Hujui katiba ya chama inasema mwenyekiti wa chama ndo mgombea urais? Na uchaguzi wa chama kuchagua mwenyekiti ni mpaka 2022 jiwe tunae mpaka 2025
Tangazo hili limfikie aliyepo enzini mahali popote alipo...Hizi thread za B.Membe ndio kusema kampeni zimeshaanza au?
Au ni katika kumshawishi akishawishika wamte.k?Msimtafutie matatizo Bure...
Jiwe atakua wapi mpaka mumletee michezo hiyo?Habari za muda mabibi na mabwana!
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza nawashauri wanachama wenzangu na wananchi kwa ujumla. Mwaka 2020 tusipoteze tena kama ilivyotokea mwaka 2015. Haya yote ni kwa sababu hatukutulia vizuri katika mchujo wa kumpata kiongozi bora.
Karibuni kwa maoni yenu.
Amchukue tu uwezo si anao?Jiwe atakua wapi mpaka mumletee michezo hiyo?
Kama mnataka kumponza achukuliwe na wasiojulikana basi sawa.
Nyie watu mbona mnamtafutia huyu mzee balaa, sasa hivi atatekwa
Si rahisi kama unavyodhani...Namuonea huruma MEMBE atapotezwa muda sio mrefu
Kwa mara ya pili meenyekiti wa ccm anaenda kushindwa Chimwaga , wa kwanza alikuwa Kikwete .
Umewaza mbali sana Kamanda.Membe hatofanya miujiza maana CCM ni walewale..
ila yafuatayo;
1-Utekaji wa raia utapungua
2-Viongozi kuwatukana wananchi kutapungua
3-Ukanda, udini na ukabila utapungua
4-Watumishi kunyimwa haki zao kutapungua
5-Kesi za kipumbavu za kubambikiziana zitapungua
6-Sheria zitakazopitishwa hazitobeba hisia za mtu mmoja pekee kwa maslahi binafsi
7-Viongozi wenye phd kuacha facts na kutoa mipasho ya taarabu kutapungua
8-Viongozi wa kitaifa hawatowakimbia wananchi kwenye misiba
9-Kuhonga kodi ili uungwe mkono kutapungua
10-Ajira zitaongezeka
11-Askari wa Rwanda nchini watapungua
12-Mtanzania atakuwa na thamani zaidi kuliko mbwa wa polisi
13-Biashara zitakuwa maana unyonyaji utapungua
14-teuzi zitapungua
15-data za kupika zitapungua
16-kukurupuka kutapungua
17-hazina itaangaliwa na wale wote wenye mamlaka kisheria na sio mtu na mpwa wake pekee
18-watu watakuwa huru kufanya siasa, kutoa maoni
19-nchi itakuwa na jembe la uwakilishi nje ya nchi, haitakuwa tena tanzania ya kukimbiakimbia vikao vya wakuu wa nchi
20-njaa itapungua na furaha itaongezeka..
21-mawazo ya wasomi yatapewa nafasi yake
Basi sawaSi rahisi kama unavyodhani...