Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Naona kama mnajifurahisha, yaani naona kama Maigizo, watu na akili zenu mnakaa mnadanganyana Membe anaenda kuchukua nchi 2020.

Mimi na akili zangu za kuvukia barabara nauliza ATAPITIA NJIA GANI?

Ndani ya CCM , Mwenyekiti ndiye mgombea urais na ndiye mwenye sauti ya mwisho ,

Kupitia Upinzani ,ndio kabisa hawezi kushinda , Tuliona kwa LOWASSA,.
Labda kama ana hela za kuchezea,

Kupitia Uhaini, hapa atadakwa mapema sana..

NAWAULIZA NYIE MLIOKULA HELA ZAKE NA KUTUMWA MITANDAONI , MNAJUA ATAKUWA RAIS KWA NJIA GANI?

Mtuambie, sio mnasumbua mitandaoni lakini hamtuambii atapitia njia gani , ya golgotha au kaanani,

JIWE ameshajizatiti ana JESHI, TISS, UHAMIHAJI, POLIS , TUME YA UCHAGUZI,N.K

MEMBE ana nini? Au anataka kuliwa hela zake kama Lowassa?
UFIPA WAMEJIANDAA KULA PESA ZA GADDAFI KAMA WALIVYOKULA PESA ZA RICHMOND.
 
Siasa za bongo bwana.....ndio maana tunafeli kila uchao.....

Huwa tunawachukulia watu wanaogombea nafasi za uongozi kama "movie characters" na si watendaji!
 
Usichokijua ni kwamba hiyo Miliion 50 kwa kila kijiji ilikuwepo kwenye Ilani ya Uchaguzi 2015 sa sijui kama angekuwa Membe ndiye mgombea angefuta hicho kipengere ama vipi! Jibu unalo mwenyewe.

Watanzania walitaka mabadiliko, Sasa jiulize mabadiliko waliyoyataka Watanzania wakati awamu ya nne inatoka madarakani tungepata kitu cha tofauti kama Membe angekuwa Rais? Unamuona Membe akiwa na utofauti kati yake na Membe?

Mabadiliko ya Kweli ypo kwa JPM. Tulizoea kuiba sasa fanya kazi kihalali upate mshahara wako wa halali. Membe angekuwa Rais wala asingeweza kuajili kila Mwananchi wa Tanzania. Membe anekuwa Rais labda angekodi Ndege sio kununua katu, SGR mradi angepewa Mchina tena kwa mkopo wa riba ya hatari, Meli ziwa Victoria! Sidhani Mradi wa maji Rufiji asingewaza hilo! namuombea JPM amalize salama kwenye awamu zake zote 2 alafu tutarudi tena hapa kufanya tathimini.
 
MEMBE ANAWEZA ASIWE RAIS 2020 LAKINI CV YAKE NI APPLICABLE INTERNATIONALLY. HIVYO KWA WATU WASOMI WA KUANZIA KIWANGO CHA KATI NA WENYE ULEWA KUHUSU DIPLOMASIA BASI LAZIMA WAMUUNGE MKONO.
We don't need a popular or international president, we only need Tanzania president, And JPM is the President till 2025.
 
Atapitata barabarani, vichochoroni, majini na angani..tafuta njia mwenyewe sisi tunalo jibu teyari.
#TimeForMembe#
 
Kuna watu tukisema Membe aongoze nchi 2020 wanabeza
Wengine wanatuita sisi ni vibaraka Wa Membe kitu ambacho sio cha kweli, Mimi sio kibaraka Wa Membe wala mheshimiwa Membe Mimi hanijui

Kitu ninachoamini ndicho nitaendelea kuamini, kwa sasa watanzania tumebadilika japo tume ya uchaguzi na vyombo vya Dora ndio hawataki kubadilika wanaturudisha nyuma

Ile kanuni ya kwamba Raisi lazima atawale miaka kumi imepitwa na wakati
Tukikupa miaka mitano ikakushinda basi kaa pembeni waachie wengine wanaoweza

Kwa miaka mitatu tu hii mambo yanaenda kombo

Vijana hawana ajira, tangu nchi kupata Uhuru awamu hii ya tano ndio awamu ambayo vijana wengi wamerandaranda mitaani bila ajira hata zile ajira za ualimu, nursing, udaktari hazipo tena

Ndani ya miaka hii mitatu watu wamefukuzwa kazi hovyo hovyo wamekua tegemezi, watu wamerudishwa kwenye Lindi la umaskini, watumishi Wa umma hawajapanda madaraja wala kuongezwa mishahara, kila siku uhakiki uchwara usio na kikomo

Ndani ya miaka mitatu ahadi zimeshindwa kutekelezeka zimebaki ni ahadi hewa, milioni hamsini kila kijiji imekua longolongo tu, ajira kwa vijana kama mnavyojionea mwenyewe,

Ndani ya miaka mitatu tumeshuhudia kauli za kibabe zisizo na mashiko kwa wananchi na viongozi wengine, wananchi wananangwa, viongozi wanatishwatishwa hovyo hovyo kama watoto wadogo

Kwa miaka hii mitatu tumeshuhudia mtu mmoja kuwa one man show, kila kitu anataka awe fonti fedi sijajua ni kupenda sifa au ni nini

Ndani ya awamu hii ndio tumeshuhudia taifa linaingia kwenye gharama za mauchaguzi uchwara yasiyo na tija kodi za wananchi zinachezewa, wananchi tumefanywa wajinga kupindukia,

Kwahayo machache yapo mengine mengi japo yapo na mambo mazuri yaliyofanyika lakini tunasema asante na yatosha sasa

2020 yafaa kwenda na mtu mwingine naye ni Bernard Membe

Bernard Membe unafaa kutuongpza
Iwe mvua liwe jua tutakua nyuma yako

Hatuwezi tena kuwasapoti watu wasio na shukrani

2020 Twende na BENARD MEMBE✔

#MEMBE_FOR_PRESIDENT2020
Tunaomba tu CCM mtuletee huyu ndugu maana ana mikono yenye baraka na ataleta mahusiano mapya ndani na nje ya TZ.. Hana uadui wa kikabila wala wa kishangazi. Ni msomi na mwenye utashi wa kiuongozi na hekima.. Kwa kweli Anatufaa sana .. CCM mtupe raha 2020 kupitia Membe
 
Tuwe wakweli tu angekuwa membe hakuna ajuayw angekuaje,tusidangante watu kuwa angekuwa mbaya au mzuri
 
Back
Top Bottom