Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

 
ASANTE.
 
Jambo hili liliwezekana kwa Raisi wa Zanzibar hayati Idrisa Abdul Wakili ambaye baada ya uongozi wake wa miaka 5 akaamua kwa hiari yake kuachiangazi na kutogombea tena
Kwa hiari yake?
 
Kiongozi wangu mpendwa, mzalendo namba moja amekuwa akilalamika mara nyingi juu ya uzito wa jukumu la kuongoza taifa. Imefika kipindi alijuta kwanini alibeep. Naamini yeye mwenyewe anatamani kupumzika na atafanya hivyo hapo 2020 japo wengi tutatamani aendelee ila kwakuwa ana maamuzi yake binafsi ni vyema tuheshimu mawazo yake pia. Kwa jinsi tunavyompenda, apumzike tu kwakweli amefanya mengi mazito.
 
kwakweli siipendi CCM lakini pogba simpendi zaidi" Naomba hili suala la membe liwe kweli na ikibidi afaulu katika hili azimio lake"... ccm mlitukosea heshima sana kumpatia nchi huyu mkaanga sumu
Hakuna kitu kizuri kama kuwa na rafiki ambae mnafanana kwa hobby,interest,hisia,chaguzi,vilabu vya michezo na mambo mengine kama hayo.kwa kifupi Mkuu hearly,hii post yako mimi sio tu nimeipenda bali pia nitaitunza kama sala yangu siku ya kupiga kura ya serikali za mitaa,diwani,mbunge na hata rais.Nitayatumia maneno ya post hii kufanya maamuzi muhimu sana ya kuchagua bila kujali kama nitakaye mchagua atatangazwa mshindi ama la.
 
Kafanye utafiti then urudi.Usiongee kitu usichokijua. Bajeti ya jk kwa mwaka ilikua kwenye billion 300+ kwa jpm ni 400+.Sijui ka hili unalijua. Ushawah sikia migomo chuo kikuu kama enzi hizo?
Maandano ya jk yalitawanywa kwa maji ya kuwasha, wakati kichaa anatawanya kwa risasi za moto je ni nani aweza kusogeza pua kwny maandamano yanayotawanywa kwa risasi za moto?
 
Kama mnamuona anafaa mwambieni anzishe chama chake au ahamie CHADEMA ili mumchague 2020
Ila sisi bado tunamuhitaji JPM aendelee kuwanyoosha mafisadi
Wee unaongea Kama nani eti aanzishe chama chake ???? Humu humu. Hahami mtu na kampeni zinaendelea wee Kama hutaki hama wewe.
 
Ni jambo la kushitua mno kwamba wafuasi wa Chadema sasa wamegeuka kuwa wafuasi kindaki ndaki wa Bernard Membe na muda wote hakauki midomoni mwao.!

Ikumbukwe Bernard Membe ni mwana ccm lakini anapata mahaba makubwa kutoka chadema kuliko hata kutoka ccm!
Kwa sasa ikitokea Bernard Membe nagombea urais na Freeman Mbowe ,Bavicha wote watamchagua Bernard Membe na kumtosa Mbowe!

Membe kukosa urais inawauma mno Chadema kuliko hata Membe mwenyewe inavyomuuma!

Swali la kujiuliza ,ni nini kimewatokea Bavicha hadi wakawa wafuasi wa kada wa ccm na kuacha viongozi wao wa Chadema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…