Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Hata kwa akili za kuazima tu mkuu,unamwona Magufuli anafaa kabisa kutuvusha?
Kaharibu kila kitu kwa muda mfupi tu,watu wanateseka mitaani na ugumu wa maisha mnawaita wapiga dili mirija imefungwa,can't you be serious?
Mama lishe,muuza mchicha nao walikuwa serikalini wakipiga dili?
Acheni utani na mambo mazito ya nchi,Magufuli hafai kabisa

Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
Membe ndio angeharibu zaidi....hii nchi ingekuwa kama Zimbabwe au Venezuela mkuu
...go for Magufuri over Membe mkuu
 
Kwani katiba ya chama chao cha kijani inasemaje?
Huyu aliyeko madarakani si mpaka amalize miaka 10 au?
Au kuna mabadiliko.
 
Maandiko matakatifu yanasema hivi , " AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU " kwa namna unavyoandika humu kila siku ni kama unamtegemea Magufuli kuliko hata moyo wako unaokusaidia kuishi , Magufuli , mtu ambaye yeye mwenyewe binafsi wala wazazi wake hawakuwahi kuijenga ccm ni nani katika ccm , hata isiwezekane kung'olewa ? kwa taarifa yako huyu aliyeua chama kwa kutegemea polisi anang'oka kirahisi mno , hana mizizi yoyote , haungwi mkono na wastaafu wala hata kanisa analosali .
 
Viongozi wetu wa taifa hili wamebarikiwa na wameweza kutufikisha hadi hapa tulipo, kuanzia Nyererr, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na inshallah 2020 ningependa nafasi iende kwa Membe

Ni mtu mwelewa, diplomatic, jasiri, mwenye hekima na alieelimika.

Namkubali Raisi wetu wa sasa ambae ni mchapa kazi, ila tu binafsi namwelewa zaidi Membe.

Inshallah Bernard Member utakuwa raisi 2020


Ikiwa nimefanya uchochezi wa aina yoyote unaoenda kinyume na katiba na sheria za nchi hii nawaombeni mnijulishe
 
Kwahiyo ukimwelewa wewe maanake watz wote million 59 tumemkubali????? Akili za watz mungu ingilia kati uwiiii
 
Tunataka Rais KIJANA!
Tupo pamoja kwenye hili. Nnasikitika sana kuona watu wanawapigia promo watu wazee waje kuwa marais. Tukubali tukatae ili nchi yetu isonge mbele zaidi tuachane na hawa wagombea wazee watatuchelewesha sana. Maana wengi wao mitizamo yao ni tofauti sana na speed ya mabadiliko ya mambo inayoendelea kwa sasa duniani
 
Nataka nijue kitu kimoja..je haiwezekani mkutano mkuu wa ccm kumkataa rais aliyeboronga na kumwachie mwingine agombee?Maana huyu jiwe hafai hata kwa bure!
 
Back
Top Bottom