Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Bora agombee Humphrey Polepole kuliko ......
 
Sasa ulitaka ndani waandamane? Ni mpaka nguo zianikwe ndiyo unajua kuwa jirani yako leo alifua.
Kuna underground movement ndani ya chama tawala.... kada wakawaida nivigumu kulijua kuna wenye chama wanataka chama chao "wamepigana mistuni zaidi ya miezi 8 kwaajiri ya chama".....
 
Kuna underground movement ndani ya chama tawala.... kada wakawaida nivigumu kulijua kuna wenye chama wanataka chama chao "wamepigana mistuni zaidi ya miezi 8 kwaajiri ya chama".....
Kuna wastaafu pia ambao hawafutahii ramani inavyokwenda.
 
Ndoto hizi zimepitwa na wakati, kinachozungumzwa hapo naona ni ndelemo na vifijo kwa mtu asiyeonekana
 
Lowassa alitumia miaka 10 kujitangaza mitandaoni na kuwatumia viongozi wa dini eti wanamuomba kugombea urais na zaidi ya yote lowassa alikuwa kila mtu mwenye harambee lowassa anaomba awe mgeni rasmi na kutoa mafedha kedekede , akaanza kupanga safu yake ya uongozi kwenye jumuiya za ccm kuanzia vijana, UWT, jumuiya ya wazazi , wajumbe wa NEC , wajumbe Wa mkutano mkuu.
Kikwete akiwa rais akawa anamchora tu akijua wapi atakapomfyekelea mbali, kikwete yeye akaanza kupanga safu ndogo sana ya kamati ya maadili Kwa kuwaweka watu wake na kuhakikisha watu wenye damu ya lowassa hawapo,ilipofika muda kikwete akiwa na kamati isiyozidi watu 10 akamfyekelea mbali.
Shikamoo kikwete

Acha kusifu dhambi,
 
Kumekuwa na ubishani mkubwa kwamba Membe hawezi kumtoa Magufuli 2020 kwa sababu katika historia ya Tanzania hilo halikuwahi kutokea. Mimi nasema hapana,yote yanawezekana na sababu zipo lukuki!

Nikiangalia kwa upande wa CCM Mwanadiplomasia Bernard Membe ndiyo mtu pekee anayeweza kupindua meza kibabe pale CCM.

Acheni mawazo duni. Mbona babu zetu waliamini Nyerere na wenzake wangeweza kupindua meza kibabe ya mkoloni. Iliwezekana vipi?Ni mikakati kabambe inahitajika na siyo jambo la kitoto.

Sababu za Membe kufanikiwa hili ni nyingi kuliko kushindwa kwake.

1. Kutokubalika kwa Magufuli ndani na nje ya CCM

2. Kukosekana kwa utengamano wa kweli

3. Nia ya kuirudisha Tz kimataifa

4. Nia ya kurudisha mchakato wa Katiba ya Watanzania

5.nk

........... itaendelea(nitafafanua)
Kwa masikitiko naomba nikiri Mkapa alikuwa sahii kuwaita Wap.....
 
KINGUNGE

“Kitendo cha kuinyang’anya Kamati Kuu mamlaka yake ni kibaya, wanajiita kamati ya maadili wakati kamati yenyewe haina maadili, hii nchi ni yetu sote hata chama ni chetu sote wachache tuliowapa madaraka ndani ya chama na serikali wanadhani nchi ni yao,”

KILA LA KHERI KACHERO MEMBE
 
Kwa utaratibu wa CCM raisi aliyepo madarakani anakaa miaka 10 labda itokee kifo.Kwa raisi huyu hamna mtu wa kuchukua fomu 2020 sijui lakini yajayo.Ataendelea JPM ili andeleze yale aliyo yaanzisha.Tumuache JPM achape kazi,badala kuleta mada amefanya nini hii 3 years mnaleta mambo ya 2020.
 
Wakuivusha Tz kwenda wapi huyo?,ameshindwa wakati akiwa Foreign Affairs.Taasisi ya uraisi haijaribiwi.Tumuache raisi achape kazi.
 
Duh kwa hyo unamaanisha bora ccm iendelee kutawala? Mm nilitegemea ungemuelezea mgombea wa upinzani anayefaa na atayekuea raisi, lakini tunarudia makosa yaleyale ya kutaka ccm iendelee kutawala tena kupitia membe!
 
KINGUNGE

“Kitendo cha kuinyang’anya Kamati Kuu mamlaka yake ni kibaya, wanajiita kamati ya maadili wakati kamati yenyewe haina maadili, hii nchi ni yetu sote hata chama ni chetu sote wachache tuliowapa madaraka ndani ya chama na serikali wanadhani nchi ni yao,”

KILA LA KHERI KACHERO MEMBE
Kwa nn membe na sio upinzani? Bado tuna hamu ya ccm kutawala?
 
Tunaenda na Magu mpaka 2022 ( Miaka 7 awamu ya kwanza) then anatuchukua awamu ya pili mpaka 2029 akimaliza hana cha kuongeza muda then ndio tunaanza kujadili wengine wa kumrithi
Hiyo imekaa vizuri kiongozi haaa hhaaa
 
Back
Top Bottom