Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

mimi si mfuasi wa siasa za Tz maana ndizo zimetufikisha hapa lakini lazma nitoe mtazamo wangu kwa hili.

Membe anaweza kuwa na haiba ya Kikwete ambaye kwa kipindi hicho naye alipwaya (japo anasafishwa kutokana na madhaifu ya aliyepo), lakini Membe hana uwezo ambao kikwete alikuwa nao.Wakati akiwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa hakuwa fanya kitu cha mshangao na alipokuwa akihojiwa sikuona substance na charisma ya kiuongozi simply alibebwa na mfumo ila alikuwa na uwezo hafifu..

Akheri kwa sasa tunabanwa lakini kuna projects zinafanyika ambazo unaona dhahiri kizazi kijacho kitanufaika ila kumpa nchi Membe ni risk iliyopo dhahiri..

Kwangu mimi Rais ambaye anatakiwa kumrithi Magufuli ni lazma awe mafia yaani aweze kuwa economical diplomat(sio mambo ya kutabasamu hovyo na kusema hawa ni marafiki zetu toka uhuru), Strategist, atakayekubali katiba mpya , visionary, mwenye upendo na uchungu na nchi hii na kadhalika..

Vigezo vyote hivyo Membe hana hata kimoja zaidi ya uswahiba na kufananishwa na Kikwete
Uwanja wa Chato?

Kuwalipa wastaafu 25%?

Kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari?

Kuua wapinzani?

Hivi unajisikia unachosema??
 
Ni mtazamo binafsi lakini wenye kuakisi ukweli... CCM inaandaliwa kuingia kwenye wakati mgumu tena, ni mtifuano wa ndani kwa ndani
. Urais 2020
. CCM asili dhidi ya CCM makinikia(mabaki)
. CCM kindakindaki dhidi ya CCM maslahi (wakuja)
Bernard Camilius Membe diplomat na jasusi wa muda mrefu, mshindwa wa kinyang'anyiro cha urais ngazi ya chama bado hajakubali kushindwa, bado ana ndoto ileile ya kukalia kiti kikubwa na amekamia hasa
Haiba ya Membe ni reincarnation ya haiba ya Kikwete (carefree) ni tofauti kabisa na haiba ya mzee baba KUKAZA hasa.... Membe ni expert mzuri sana kwenye mahusiano ya kimataifa, na pengine kwenye ushushushu lakini si kwenye siasa tena kukalia kiti kikubwa
Kipindi kile wakati wa kutafuta nafasi ya kuteuliwa, hakuonesha tofauti na wanaccm wengine, hakuongea cha ziada, wote walifanana... Hakutupa dira na maono ya tulipotoka, tulipo na tunapoelekea.. Wote katika ujumla wao ndani ya CCM walifanya mahubiri ya kisiasa
Akiwa shina moja na JK, ana sehemu kubwa ya lawama nchi ilipokuwa imefikia kipindi kile, kumpa usukani na kuendelea kuchanja mbuga kuelekea maporini

Sasa basi kwanini nasemwa asibezwe?! Huyu ni tarumbeta ya kupaza sauti ya wanaccm wengi wanaougulia kimyakimya na kushindwa kuongea kwa uwazi, kwa sauti
Huyu ni sauti ya manung'uniko ya wanaccm wengi ambao hawaridhishwi kabisa na mwenendo wa chama kwenye kila kitu lakini kubwa kuliko yote ni kule kuwapa wahamiaji (haramu) madaraka na nafasi za upendeleo... Wanapatwa na hisia kuwa kuna CCM mpya inaundwa taratibu ndani ya CCM halisi (CCM ya mwenyekiti dhidi ya CCM ya wote)
Ni kupitia hayo kwa uchache ndani ya mengi chamani, Membe ananijenga kwa kasi ya ajabu, na harakati zake hizo zilianza mara baada ya uchaguzi mkuu.... Membe ana kundi kubwa nyuma yake.. Ni vigumu kumdhibiti kama walivyodhibitiwa kina Makamba Jr, Lameck, Nape nk.. Huyu ni kada mzoefu chamani na wa muda mrefu... Ametumwa...!!

2019 hiyoo bado siku chache tu, Membe yuko nje ya nchi anakotuhumiwa kupanga mambo yasiyowapendeza watu fulani.. Huku wengine wakiona ni sawa... Hapa ni swala la mizania.. Nani ana wafuasi wengi zaidi wa hiari...
Membe anarudi kukanusha/kujibu tuhuma,.. Anajipanga kisawasawa, ameshaanza kusafishiwa njia na timu zake mitandaoni .... Ni yeye tu ndio anasikika na kujadiliwa... Na kwa sehemu kubwa akisemwa vizuri na akitabiriwa vema... Hivi vitu havifanyiki kwa bahati mbaya... Ni mipango inayosukwa kwa ustadi sana..

Hivyo basi pamoja na kwamba hatoshi kukalia kiti kikubwa, lakini ni tishio kubwa... Akiamua (kwa nguvu ya wapambe wake) ataiteka December yote.... Atavuruga hasa... Atawavuruga.... Na CCM itaingia 2019 ikiwa mapande makubwa matatu
. CCM mwenyekiti
. CCM Membe
. CCM wengine
Ujumbe huo wa Nape unabeba siri kubwa nyuma ya kinachoendelea sasa chamani... Muda utasema.. View attachment 952923
Mshana naheshimu mchango,wako, ila nina swali moja ...
Hv nyie mnaosema BM hatoshi Je mnazingatia nn hasa..
Na je kwani,huyu aliyepo anatosha..?

