozi ni upofu uliotopea na hatua inayofuata ni ujinga. Nitty gritty!
Kuhusu endapo watu wanajua kilicho moyoni mwa Dr Slaa, hakika hakuna ajuaye kama tulivyokuwa hatujui ya Mwinyi, Mkapa au JK. Nadhani muhimu ni kuangalia kiongozi anasimamia nini na anatetea sera gani kwa hoja na si kwa dhana.
Hakika hakuna ambaye tunaweza kujua dhamira yake.
Na mwisho nikumbushe kuwa katika uongozi kuna mambo mengi sana yakuzingatia.
Baadhi ya vitu vinavyomtengeneza kiongozi ni kama Charisma(haiba), popularity(umaarufu), intellectual (weledi) n.k.
Ukicheza karata vema kwa vitu hivyo unaweza kufanikiwa katika siasa.
Muhimu sana ni 'intellectual' ambayo si degree tu, bali kiongozi anavyoweza kuji-present, present his or her ideas, communication, emotion nk.
Lakini pia katika siasa kuna kitu wanasema ni 'political strategy' mkakati wa kisiasa na huu hufungamana sana na timing
Unaweza kuwa na vitu vyote lakini ukashindwa kufikia matamanio kwakukosa kitu kidogo tu, political strategy.
Sijui kama nimeeleweka!
Wanabodi,
Mara baada ya mazishi ya Mhe. Regia, (RIP), on route back to Dar, nilibahatika kukutana mahali na Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wibroad Slaa akiwa na wife wake, Fina, tuliendesha mazungumzo mafupi, informal, na miongoni mwa maswali niyomuuliza, ni hili la iwapo atagombea tena nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi wa 2015!.
Nayakumbuka vizuri sana majibu ya Dr. Slaa kuhusu swali hilo!. Kwa vile mazungumzo yale hayakuwa rasmi, kuna uwezekano mkubwa, Dr. Slaa alizungumza "off the record", sio busara kuyaleta mazungumzo ya "off the record" kwenye public na kuyaweka "on the record" bila "idhini" ya msemaji.
Kwa vile msimamo wa "Dr. Slaa kuhusu kugombea urais 2015, mimi naujua!, nawashauri, wale wote wanaumlaumu au kumshutumu Zitto, kuonyesha nia ya kuwania urais wa 2015 kwa tiketi ya Chadema, kwa kujenga mazingira "impliedly" not "expressly"!, wasimlaumu bali wamsupport!.
Hivi kuna ubaya gani, kuonyesha nia ya kuwania the highest office?. Wote wanaoutaka urais, huitwa "presidential hopeful", hivi kuna ubaya wowote to aim high?!...
Kwa kuwa masikio unayo Zito, basi yasikie maneno hayo na uyazingatie.
Ben,
Kwa vile umeshawahi kugombea nafasi za kisiasa unafahamu kuwa mikakati ya kuwania nafasi hiyo ni lazima ianza mara unapoamua kwa dhati kuiwania nafasi hiyo.
Odinga kuwa hajatangaza hadharani haimaanishi kuwa hakuwa anafanya mikakati ya chinichini. Raila akiwa Afrika Kusini aliulizwa kama atagombea Urais akasema hatagombea, kumbe alidanganya!
Unaposhauri Zitto afanye mikakati ya chinichini kwa siri unaamanisha kuwa Zitto asiwe mkweli kwa watanzania. Na pia unapendekeza watanzania wafichwe juu ya habari muhimu kama mtu anayetaka kugombea Urais, just kwa manufaa ya CHADEMA. Kwako wewe CHADEMA ni muhimu kuliko watanzania.
Watanzania wakijua mapema watapata muda wa kutosha kuchuja Zitto. Wanasiasa jengeni tabia ya kupenda wananchi kuwa na taarifa sahihi kwa muda wa kutosha ili wafanya maamuzi sahihi yanayoongozwa na taarifa walizopata.
