Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Watumishi fanyeni hujuma indirect dhidi ya serikali hii onevu kwenu ni miaka 3 hakuna ongezeko la mishahara na maslahi yenu yanazidi kukandamizwa.
 
Watumishi fanyeni hujuma indirect dhidi ya serikali hii onevu kwenu ni miaka 3 hakuna ongezeko la mishahara na maslahi yenu yanazidi kukandamizwa.
 
Mimi sidhani kama watanzania tuna shida ya raisi, Tanzania tulihitaji mtu wakusimamia Rasilimali zetu, mtu wakutujengea miundombinu ya kisasa, mtu wakutufufulia shirika letu la ndege, mtu wakurudisha heshima kazini, mtu wakutetea wakulima dhidi ya wanyonyaji, mtu wakuturudishia heshima ya nchi yetu kimataifa, mtu anayezungumza ukweli ma kutenda anachokiamini kwa wakati, mtu anayetaka maendeleo kwa haraka na sio porojo, mtu anayerudisha heshima na utu ulioanza kupotea miongoni mwa watanzania, mtu anayetaka watu wale vya halali na sio vya haramu, mtu anayehakikisha wanafunzi wanapewa mkopo kwa wakati bila mgomo, mtu anayetekeleza sera ya viwanda kwa votendo kwa kujenga Nyerere george 2100MW, mtu anayechukizwa na kupambana na rushwa kwa vitendo, mtu anayetenda mambo makubwa kwa mda mfupi. Namshukuru Mungu katika uhai wangu nimebahatika kushuhudia raisi na mwanasia anayetekeleza kile alichokihaidi tena kwa wakati, maana huko nyuma nilijua ili uwe mwanasiasa ni lazima uwe muongo na nikaamini kuwa siasa ni mchezo mchafu, kwa hiyo wale tulioshika amri ya tano ya Mungu tuliogopa kuwa wanasiasa ila kupitia raisi JPM ile dhana ya siasa ni uongo na mchezo mchafu nimeifuta. Mungu akulinde raisi wetu.
 
Ni kweli hajawagusa wanasiasa wenzie wanao husishwa na ufisadi au ubadhirifu wa mali za umma. Lakini naona juhudi za kuzuia wasitokee wanasiasa wengine wengi watakao fanya ufisadi uliokufuru bila woga kama awamu zilizopita.

Angalau yeye ana anzia hapa ingawa siso tunapenda angelianzia na wa awamu zile kuwawajibisha kisheria.
Hahahaa! Is that what you believe?! How old were you during Mkapa Administration?!

Anyway, wakati wa Mkapa ingawaje bado nilikuwa shule lakini nilikuwa mfuatiliaji mkubwa sana wa siasa! Ukitoa tuhuma za kupika za akina Mrema kwa Profesa Mbilinyi, sikumbuki kama wakati wa Mkapa kulikuwa na tuhuma za rushwa za viongozi wa juu na kama zilikuwepo, sidhani kama zilikuwa za kutisha!

But look... alipotoka tu madarakani; uozo wakati wa Mkapa ukawekwa bayana! Na ninaweza kusema with confidence, hata utawala wa JK haukuwa corrupt kama utawala wa Mkapa manake tuhuma nyingi ambazo zili-hit sana wakati wa JK zilitokana na utawala wa Mkapa!!!

Maana yake nini?!

Unlike JK ambae aliacha watu na bunge wabonge wapendavyo na hivyo kashifa zote za ufisadi kufahamika mapema kabisa tena wakati akiwa bado madarakani, staili ya Magu ni kama ya Mkapa! Ben alikuwa mkali sana kuanzia kwa wabunge wa CCM hadi kwa media!

Sasa tuendelee kujipa matumaini kwamba anazuia wasitokee wanasiasa wengine mafisadi kama hatujakimbiana hapa watu wakianza kufukua mafaili baada ay JPM kutoka Magogoni!!
 
Hivi tuendelee tu na mtu anaejiita kichaa na anaonekana hivyo.
 
Screenshot_20181202-135930.png

Screenshot_20181202-135913.png

Screenshot_20181202-140604.png


Baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), bashiru Ally kumtaka aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Mambo ya nchi za nje, Benard Membe kwenda ofisini kwake kujibu tuhuma dhidi yake za kuanza Kampeni za kuwania urais 2020, Mwanasiasa huyo Mkongwe na anayesemekana kuitumikia taasisi nyeti ya Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania akiwa nje ya nchi aliitikia wito wa Dkt. Bashiru lakini akalalamikia utaratibu uliotumika kumuita huku akimtupia lawama mwanaharakati huru Cipryan Musiba kuwa ndiye aliyezusha madai kuwa anajiandaa na urais 2020.