Majib please
 
🤔🤔🤔

Embu kwanza niambie mabaya gani haswa unaona uchaguzi ungekuwa leo hasingeshinda.. maana hayo matatu kwangu naona hayafuniki mazuri ambayo wananchi wengi wapiga kura nchini wanaona anafanya.. wala kumshusha kiungozi..

Pia uliyosema wananchi wengi... wewe umeamua tu kusema hauna proof ya hilo.. kwa sababu mfano kama ni viongozi hao wabunge kura zao haziwezi badili kitu.. wakulima pesa wanalipwa zaidi ya walizokuwa wanajua watapata.. hao utawaambia nini lingine now..
Ya pensheni nijuavyo mimi kuna nchi waliostaafu wanaishi kwa kupokea malipo kila mwezi..


Ha ha haaaaaaaa
Naona umepokea dozi ingine

Unaandika kutaka kunishusha.. hata sijui nini kinakuwasha washa juu ya Cocochanel

Hii ni forum.. nitaandika nitakavyo.. na uandishi wangu humu umekufanya upende kunisoma..

Weww tabu yako ni ulishaanza kyisoma namba tangu.. so lolote unalobwabwaja kwangu wewe ni pupwuu mjaa upupwu.

Acha wivu juu yangu.. huniwezi.. jiandikie jisome

Ukinisoma tegemea 💉💉💉💉💉💉 zaidi na zaidi..

Ulitaka nikufundishe juu ya kuandika ukiwa umefikiria dk 5 mbele.. karibu.. bila kusahau luchungulia nyuma pia..

Huniwezi kabisaaaaaaa.. halafu lazima unaandikaga upupwu kisa wataka kuona upinzani ukipaaa.. unajua haiwezekani.. never.. kaa tu CCM ulipokuwepo tangu uisome namba.. na segerea uende jambwazi.
We kibinti acha ujinga Mimi ntakuwezaje wakat unakung'utwa na jiwe.
 
Pendekezo lako ni jema sana lakini hiyo katiba mpya tutaipata wapi na kwa nani?[emoji848]
Katiba Mpya itatokana na sisi wananchi...cha msingi ni kupaza sauti...ipo siku milango ya gereza itafunguka...cha msingi ni kujiamini na kuwa na umoja....

Kama namba tunasoma wote, basi umoja upo karibu....wafanyakazi na wakulima wote wanalia...Katiba ipo karibu...ngoja kuni za wastaafu zichochewe tu...katiba ipo njiani....
 
Tunataka mkali + hapana asiwe mkali + tunataka anayesafiri + hapana hatutaki Vasco dagama + tunataka anayecheka + hapana hatutaki anayecheka cheka = ?
 
Tunataka mkali + hapana asiwe mkali + tunataka anayesafiri + hapana tunataka asiyeenda nje + tunataka anayecheka + hapana hatutaki anayecheka cheka = ?
Unamaanisha kuwa hatujui tunachokitaka au?[emoji848]
 
Katiba Mpya itatokana na sisi wananchi...cha msingi ni kupaza sauti...ipo siku milango ya gereza itafunguka...cha msingi ni kujiamini na kuwa na umoja....

Kama namba tunasoma wote, basi umoja upo karibu....wafanyakazi na wakulima wote wanalia...Katiba ipo karibu...ngoja kuni za wastaafu zichochewe tu...katiba ipo njiani....
Natamani sana iwe hivyo ila huu umoja wetu ndio unaonipa wasiwasi
 
Kwani Magu anafanya nn pale ikulu hadi membe ashindwe. Kuteua na kutengua? . 2020 twende na membe
 
Kwa jicho langu la 3 sijaona chochote Membe atakuja kufanya kumpiku JPM, JPM ni Rais mwenye maono makubwa! Naimani mpaka JPM anastafu 2025 Tanzania itakuwa mbali!

Membe ni mpigaji tu! gas itauzwa yote mikataba yote ya ovyo itarudi wapigaji watarudi kwenye system.

Sikumchagua JPM ili aje anipe ugali maana nilijua ifikapo mbeleni mi mwenyewe ndiye nitaangaika kuhakikisha napata ugali.

JPM endelea kuchapa kazi, tengeneza mazingira mazuri ya miundombinu ya barabara, reli, meli na ndege maana ndiyo kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi.

Niko tayari kumpigania JPM.
 
Kuitambua hatima ya CCM siku zijazo ni kazi sana unaweza omba miwani ili uone vizuri.Ni wachahe sana wanaoaminiana njia rasmi ya kuiokoa CCM ni kutumia polis na TISS ila hadi lini itakuwa hivi nadhani inabidi tutambue hiki ni kizazi kingine kizazi kinachotaka mabadiliko ya haraka tuwekeze kwa vijana.
 
Jiwe ni gunia la misumari. Ni muuaji, watanzania hawamhitaji tena. Anaua wastaafu kimya kimya.
 
tusimlishe maneno.
CCM ni chama imara chenye mfumo madhubuti, mihula miwili ya urais ni sehemu ya utaratibu wa kudumu na unaheshimiwa na kila mwanachama mtiifu wa ccm akiwemo BM kamwe hawezi kuwa muuasi labda awe nje ya ccm lkn sio ndani ya ccm
utaratibu wa zanzibar na bara mbona haupo tena
 
We kibinti acha ujinga Mimi ntakuwezaje wakat unakung'utwa na jiwe.

Ha ha ha haaaaaaa
Eeeeeeeh
Yaani unaonyesha kweli awamu hii 💉💉💉

Ukionana nae mwambie Cocochanel ni shabiki wake na nitapenda kumsalimia.. usisahau akiwa mahala uwe unanishtua ikiwa ni area niliyopo nitaenda nimuone.. hata kwa mbali maana sijawahi kumuona uso kwa uso.

Kwa sasa pokea tu 💉💉💉💀🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom