Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Kuna watu tukisema Membe aongoze nchi 2020 wanabeza
Wengine wanatuita sisi ni vibaraka Wa Membe kitu ambacho sio cha kweli, Mimi sio kibaraka Wa Membe wala mheshimiwa Membe Mimi hanijui

Kitu ninachoamini ndicho nitaendelea kuamini, kwa sasa watanzania tumebadilika japo tume ya uchaguzi na vyombo vya Dora ndio hawataki kubadilika wanaturudisha nyuma

Ile kanuni ya kwamba Raisi lazima atawale miaka kumi imepitwa na wakati
Tukikupa miaka mitano ikakushinda basi kaa pembeni waachie wengine wanaoweza

Kwa miaka mitatu tu hii mambo yanaenda kombo

Vijana hawana ajira, tangu nchi kupata Uhuru awamu hii ya tano ndio awamu ambayo vijana wengi wamerandaranda mitaani bila ajira hata zile ajira za ualimu, nursing, udaktari hazipo tena

Ndani ya miaka hii mitatu watu wamefukuzwa kazi hovyo hovyo wamekua tegemezi, watu wamerudishwa kwenye Lindi la umaskini, watumishi Wa umma hawajapanda madaraja wala kuongezwa mishahara, kila siku uhakiki uchwara usio na kikomo

Ndani ya miaka mitatu ahadi zimeshindwa kutekelezeka zimebaki ni ahadi hewa, milioni hamsini kila kijiji imekua longolongo tu, ajira kwa vijana kama mnavyojionea mwenyewe,

Ndani ya miaka mitatu tumeshuhudia kauli za kibabe zisizo na mashiko kwa wananchi na viongozi wengine, wananchi wananangwa, viongozi wanatishwatishwa hovyo hovyo kama watoto wadogo

Kwa miaka hii mitatu tumeshuhudia mtu mmoja kuwa one man show, kila kitu anataka awe fonti fedi sijajua ni kupenda sifa au ni nini

Ndani ya awamu hii ndio tumeshuhudia taifa linaingia kwenye gharama za mauchaguzi uchwara yasiyo na tija kodi za wananchi zinachezewa, wananchi tumefanywa wajinga kupindukia,

Kwahayo machache yapo mengine mengi japo yapo na mambo mazuri yaliyofanyika lakini tunasema asante na yatosha sasa

2020 yafaa kwenda na mtu mwingine naye ni Bernard Membe

Bernard Membe unafaa kutuongpza
Iwe mvua liwe jua tutakua nyuma yako

Hatuwezi tena kuwasapoti watu wasio na shukrani

2020 Twende na BENARD MEMBE✔

#MEMBE_FOR_PRESIDENT2020
 
Majanga haya. Leo vijana wa bavicha niwakumpigia debe mwana CCM tena kuwa raisi wa nchi hii kweli? Naapa nakukata tamaa ya kurudi kwenye chama cha upinzani.
Hii ni hatari sana
 
Wakuu samahani kwa kuwa outdated
Hivi Membe kafanya nini hasa?! Maana naona ghafla ana trend kila kona ya mtandao
Naomba msaada wa maelezo mafupi wa alichofanya au hata link nisome walau nipate mwanga
Watu wanaomshabia huyo Membe sijui kama wana nia nzuri na nchi hii
....viva Magufuri viva
 
Naona kama mnajifurahisha, yaani naona kama Maigizo, watu na akili zenu mnakaa mnadanganyana Membe anaenda kuchukua nchi 2020.

Mimi na akili zangu za kuvukia barabara nauliza ATAPITIA NJIA GANI?

Ndani ya CCM , Mwenyekiti ndiye mgombea urais na ndiye mwenye sauti ya mwisho ,

Kupitia Upinzani ,ndio kabisa hawezi kushinda , Tuliona kwa LOWASSA,.
Labda kama ana hela za kuchezea,

Kupitia Uhaini, hapa atadakwa mapema sana..

NAWAULIZA NYIE MLIOKULA HELA ZAKE NA KUTUMWA MITANDAONI , MNAJUA ATAKUWA RAIS KWA NJIA GANI?

Mtuambie, sio mnasumbua mitandaoni lakini hamtuambii atapitia njia gani , ya golgotha au kaanani,

JIWE ameshajizatiti ana JESHI, TISS, UHAMIHAJI, POLIS , TUME YA UCHAGUZI,N.K

MEMBE ana nini? Au anataka kuliwa hela zake kama Lowassa?
 
Nyie mtamponza mzee wa watu ........

Kwan amewaambieni kuwa anampango huo au mnataka kutuaminisha nini?!

Mtamponza mzee wa watu yatamkuta makubwa bure ile hali hata hakuwa na mpango huo.....hebu kausheni ....
 
MEMBE ANAWEZA ASIWE RAIS 2020 LAKINI CV YAKE NI APPLICABLE INTERNATIONALLY. HIVYO KWA WATU WASOMI WA KUANZIA KIWANGO CHA KATI NA WENYE ULEWA KUHUSU DIPLOMASIA BASI LAZIMA WAMUUNGE MKONO.
 
Back
Top Bottom