Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Kuna watu tukisema Membe aongoze nchi 2020 wanabeza
Wengine wanatuita sisi ni vibaraka Wa Membe kitu ambacho sio cha kweli, Mimi sio kibaraka Wa Membe wala mheshimiwa Membe Mimi hanijui

Kitu ninachoamini ndicho nitaendelea kuamini, kwa sasa watanzania tumebadilika japo tume ya uchaguzi na vyombo vya Dora ndio hawataki kubadilika wanaturudisha nyuma

Ile kanuni ya kwamba Raisi lazima atawale miaka kumi imepitwa na wakati
Tukikupa miaka mitano ikakushinda basi kaa pembeni waachie wengine wanaoweza

Kwa miaka mitatu tu hii mambo yanaenda kombo

Vijana hawana ajira, tangu nchi kupata Uhuru awamu hii ya tano ndio awamu ambayo vijana wengi wamerandaranda mitaani bila ajira hata zile ajira za ualimu, nursing, udaktari hazipo tena

Ndani ya miaka hii mitatu watu wamefukuzwa kazi hovyo hovyo wamekua tegemezi, watu wamerudishwa kwenye Lindi la umaskini, watumishi Wa umma hawajapanda madaraja wala kuongezwa mishahara, kila siku uhakiki uchwara usio na kikomo

Ndani ya miaka mitatu ahadi zimeshindwa kutekelezeka zimebaki ni ahadi hewa, milioni hamsini kila kijiji imekua longolongo tu, ajira kwa vijana kama mnavyojionea mwenyewe,

Ndani ya miaka mitatu tumeshuhudia kauli za kibabe zisizo na mashiko kwa wananchi na viongozi wengine, wananchi wananangwa, viongozi wanatishwatishwa hovyo hovyo kama watoto wadogo

Kwa miaka hii mitatu tumeshuhudia mtu mmoja kuwa one man show, kila kitu anataka awe fonti fedi sijajua ni kupenda sifa au ni nini

Ndani ya awamu hii ndio tumeshuhudia taifa linaingia kwenye gharama za mauchaguzi uchwara yasiyo na tija kodi za wananchi zinachezewa, wananchi tumefanywa wajinga kupindukia,

Kwahayo machache yapo mengine mengi japo yapo na mambo mazuri yaliyofanyika lakini tunasema asante na yatosha sasa

2020 yafaa kwenda na mtu mwingine naye ni Bernard Membe

Bernard Membe unafaa kutuongpza
Iwe mvua liwe jua tutakua nyuma yako

Hatuwezi tena kuwasapoti watu wasio na shukrani

2020 Twende na BENARD MEMBE[emoji818]

#MEMBE_FOR_PRESIDENT2020
Sio bure utakua umelipwa maana hizi juhudi siyo za kawaida, ili tuwe pamoja ebu tugawane
 
Kuna hatari ya Membe kufukuzwa uanachama wa ccm, otherwise akanushe kua yuko nyuma ya hizi mbio za kuwania uraisi.

JPM hawezi fanya haya, ni muoga sana yule mzee... na ndio maana anatumia nguvu kubwa sana kupambana na watu.. Membe ana muogopa maana anajua jamaa ni master, naishia kuugulia na kukasirima maana yule ni chaguo la kitengo toka 2015... ila ndio ivyo kosa likatokea
 
Membe ukimsikiliza anaongea kwa umakini mkubwa wala haongei kwa kufokafoka kila saa kama vile anafokea watoto wadogo, Membe analugha ya kidiplomasia maana yeye ni mwanadiplomasia mashuhuri. Hata penati aliyokosa samatta juzi juzi angekua Membe angeipata tu maana angatumia diplomasia kufunga Goli.
Hiyo diplomasia mbona haikuwahi kuipeleka Taifa Stars kwenye michuano yoyote?
Mwenzenu mwaka mmoja tu akina madarakani, tayari Vijana wetu wakaenda mashindano ya Afrika huko Gabon.
 
Membe ana sifa za kiuongozi, siyo kama huyu anayetumia misuli bila akili kwenye mambo yanayohitaji akili na nguvu kidogo
 
Tunaoujua michezo ya siasa tunakwambia chochote kinaweza tokea siku yoyote.
 
LAZIMA WAMCHOKE, UNANUNUA WATU HARAFU UNAWAPITISHA HAOHAO KIBABE BILA KUWASHINDANISHA LAZIMA WENYE CHAMA CHAO WAKUCHUKIE NO DEMOCRACY
 
Kelele za nini? Kama mtu amefanya yake akidhani anawatumikia ipasavyo na kumbe kashindwa kufikia matarajio yenu si kipindi kimoja kiki isha anakupeni mkono wa kwaheri kwa heshima na shukrani anaenda zake kula pension yake kwa amani?

Jambo hili liliwezekana kwa Raisi wa Zanzibar hayati Idrisa Abdul Wakili ambaye baada ya uongozi wake wa miaka 5 akaamua kwa hiari yake kuachiangazi na kutogombea tena ingawa alikuwa anajua kwa mfumo wa nchi hii ukitoka chama tawala kura wakitaka zitoshe zitatosha hata kama ziko mia tuu.

Nashangaa sasa hivi mjadala wa Magufuli VS Membe umepamba moto hasa kwa vile wanaccm wameonyesha kumchoka mwenyekiti wao naye kaonyesha mawimbi na ghoruba za bahari zimemzidi kama nahodha.

Mie namshauri bwana mkubwa kuwa aachane na wapambe wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili wale kwa ulaini, bahari imechafuka na dhoruba zaanza kuzamisha chombo chetu, 2020 akimuiga muungwana Abdul Wakili akamuachia unahodha mwingine kwa hiari kabla chombo hakijazama atajenga heshima.

Anaweza kuitumikia nchi hata kwa kutoa ushauri tuu.

Ya nini kubadilishana vijiti ionekane kama nongwa na kukasirikiana? Nyerere alisema hiyo kazi nzito sana, sasa kama mtu anataka kukupokea mzigo mzito kwa nini unanuna?
Sasa Membe akagombee Zanzibar basi!
 
Kwahiyo mkuu unatushauri tuendelee kutawaliwa na hawahawa ccm?

Jitafakari upya tatizo siyo Magufuli ba li tatizo ni ccm, ukikaa na ukatuliza akili utaelielewa hili vizuri, Magufuli ana kura moja tu hata kama ni ya veto, veto huwa haina nguvu ya kushindana na kura nyingi.

Ccm ni mashetani akiwemo huyo Membe, mateso tunayopitia leo hayaletwa na Magufuli bali ni mashetani wa ccm kuikataa rasimu ya katibsa mpya ya Warioba.

Someni biblia mtaelewa vizuri Mungu aliwachapa Waisrael pale walipokengeuka, na Watanzania wanastahili kuishi maisha magumu ili akili ziwarudie.
Hao wenzio ni manyumbu yani uadui wao na zao ninkwa magufuli tu basi! Yani wanaona tatizo ni magufuli,

Hawachukulii urais kama taasisi bali wanamuona magufuli tu basi.
 
Kelele za nini? Kama mtu amefanya yake akidhani anawatumikia ipasavyo na kumbe kashindwa kufikia matarajio yenu si kipindi kimoja kiki isha anakupeni mkono wa kwaheri kwa heshima na shukrani anaenda zake kula pension yake kwa amani?

Jambo hili liliwezekana kwa Raisi wa Zanzibar hayati Idrisa Abdul Wakili ambaye baada ya uongozi wake wa miaka 5 akaamua kwa hiari yake kuachiangazi na kutogombea tena ingawa alikuwa anajua kwa mfumo wa nchi hii ukitoka chama tawala kura wakitaka zitoshe zitatosha hata kama ziko mia tuu.

Nashangaa sasa hivi mjadala wa Magufuli VS Membe umepamba moto hasa kwa vile wanaccm wameonyesha kumchoka mwenyekiti wao naye kaonyesha mawimbi na ghoruba za bahari zimemzidi kama nahodha.

Mie namshauri bwana mkubwa kuwa aachane na wapambe wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili wale kwa ulaini, bahari imechafuka na dhoruba zaanza kuzamisha chombo chetu, 2020 akimuiga muungwana Abdul Wakili akamuachia unahodha mwingine kwa hiari kabla chombo hakijazama atajenga heshima.

Anaweza kuitumikia nchi hata kwa kutoa ushauri tuu.

Ya nini kubadilishana vijiti ionekane kama nongwa na kukasirikiana? Nyerere alisema hiyo kazi nzito sana, sasa kama mtu anataka kukupokea mzigo mzito kwa nini unanuna?

Akishasema ukimshauri ndio umeharibu kabisa.
 
Mtaimba Ngonjera na mashairi na tenzi zote Mwaka huu, Hizo siasa chafu haziepukiki Africa, what matters is Nchi ijengwe kwanza hizo siasa badae.
Ni haki kwa Raia kumweleza Raisi wao mambo mazuri au mabaya yanayoendelea katika nchi husika.
Kumzuia raia kutoa maoni ya kuikosoa serikali yake na kuishia tu kusifiasifia ni ujuha na haukubali kwa wenye uelewa mpana.
Raisi sio Malaika, na ana madhaifu yake ambayo ni lazima aelezwe ili ajirekebishe.
Wakati wa
" Zidumu Fikra na Matendo ya Mwenyekiti "
Umeshapitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom