Majukumu aliyonayo rais ni makubwa mengi na yanachosha akili na mwili pia, Jana rais mwenyewe amekiri uzito wa kazi aliyonayo kiasi kwamba alisema, ukiingia chumbani mwake utashangaa kuona mafaili yamejaa hadi kitandani, kukiri kwake huko ni sawa na kutoa rai kwetu tumsaidie.
Nafikiri sasa ni muda mwafaka kabisa kwa CCM kumsaidia rais kwa kutenganisha kofia mbili ya urais na uenyekiti isivaliwe na mtu mmoja, rais abaki kuwa rais akitekeleza majukumu ya urais ambayo ni mengi full-time job, na mwenyekiti wa chama abaki kuwa mwenyekiti. Pamoja na kumsaidia rais itaondoa mwingiliano wa majukumu kiutendaji, leo rais akizungumza huwezi kujua kazungumza kama rais au mwenyekiti wa CCM.
Hili wazo sii geni, mabadiliko haya yameshaanza ndani ya chama kwa baadhi ya ngazi za chama, baada ya mwenyekiti wa CCM Iringa Albert Chalamila kuteuliwa kuwa RC Mbeya aliambiwa achague moja kuendelea kuwa mkiti au mkuu wa mkoa, kwanini ishindikane kwa ngazi ya taifa.
Baada ya kutenganisha 'rasmi' kwa maana ya kubadili baadhi ya vifungu vya katiba ya chama, mwanachama yeyote aruhusiwe kugombea uenyekiti, tofauti na sasa ambapo wanachama wa kawaida haruhudiwi kugombea uenyekiti hadi awe rais.
Mawazo Yangu.