Si mwingine bali ni yeye mwanadiplomasia mbobezi Cammilius
Mpole mnyenyekevu mtaalam aliyebobea Jasusi
Ana huruma utu uungwana na hana visasi
Hawezi kuonea watu, kuwateka au kuwapiga risasi
Toka Mtukula, Pemba, Kigoma, Ruvuma hadi kule Masasi
Ni Bernard Cammilius atakuza uchumi kwa kasi
Chukua fomu baba muda ukifika nchi upewe
Tumechoka sisi kugeuzwa kuku kuonewa na mwewe
Nchi hii haina tena wa kuiokoa tunakukabidhi mikoba wewe
Tumekandamizwa sana, kubebeshwa zigo la jiwe
Cammilius baba huko uliko ubarikiwe
Tia nia kiongozi, tusonge mbele madhalimu waingiwe kiwewe
Tusamehe 2015 hatukujua ni kipi kitajiri huko mbele
Tukacheza makida, bila kujua tukapiga vigelegele
Sasa tumeshajua kuwa uongozi bora si uwezo wa kufoka na kupiga kelele
bali ni hekima uungwana, kufikiri na si ndulele
Tuliodhani ni wakombozi wanatuletea mambo ya kale
Wanabana kila kona, kila uhuru ili kinyonge watutawale
Taifa la Kambarage eti leo wanatugeuza misukule?
Hapana, Mzee baba kamata fomu tulale nao mbele kwa mbele
Washa moto Cammilius mzee baba tutafanya taifa letu jema tena
Walipoharibu rekebisha, mapya leta, Jamhuri iweze kufana
Sisi ni watu wazima, hawawezi kutugeuza wana
Kututia hofu ndani ya nchi yetu wenyewe, kutugeuza watwana
Watu wanatekwa, watu wanapotezwa, watu wanaokotwa kwenye viroba, mambo ya ajabu sana
Tunataka uhuru wetu, Uchumi, Elimu bora, afya njema, haki ktk nchi hayo ndo mambo ya maana
Tangaza nia kiongozi 2020 tusonge
Tumechoka sisi kugeuzwa wanyonge