Hata hazijapita siku mbili tangu KM kumtaka Membe aende ofisini kwake na Membe kuitikia wito, wamejitokeza marafiki zake wa.muda mfupi kurusha picha wakiwa naye na maneno ya hapa na pale kutaka kuuonesha Umma kuwa Membe ndiye na Wako na Membe na kamwe hawatamwangusha. Wanaahidi kula naye bata. Watu hawa ndiyo walewale ambao wamediriki hata kuhujumu jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika kuleta maendeleo, Kupambana na ufisadi na kutetea rasilimali za Taifa. Mbaya kabisa watu hawa wanaweka picha wakiwa na Membe na wazungu ambao uvibaraka wao kwao katika kulihujumu taifa ndiyo kwanza umepamba moto. Wameshindwa hata kuficha hisia zao na kumfichia siri mbobezi wao kama wanavyomuita. Kwanini Watanzania tusiamini alichokisema KM B. Ally? Kwanini Watanzania tusiamini mbobezi wao yuko nyuma ya ukibaraka wao ili wampigie debe kuelekea 2020?

Niwakumbushe akina Zitto, Lema, Jusa, Yeriko Nyerere na weingine ambao leo ndiyo wamjazao upepo mbobezi wao kwamba, 2015 Membe na Lowassa waliingia kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM lakini kukatwa kwa Membe haikuwa habari ya mjini bali kukatwa kwa Lowassa. Maana yake ni nini? Kama umaarufu wa kisiasa ungekuwa unaonekana na ukapinwa kwa urefu, basi Membe hamfikii Lowassa hata kwenye magoti. Lowassa alikatwa, akahamia Upinzani kwa mbwembwe, akateuliwa kugombea urais akakosa , hadithi ikaishia hapo na maisha yakaendeleo. Leo Lowassa anaonekana msaliti tena kwa Chadema kwa sababu tu ya kutaka angalau aonekane anazungumza na Mkuu wa nchi ikulu. Membe ni nani? Atakatwa, atahamia CHADEMA au ACT, mnajua hatakuwa na. Madhara yoyote kama ilivyotarajiwa kwa Lowassa, angalau Lowassa alifurukuta. Endeleeni kumjaza upepo bila shaka na nyie mmepata pa kupumulia baada ya kukosa hoja za kushindana na Serikai ya awamu ya tano, Serikali ya wanyonge, Serikali ya SGR, serikali ya stieglers Gorge, Serikai ya Madege, Serikali ya elimu bure, Serikali ya Maji kwa kila Mtanzania, Serikali ya Umeme nchi nzima, Serikali ya Barabara za juu na chini, Serikali inayowajali Wamachinga, Serikali ibayowatetea Wakulima wake waoate bei bzuri yq mazao yao, Serikali inayolinda rasilimali za nchi, Serikali inayopinga kwa nguvu zote Ushoga.

Aidha nimtahadharishe Membe. Apime uwezo wake na uwezo wa Lowassa kisiasa. Hawa wanaomjaza upepo leo ndiyo waliouanika ufisadi wa Lowasaa wakamuita kila aina ya jina mara Paka shume, mara Fisadi, mara jizi, ndiyo hao hao 2015 waliosema CCM haina uwezo wa kumkata Lowassa, Akakatwa akahamia. Kwao wakiamini sasa Upinzani unaingia ikulu kupitia yeye. CCM siyo Chama cha Mwenyekiti wa kudumu, CCM siyo chama. Cha Kiongozi wa Chama (Yule mwenyekiti alipoteuliwa kuwa RC basi Kiongozi wa Chama akavaa kofia zote, Chama kimebaki kuwa mali yake ). Lakini hata hivyo tangu lini Zitto, Lema, Yeriko Nyerere, Jusa na Upinzani kwa ujumla wao wakawa marafiki wa Membe? Lini? Labda mwenye kumbukumbu atuje.

CCM ni Taasisi, Lowassa alkatwa, Membe atakatwa na yeyote anayedhani anaweza kuwa juu ya CCM atakatwa tu na atang'ong'wa na hao anaodhani wanampenda kumbe wanatafuta pa kupumulia baada ya kufilisika kisiasa.

Labda tofauti ya hawa watu kwa Membe na Lowassa ni kwamba Lowassa walimtukana kwanza kabla ya kimtumia na sasa wanamuona mzigo, Kwa.Membe wameanza na kumpenda ili baadaye wamtumie na mwisho wake watamtukana na watamalizia na kumuona mzigo. Yote kwa yote hakuna atakayenufaika na kiki hizi, Siyo Membe, siyo Wapinzani wanaomtumia. Ni kama ilivyokuwa kwa Lowassa.

