Ni mtazamo binafsi lakini wenye kuakisi ukweli... CCM inaandaliwa kuingia kwenye wakati mgumu tena, ni mtifuano wa ndani kwa ndani
. Urais 2020
. CCM asili dhidi ya CCM makinikia(mabaki)
. CCM kindakindaki dhidi ya CCM maslahi (wakuja)
Bernard Camilius Membe diplomat na jasusi wa muda mrefu, mshindwa wa kinyang'anyiro cha urais ngazi ya chama bado hajakubali kushindwa, bado ana ndoto ileile ya kukalia kiti kikubwa na amekamia hasa
Haiba ya Membe ni reincarnation ya haiba ya Kikwete (carefree) ni tofauti kabisa na haiba ya mzee baba KUKAZA hasa.... Membe ni expert mzuri sana kwenye mahusiano ya kimataifa, na pengine kwenye ushushushu lakini si kwenye siasa tena kukalia kiti kikubwa
Kipindi kile wakati wa kutafuta nafasi ya kuteuliwa, hakuonesha tofauti na wanaccm wengine, hakuongea cha ziada, wote walifanana... Hakutupa dira na maono ya tulipotoka, tulipo na tunapoelekea.. Wote katika ujumla wao ndani ya CCM walifanya mahubiri ya kisiasa
Akiwa shina moja na JK, ana sehemu kubwa ya lawama nchi ilipokuwa imefikia kipindi kile, kumpa usukani na kuendelea kuchanja mbuga kuelekea maporini
Sasa basi kwanini nasemwa asibezwe?! Huyu ni tarumbeta ya kupaza sauti ya wanaccm wengi wanaougulia kimyakimya na kushindwa kuongea kwa uwazi, kwa sauti
Huyu ni sauti ya manung'uniko ya wanaccm wengi ambao hawaridhishwi kabisa na mwenendo wa chama kwenye kila kitu lakini kubwa kuliko yote ni kule kuwapa wahamiaji (haramu) madaraka na nafasi za upendeleo... Wanapatwa na hisia kuwa kuna CCM mpya inaundwa taratibu ndani ya CCM halisi (CCM ya mwenyekiti dhidi ya CCM ya wote)
Ni kupitia hayo kwa uchache ndani ya mengi chamani, Membe ananijenga kwa kasi ya ajabu, na harakati zake hizo zilianza mara baada ya uchaguzi mkuu.... Membe ana kundi kubwa nyuma yake.. Ni vigumu kumdhibiti kama walivyodhibitiwa kina Makamba Jr, Lameck, Nape nk.. Huyu ni kada mzoefu chamani na wa muda mrefu... Ametumwa...!!
2019 hiyoo bado siku chache tu, Membe yuko nje ya nchi anakotuhumiwa kupanga mambo yasiyowapendeza watu fulani.. Huku wengine wakiona ni sawa... Hapa ni swala la mizania.. Nani ana wafuasi wengi zaidi wa hiari...
Membe anarudi kukanusha/kujibu tuhuma,.. Anajipanga kisawasawa, ameshaanza kusafishiwa njia na timu zake mitandaoni .... Ni yeye tu ndio anasikika na kujadiliwa... Na kwa sehemu kubwa akisemwa vizuri na akitabiriwa vema... Hivi vitu havifanyiki kwa bahati mbaya... Ni mipango inayosukwa kwa ustadi sana..
Hivyo basi pamoja na kwamba hatoshi kukalia kiti kikubwa, lakini ni tishio kubwa... Akiamua (kwa nguvu ya wapambe wake) ataiteka December yote.... Atavuruga hasa... Atawavuruga.... Na CCM itaingia 2019 ikiwa mapande makubwa matatu
. CCM mwenyekiti
. CCM Membe
. CCM wengine
Ujumbe huo wa Nape unabeba siri kubwa nyuma ya kinachoendelea sasa chamani... Muda utasema.. View attachment 952923
Siasa na drama za chama tawala.
Wanajua vizuri walifanyalo.
Sasa badala ya opposition wakomae na yao watakuwa taken away na haya matukio ya kutengeneza hata wajiingize huko wasahau yao.