Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Si mwingine bali ni yeye mwanadiplomasia mbobezi Cammilius
Mpole mnyenyekevu mtaalam aliyebobea Jasusi
Ana huruma utu uungwana na hana visasi
Hawezi kuonea watu, kuwateka au kuwapiga risasi
Toka Mtukula, Pemba, Kigoma, Ruvuma hadi kule Masasi
Ni Bernard Cammilius atakuza uchumi kwa kasi

Chukua fomu baba muda ukifika nchi upewe
Tumechoka sisi kugeuzwa kuku kuonewa na mwewe
Nchi hii haina tena wa kuiokoa tunakukabidhi mikoba wewe
Tumekandamizwa sana, kubebeshwa zigo la jiwe
Cammilius baba huko uliko ubarikiwe
Tia nia kiongozi, tusonge mbele madhalimu waingiwe kiwewe

Tusamehe 2015 hatukujua ni kipi kitajiri huko mbele
Tukacheza makida, bila kujua tukapiga vigelegele
Sasa tumeshajua kuwa uongozi bora si uwezo wa kufoka na kupiga kelele
bali ni hekima uungwana, kufikiri na si ndulele
Tuliodhani ni wakombozi wanatuletea mambo ya kale
Wanabana kila kona, kila uhuru ili kinyonge watutawale
Taifa la Kambarage eti leo wanatugeuza misukule?
Hapana, Mzee baba kamata fomu tulale nao mbele kwa mbele

Washa moto Cammilius mzee baba tutafanya taifa letu jema tena
Walipoharibu rekebisha, mapya leta, Jamhuri iweze kufana
Sisi ni watu wazima, hawawezi kutugeuza wana
Kututia hofu ndani ya nchi yetu wenyewe, kutugeuza watwana
Watu wanatekwa, watu wanapotezwa, watu wanaokotwa kwenye viroba, mambo ya ajabu sana
Tunataka uhuru wetu, Uchumi, Elimu bora, afya njema, haki ktk nchi hayo ndo mambo ya maana

Tangaza nia kiongozi 2020 tusonge
Tumechoka sisi kugeuzwa wanyonge
 
Mpaka siku wapinzani watapopata akili kwamba kila tukio linakuja kwa kusudi maalumu ndio angalau wanaweza kucheza vizuri karata za siasa zao!

Nacheka sana ninapoona watu wamekumbwa na upepo huu wa sasa unaoendelea hapa mtandaoni eti kuna mtu awe rais alafu eti kirahisi tu hivi kama kunywa maji?

Niwaambieni wapinzani nyie hata muwekewe kujifunza kwa picha hamtakaa muelewe.

Ikiisha hii movie ya Membe jiandaeni na nyingine pia.
Kwaiyo hiki kiuzi mmekifungua kujifariji???

Watu hawamtaki kichaaa hayo ya wapinzani ni maoni yako sio ulazimishe yawe unavyotaka

Pole sana jamaa anang'ooka huyo jiandae kumsindikiza Bujumbura
 
CCM, their CCM. Kama Lowassa pamoja na ushawishi na pesa alishindwa kuteuliwa kua mgombea katika kipindi kigumu kwa CCM huyu Snowden ndo hawezi kabisaaa. Ataishia kupata magonjwa ya kurithi tu
 
Si mwingine bali ni yeye mwanadiplomasia mbobezi Cammilius
Mpole mnyenyekevu mtaalam aliyebobea Jasusi
Ana huruma utu uungwana na hana visasi
Hawezi kuonea watu, kuwateka au kuwapiga risasi
Toka Mtukula, Pemba, Kigoma, Ruvuma hadi kule Masasi
Ni Bernard Cammilius atakuza uchumi kwa kasi

Chukua fomu baba muda ukifika nchi upewe
Tumechoka sisi kugeuzwa kuku kuonewa na mwewe
Nchi hii haina tena wa kuiokoa tunakukabidhi mikoba wewe
Tumekandamizwa sana, kubebeshwa zigo la jiwe
Cammilius baba huko uliko ubarikiwe
Tia nia kiongozi, tusonge mbele madhalimu waingiwe kiwewe

Tusamehe 2015 hatukujua ni kipi kitajiri huko mbele
Tukacheza makida, bila kujua tukapiga vigelegele
Sasa tumeshajua kuwa uongozi bora si uwezo wa kufoka na kupiga kelele
bali ni hekima uungwana, kufikiri na si ndulele
Tuliodhani ni wakombozi wanatuletea mambo ya kale
Wanabana kila kona, kila uhuru ili kinyonge watutawale
Taifa la Kambarage eti leo wanatugeuza misukule?
Hapana, Mzee baba kamata fomu tulale nao mbele kwa mbele

Washa moto Cammilius mzee baba tutafanya taifa letu jema tena
Walipoharibu rekebisha, mapya leta, Jamhuri iweze kufana
Sisi ni watu wazima, hawawezi kutugeuza wana
Kututia hofu ndani ya nchi yetu wenyewe, kutugeuza watwana
Watu wanatekwa, watu wanapotezwa, watu wanaokotwa kwenye viroba, mambo ya ajabu sana
Tunataka uhuru wetu, Uchumi, Elimu bora, afya njema, haki ktk nchi hayo ndo mambo ya maana

Tangaza nia kiongozi 2020 tusonge
Tumechoka sisi kugeuzwa wanyonge

N.B
MWANA JF KAMA NA WEWE UNAWEZA KUANDIKA MISTARI TUPIA HAPA
 
Back
Top Bottom