Nawasilisha
 
Ndugu zangu, huyu anayezungumzwa na kuandikwa kila chochoro, Hana jipya, wala hatakuwa na jipya.
Kukaa na kupoteza rasimali muda, huku ukimpigia "Promo za Kipuuzi" mtu ambaye hatakusaidia kwa lolote, huo nao ni upuuzi.

Ndugu zangu, huu ni Msimu wa "Maembe" Fanyeni biashara ya "Maembe"
Huyo "Membe" hatatusaidia chochote.

Sana sana atatuletea "Mende"

Asanteni, Ngoja nimpikie mume wangu kipenzi chakula cha lala salama.
Hakuna mtu anayesaidiwa na mtu chochote mana hakuna anayetoa pesa zake mfukoni kuendesha nchi.

Tunamtaka mtu atakayeondoa chuki kwa watanzania. Ubaguzi, upendeleo, ukanda, ukabila ,udini, siasa muda wote majukwaani tena siasa za chuki na kukashifiana huku kundi moja likinyimwa haki ya kujibu. Hatutaki kuishi kama watumwa kwenye nchi yetu tuliopewa na Mungu.

Hatutaki watu wanaoua imani zetu za kumwamini Mungu mmoja aliyeumba vitu vyote kwa kujigeuza wao ndio miungu ma wenye mamlaka juu ya kila kitu mpaka roho za watu ziko mikononi mwao na riziki wanagawa wao.
Tunataka kiongozi anayejijua kuwa yeye sio Mungu ni binadam na anakosea na hatakuja malaika kumkosoa Bali ni binadam wenzake hata kama hawapendi.

Tunataka mtu atakayejenga umoja wa watanzania bila kubaguana na kuweka watu was kutisha wenzao kama anavyofanya Msiba mkuu.

Tunataka mtu atakayeweka maendeleo kwa uwiano na sio maendeleo ya upande mmoja tu.
Tunataka mtu atakayeheshimu mihimili mingine na kuiacha itimize majukumu yake kwa haki. Bunge liwe live tuone wanapojadili mambo muhimu kwa ajili yaaisha yetu. Matokeo ya kuficha bunge ni hayo ya Sheria ya mafao kupitia bungeni bila kuonekana ilipitaje.
Na sheria ya vyama vya siasa nayo inataka kupita bila kujulikana itapitaje.

Tunataka mtu atakayeifanya nchi kuwa mahali salama kwa watu wote sio kwa watawala tuu.

Tunataka mtu atakayewafanya watumishi wote wa umma na watawala kuheshimu sheria na kuwa watiifu kwa wananchi wanaowapigia kura na wanaowalipa kodi ili walipwe mamilioni ya mishahara.

Tunataka kiongozi atakayejenga demokrasia na maadili ya uongozi kwa viongozi kupatikana kupitia sanduku la kura sio hila na kutisha na kuumiza watanzania wenzetu kwa sababu ya madaraka.

Tunataka kiongozi atakayeleta tume huru ya uchaguzi ili viongozi wapatikane kihalali na kwa haki. Nchi ikiwa na haki inakua na amani na furaja ndani ya mioyo ya watu.

Tunataka kiongozi atakayejenga mifumo na taasisi zenye kuwaheshimu watu na kujali uhai wa watu na Mali zao bila kuangalia tajiri,maskini, mkulima ,mfanyakazi ,mwanasiasa , mfanyabiashara n.k.

Tunataka mtu atakayejenga mifumo ya haki kuanzia kwenye chaguzi bila kutishwa au kufanya hila na kupata viongozi wa hila hila.

Tunataka mtu atakayeweza kusimamia rasilimali za nchi kama madini ,samaki, wanyama, misitu,gesi, utalii n.k kwa ajili ya kukuza uchumi sio kuficha hizo rasilimali kwa uchoyo na ubahili kama Mali binafsi ili wote tukose matokeo yake maskini wanaumizwa kwa kodi kila kukicha na rasilimali za nchi hazitumiki kwa ubunifu zaidi ya kiki za kisiasa.

Tunataka kiongozi hatutaki mtu wa kutusaidia kwa kupita na kutugawia hela mitaani kama ombaomba ili atufanye watumwa na kutegemea hisani kwa kodi zetu wenyewe.

Mwenyezi Mungu tunakuomba utupe akili za kumtambua kiongozi bora ifikapo 2020.
 
Back
Top Bottom