Ndugu zangu, huyu anayezungumzwa na kuandikwa kila chochoro, Hana jipya, wala hatakuwa na jipya.
Kukaa na kupoteza rasimali muda, huku ukimpigia "Promo za Kipuuzi" mtu ambaye hatakusaidia kwa lolote, huo nao ni upuuzi.
Ndugu zangu, huu ni Msimu wa "Maembe" Fanyeni biashara ya "Maembe"
Huyo "Membe" hatatusaidia chochote.
Sana sana atatuletea "Mende"
Asanteni, Ngoja nimpikie mume wangu kipenzi chakula cha lala salama.
Hakuna mtu anayesaidiwa na mtu chochote mana hakuna anayetoa pesa zake mfukoni kuendesha nchi.
Tunamtaka mtu atakayeondoa chuki kwa watanzania. Ubaguzi, upendeleo, ukanda, ukabila ,udini, siasa muda wote majukwaani tena siasa za chuki na kukashifiana huku kundi moja likinyimwa haki ya kujibu. Hatutaki kuishi kama watumwa kwenye nchi yetu tuliopewa na Mungu.
Hatutaki watu wanaoua imani zetu za kumwamini Mungu mmoja aliyeumba vitu vyote kwa kujigeuza wao ndio miungu ma wenye mamlaka juu ya kila kitu mpaka roho za watu ziko mikononi mwao na riziki wanagawa wao.
Tunataka kiongozi anayejijua kuwa yeye sio Mungu ni binadam na anakosea na hatakuja malaika kumkosoa Bali ni binadam wenzake hata kama hawapendi.
Tunataka mtu atakayejenga umoja wa watanzania bila kubaguana na kuweka watu was kutisha wenzao kama anavyofanya Msiba mkuu.
Tunataka mtu atakayeweka maendeleo kwa uwiano na sio maendeleo ya upande mmoja tu.
Tunataka mtu atakayeheshimu mihimili mingine na kuiacha itimize majukumu yake kwa haki. Bunge liwe live tuone wanapojadili mambo muhimu kwa ajili yaaisha yetu. Matokeo ya kuficha bunge ni hayo ya Sheria ya mafao kupitia bungeni bila kuonekana ilipitaje.
Na sheria ya vyama vya siasa nayo inataka kupita bila kujulikana itapitaje.
Tunataka mtu atakayeifanya nchi kuwa mahali salama kwa watu wote sio kwa watawala tuu.
Tunataka mtu atakayewafanya watumishi wote wa umma na watawala kuheshimu sheria na kuwa watiifu kwa wananchi wanaowapigia kura na wanaowalipa kodi ili walipwe mamilioni ya mishahara.
Tunataka kiongozi atakayejenga demokrasia na maadili ya uongozi kwa viongozi kupatikana kupitia sanduku la kura sio hila na kutisha na kuumiza watanzania wenzetu kwa sababu ya madaraka.
Tunataka kiongozi atakayeleta tume huru ya uchaguzi ili viongozi wapatikane kihalali na kwa haki. Nchi ikiwa na haki inakua na amani na furaja ndani ya mioyo ya watu.
Tunataka kiongozi atakayejenga mifumo na taasisi zenye kuwaheshimu watu na kujali uhai wa watu na Mali zao bila kuangalia tajiri,maskini, mkulima ,mfanyakazi ,mwanasiasa , mfanyabiashara n.k.
Tunataka mtu atakayejenga mifumo ya haki kuanzia kwenye chaguzi bila kutishwa au kufanya hila na kupata viongozi wa hila hila.
Tunataka mtu atakayeweza kusimamia rasilimali za nchi kama madini ,samaki, wanyama, misitu,gesi, utalii n.k kwa ajili ya kukuza uchumi sio kuficha hizo rasilimali kwa uchoyo na ubahili kama Mali binafsi ili wote tukose matokeo yake maskini wanaumizwa kwa kodi kila kukicha na rasilimali za nchi hazitumiki kwa ubunifu zaidi ya kiki za kisiasa.
Tunataka kiongozi hatutaki mtu wa kutusaidia kwa kupita na kutugawia hela mitaani kama ombaomba ili atufanye watumwa na kutegemea hisani kwa kodi zetu wenyewe.
Mwenyezi Mungu tunakuomba utupe akili za kumtambua kiongozi bora ifikapo 2020.