Mwisho kabisa: Ben ukiwa kama insider wa CHADEMA unadhihirisha kuwa huko CHADEMA hamfanyi mambo kwa maslahi ya taifa ila ni kwa maslahi binafsi. Hii imedhihirishwa na kauli yako kuwa mtu kutangaza kutaka kugombea Urais kunavunja umoja wenu. Ina maana huko kuna watu wapo just because wanajua fulani hatakuwa Rais lakini sio kwa kuiamini ideology ya Chama. Sasa anzeni kujenga chama kinachounganishwa na ideology. Acheni tabia ya kuunganishwa na matumaini ya kuwa karibu na mtu atakayeingia Ikulu.
Mkuu Ben, ni kweli kwa CCM chaguo la mgombea wa kusimamishwa ni EL mpaka kesho, kana ni kweli afya yake ni mgogoro, then I support Membe!.
Kwa mtu asiye na chama kama mimi, I just wish to get the best for this nation. EL ndie the one and only best of the best wa CCM!. Zitto is of of the best Chadema has!. Najua wengi wenu mna mtu wenu!, if you cant get what you want, just take what you get!.
Kama unataka kutoka point A kwenda point B, na ulipanga lazima uruke kwa helcopter, isipokuja, na usafiri uliopatikana ni gari, wewe panda gari safari eiendelee!. Na taka gari ikikosekana, ikapatikana bajaj, wee panda, hata boda boda wee panda, hata baiskeli, panda tuu au vikikosekana vyote, tembea hata kwa miguu!, ili mradi ufike safari yako!.
Huyo mgombea wako ndio ile choper au gari, Zitto ni kibajaj, mimi ninazo taarifa za choper, nawashauri mpande hicho hicho kibajaj ili mfike 2015!.
Mkuu Ben Saanane, kwanza lazima nikiri wazi kuwa wewe uu miongoni mwa hazina kubwa ndani ya Chadema kutokana na genuinity na objectivity ya majibu yako kwenye hoja hii.
Niliwahi kusema humui kuwa chadema-haijajipanga nilishambuliwa sana. Wapenzi wa Chadema hawakusoma hoja zangu wakaishia kumjadili mtoa hoja!......
Zitto hawezi kuwa ticket ya Waislaam kukipigia kura Chadema, maana chuki yao ni Chadema na sii Zitto. mapenzi yao ni CCM na sii JK maana miaka yote waislaam wamekuwa wapiga kura wazuri sana wa CCM toka enzi za Mwalimu.. Nitasema wazi haijawahi kuttoke mkutano wala sherehe Dar zilzizomwondoa record ya Nyerere ktk mikutano yake yote iwe Karume, uwanja wa Taifa au redioni. Hakuna rais aliyewahi kusikilizwa kwa maanani, kwa mahudhurio makubwa kama Nyerere iwe Dar, Tanga, Kigoma, Songea au Mtwara ama kokote kule nchini..
Wanabodi,
Mara baada ya mazishi ya Mhe. Regia, (RIP), on route back to Dar, nilibahatika kukutana mahali na Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. Wibroad Slaa akiwa na wife wake, Fina, tuliendesha mazungumzo mafupi, informal, na miongoni mwa maswali niyomuuliza, ni hili la iwapo atagombea tena nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema katika uchaguzi wa 2015!...
Ben,
Kwa vile umeshawahi kugombea nafasi za kisiasa unafahamu kuwa mikakati ya kuwania nafasi hiyo ni lazima ianza mara unapoamua kwa dhati kuiwania nafasi hiyo.
Odinga kuwa hajatangaza hadharani haimaanishi kuwa hakuwa anafanya mikakati ya chinichini. Raila akiwa Afrika Kusini aliulizwa kama atagombea Urais akasema hatagombea, kumbe alidanganya!
Unaposhauri Zitto afanye mikakati ya chinichini kwa siri unaamanisha kuwa Zitto asiwe mkweli kwa watanzania. Na pia unapendekeza watanzania wafichwe juu ya habari muhimu kama mtu anayetaka kugombea Urais, just kwa manufaa ya CHADEMA. Kwako wewe CHADEMA ni muhimu kuliko watanzania.
Watanzania wakijua mapema watapata muda wa kutosha kuchuja Zitto. Wanasiasa jengeni tabia ya kupenda wananchi kuwa na taarifa sahihi kwa muda wa kutosha ili wafanya maamuzi sahihi yanayoongozwa na taarifa walizopata.
Mwisho kabisa: Ben ukiwa kama insider wa CHADEMA unadhihirisha kuwa huko CHADEMA hamfanyi mambo kwa maslahi ya taifa ila ni kwa maslahi binafsi. Hii imedhihirishwa na kauli yako kuwa mtu kutangaza kutaka kugombea Urais kunavunja umoja wenu. Ina maana huko kuna watu wapo just because wanajua fulani hatakuwa Rais lakini sio kwa kuiamini ideology ya Chama. Sasa anzeni kujenga chama kinachounganishwa na ideology. Acheni tabia ya kuunganishwa na matumaini ya kuwa karibu na mtu atakayeingia Ikulu.
Mimi nitaongezea tu kusema ya kwamba hivi kweli watu bado hawajakusoma vizuri wewe Pasco au kweli MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO...Mkuu Nguruvi3, asante, nimekupata vilivyo!. Pia nimewafitisha wale wote ninaowapigia debe
1. EL
2. Membe
3. ZZK,
Nikakuta wote, wanavyo!. Wote wana Charisma(haiba) japo inazidiana, wote ni popularity(umaarufu), na wote ni ma intellectual (weledi) na wote kwa sasa, wanazichanga karata zao vizuri kusubiri kuzicheza vema muda muafaka utakapowadia!.
Pia nakiri, 'intellectual' za hawa watu wangu nazo zina differ, sio tuu katika kuji-present, present their ideas, communication, emotion, kwani mmoja intelect yake iko mdomoni, mwingine iko kwenye strategies na mwingine iko kichwani! ila wote wana good 'political strategy' mkakati wa kisiasa japo kuna baadhi wana tatizo kidogo katika timing!. Strategy ya mmoja ina vission na mission anataka kulipeleka wapi taifa hili!. Kuna mmoja anajiona anastahili kwa sababu watu wa hovyo kabisa wameweza na kumpandia kichwani!, na kuna mmoja anataka kuwa rais ili tuu na yeye awe rais!, kutembea na yale mapiki piki na kupigiwa saluti!. All and all ali muradi, tutafika!.
Mkuu FJM, Zitto alipogombea uenyekiti Chadema, yalimkuta haya haya kwa vile kuna wana Chadema wanaabudu watu!, kwao maadam Mbowe ni Mwenyekiti, yoyote atakaye mchallenge huonekana adai na kitendo hicho kinaonekana kama ni usaliti!.
Baada ya uchuguzi wa 2010, tuliaminishwa kuna watu ndio walioshinda kihalali, matokeo yakachakachuliwa, akatangazwa aliyeshindwa!. Kuapishwa kukasusuri na hotuba ya uzinduzi bunge pia ikasusiwa na kauli kali "hatumtambui"!.
Hivi ni viashiria tosho kuwa kwa Chadema, tayari inae mgombea urais wa 2015, hivyo any move from anybody wa Chadema na urais wa 2015, unaonekana ni usaliti!.
Nikawauliza, hivi mnaujua msimamo wa huyo mtarajiwa?!. Kwa vile niliongea nae off the record, naujua msimamo wake!, nawashauri Zitto asimbezwe!.
Amini nawaambieni, harakati hizi zingefanywa na Dr, hakuna yoyote ambaye angetia neno!.
Kwani kuna kuna uhusiano gani kati ya ugombeaji wa Slaa na wa Zitto au mwanachama mwingine? Kwamba kuna watu wanataka Slaa kwanza akatae ndio wengine waruhusiwe? Kwani CHADEMA wanapeana nafasi, au ni mchakato wa mchujo? Naona hapo umeandika kama Ponda wa sensa!