Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio bure utakua umelipwa maana hizi juhudi siyo za kawaida, ili tuwe pamoja ebu tugawaneKuna watu tukisema Membe aongoze nchi 2020 wanabeza
Wengine wanatuita sisi ni vibaraka Wa Membe kitu ambacho sio cha kweli, Mimi sio kibaraka Wa Membe wala mheshimiwa Membe Mimi hanijui
Kitu ninachoamini ndicho nitaendelea kuamini, kwa sasa watanzania tumebadilika japo tume ya uchaguzi na vyombo vya Dora ndio hawataki kubadilika wanaturudisha nyuma
Ile kanuni ya kwamba Raisi lazima atawale miaka kumi imepitwa na wakati
Tukikupa miaka mitano ikakushinda basi kaa pembeni waachie wengine wanaoweza
Kwa miaka mitatu tu hii mambo yanaenda kombo
Vijana hawana ajira, tangu nchi kupata Uhuru awamu hii ya tano ndio awamu ambayo vijana wengi wamerandaranda mitaani bila ajira hata zile ajira za ualimu, nursing, udaktari hazipo tena
Ndani ya miaka hii mitatu watu wamefukuzwa kazi hovyo hovyo wamekua tegemezi, watu wamerudishwa kwenye Lindi la umaskini, watumishi Wa umma hawajapanda madaraja wala kuongezwa mishahara, kila siku uhakiki uchwara usio na kikomo
Ndani ya miaka mitatu ahadi zimeshindwa kutekelezeka zimebaki ni ahadi hewa, milioni hamsini kila kijiji imekua longolongo tu, ajira kwa vijana kama mnavyojionea mwenyewe,
Ndani ya miaka mitatu tumeshuhudia kauli za kibabe zisizo na mashiko kwa wananchi na viongozi wengine, wananchi wananangwa, viongozi wanatishwatishwa hovyo hovyo kama watoto wadogo
Kwa miaka hii mitatu tumeshuhudia mtu mmoja kuwa one man show, kila kitu anataka awe fonti fedi sijajua ni kupenda sifa au ni nini
Ndani ya awamu hii ndio tumeshuhudia taifa linaingia kwenye gharama za mauchaguzi uchwara yasiyo na tija kodi za wananchi zinachezewa, wananchi tumefanywa wajinga kupindukia,
Kwahayo machache yapo mengine mengi japo yapo na mambo mazuri yaliyofanyika lakini tunasema asante na yatosha sasa
2020 yafaa kwenda na mtu mwingine naye ni Bernard Membe
Bernard Membe unafaa kutuongpza
Iwe mvua liwe jua tutakua nyuma yako
Hatuwezi tena kuwasapoti watu wasio na shukrani
2020 Twende na BENARD MEMBE[emoji818]
#MEMBE_FOR_PRESIDENT2020
Kuna hatari ya Membe kufukuzwa uanachama wa ccm, otherwise akanushe kua yuko nyuma ya hizi mbio za kuwania uraisi.
Hapo ndo unaonyesha uwezo wako ndogo mno wa kufikiria,kununua wabunge unadhani ndo kuua upinzani?Jidanganyeni, tu, ikiwa upinzan unakufa ,je kwenye urais ndio mtatoboa?
Hiyo diplomasia mbona haikuwahi kuipeleka Taifa Stars kwenye michuano yoyote?Membe ukimsikiliza anaongea kwa umakini mkubwa wala haongei kwa kufokafoka kila saa kama vile anafokea watoto wadogo, Membe analugha ya kidiplomasia maana yeye ni mwanadiplomasia mashuhuri. Hata penati aliyokosa samatta juzi juzi angekua Membe angeipata tu maana angatumia diplomasia kufunga Goli.
Hawa jamaa wanamponza membe bila kujua yatamkuta ya Lowasa.Miluzi mingi humpoteza mbwa, wahenga walinena.
Wewe unapenda kutekwa ?Mtaimba Ngonjera na mashairi na tenzi zote Mwaka huu, Hizo siasa chafu haziepukiki Africa, what matters is Nchi ijengwe kwanza hizo siasa badae.
Sasa Membe akagombee Zanzibar basi!Kelele za nini? Kama mtu amefanya yake akidhani anawatumikia ipasavyo na kumbe kashindwa kufikia matarajio yenu si kipindi kimoja kiki isha anakupeni mkono wa kwaheri kwa heshima na shukrani anaenda zake kula pension yake kwa amani?
Jambo hili liliwezekana kwa Raisi wa Zanzibar hayati Idrisa Abdul Wakili ambaye baada ya uongozi wake wa miaka 5 akaamua kwa hiari yake kuachiangazi na kutogombea tena ingawa alikuwa anajua kwa mfumo wa nchi hii ukitoka chama tawala kura wakitaka zitoshe zitatosha hata kama ziko mia tuu.
Nashangaa sasa hivi mjadala wa Magufuli VS Membe umepamba moto hasa kwa vile wanaccm wameonyesha kumchoka mwenyekiti wao naye kaonyesha mawimbi na ghoruba za bahari zimemzidi kama nahodha.
Mie namshauri bwana mkubwa kuwa aachane na wapambe wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili wale kwa ulaini, bahari imechafuka na dhoruba zaanza kuzamisha chombo chetu, 2020 akimuiga muungwana Abdul Wakili akamuachia unahodha mwingine kwa hiari kabla chombo hakijazama atajenga heshima.
Anaweza kuitumikia nchi hata kwa kutoa ushauri tuu.
Ya nini kubadilishana vijiti ionekane kama nongwa na kukasirikiana? Nyerere alisema hiyo kazi nzito sana, sasa kama mtu anataka kukupokea mzigo mzito kwa nini unanuna?
😳😳😳Sisi wanaCCM kindakindaki wote tukiongozwa na Lizaboni jingalao Magonjwa Mtambuka Barbarosa MTAZAMO Mzee Mwanakijiji TUNAMTAKA MEMBE AWE RAIS WA TANZANIA KABLA YA 2020.
HalipendwiUmefanya utafiti?
Hao wenzio ni manyumbu yani uadui wao na zao ninkwa magufuli tu basi! Yani wanaona tatizo ni magufuli,Kwahiyo mkuu unatushauri tuendelee kutawaliwa na hawahawa ccm?
Jitafakari upya tatizo siyo Magufuli ba li tatizo ni ccm, ukikaa na ukatuliza akili utaelielewa hili vizuri, Magufuli ana kura moja tu hata kama ni ya veto, veto huwa haina nguvu ya kushindana na kura nyingi.
Ccm ni mashetani akiwemo huyo Membe, mateso tunayopitia leo hayaletwa na Magufuli bali ni mashetani wa ccm kuikataa rasimu ya katibsa mpya ya Warioba.
Someni biblia mtaelewa vizuri Mungu aliwachapa Waisrael pale walipokengeuka, na Watanzania wanastahili kuishi maisha magumu ili akili ziwarudie.
Kelele za nini? Kama mtu amefanya yake akidhani anawatumikia ipasavyo na kumbe kashindwa kufikia matarajio yenu si kipindi kimoja kiki isha anakupeni mkono wa kwaheri kwa heshima na shukrani anaenda zake kula pension yake kwa amani?
Jambo hili liliwezekana kwa Raisi wa Zanzibar hayati Idrisa Abdul Wakili ambaye baada ya uongozi wake wa miaka 5 akaamua kwa hiari yake kuachiangazi na kutogombea tena ingawa alikuwa anajua kwa mfumo wa nchi hii ukitoka chama tawala kura wakitaka zitoshe zitatosha hata kama ziko mia tuu.
Nashangaa sasa hivi mjadala wa Magufuli VS Membe umepamba moto hasa kwa vile wanaccm wameonyesha kumchoka mwenyekiti wao naye kaonyesha mawimbi na ghoruba za bahari zimemzidi kama nahodha.
Mie namshauri bwana mkubwa kuwa aachane na wapambe wanaompaka mafuta kwa mgongo wa chupa ili wale kwa ulaini, bahari imechafuka na dhoruba zaanza kuzamisha chombo chetu, 2020 akimuiga muungwana Abdul Wakili akamuachia unahodha mwingine kwa hiari kabla chombo hakijazama atajenga heshima.
Anaweza kuitumikia nchi hata kwa kutoa ushauri tuu.
Ya nini kubadilishana vijiti ionekane kama nongwa na kukasirikiana? Nyerere alisema hiyo kazi nzito sana, sasa kama mtu anataka kukupokea mzigo mzito kwa nini unanuna?
Ni haki kwa Raia kumweleza Raisi wao mambo mazuri au mabaya yanayoendelea katika nchi husika.Mtaimba Ngonjera na mashairi na tenzi zote Mwaka huu, Hizo siasa chafu haziepukiki Africa, what matters is Nchi ijengwe kwanza hizo siasa badae.