Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Ukisema Membe aendelee kujiandaa
Paskali eidha IQ yako iko juu sana,au unafanya kazi za Kitengo,au vyote kwa pamoja..nimejaribu kukufuatilia lakini..daah!!! kama wewe ni mwandishi wa kujitegemea tu kama (unavyotuaminisha) na huyo ndugu yako hajagundua Talent yako tu basi kuna tatizo la IQ huko juu.
 
Habari za muda mabibi na mabwana!

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza nawashauri wanachama wenzangu na wananchi kwa ujumla. Mwaka 2020 tusipoteze tena kama ilivyotokea mwaka 2015. Haya yote ni kwa sababu hatukutulia vizuri katika mchujo wa kumpata kiongozi bora.

Karibuni kwa maoni yenu.

====
MANENO KUNTU HAYO NI NANI KAMA MEMBE !!
 
wamejadili na wamekuja na uamuzi wa pamoja. jiulize, ingekuwa kwa chama chako mbowe angefanya haya hata walau kujipa muda wa kulitafari jambo hilo kwa undani? CCM imeonesha ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa.
Ni kwa nini kuhusu CCM unataja chama lakini kuhusu CHADEMA unamtaja Mbowe!?
 
Ni kwa nini kuhusu CCM unataja chama lakini kuhusu CHADEMA unamtaja Mbowe!?
kwa sababu CCM si mali ya mtu binafsi ila CHADEMA ni mali ya mtu binafsi kwa hiyo kila inapotajwa CHADEMA lazima litajwe jina la mwenye mali
 
Nani kakwambia ccm si mali binafsi
kwa sababu CCM si mali ya mtu binafsi ila CHADEMA ni mali ya mtu binafsi kwa hiyo kila inapotajwa CHADEMA lazima litajwe jina la mwenye mali
 
Ccm mpya mwenye chama kuunda chama kipya ndani ya chama cha zamani
Najaribu tu kuwakumbusha wale wenye tabia za kusahau kuwa kwenye hii CCM mpya hakuna aliye maarufu kuliko chama, na lolote lawezekana kwa yeyote. Tuache tabia ya kukariri tafadhali.

Niishie hapo!
 
Mwaka 2015 , Tanzania ilikuwa na uchaguzi mkuu wa madiwani, ubunge na urais.

Nitajikita zaidi kuzungumzia chama cha Mapinduz, chama tawala kwa zaidi ya miaka 23, kimekuwa kikishika dola na kupata nafasi ya kuunda serikali,

Niweke wazi mapema, mimi ni mwanachama wa chama cha CHAUMA.

Mwaka 2015 katika mchakato wao wa kupata mgombea wa urais kupitia chama chao hicho, kulikuwa na mtifuano na mnyukano wa hali ya juu sana hasa kwa watu wawili waliojiandaa kikamilifu kuwa rais wa Tanzania, Benard Kamilius Membe na Edward Ngoyai Lowasa.

Hawa watu wawili walijiandaa kushika nafasi hiyo kubwa kabisa ya uongozi wa nchi, Kwa bahati mbaya na sababu wazijuazo ccm wakampitisha Dr John Magufuli kuwa mgombea wao , ambae pia ndiye rais wetu kwa sasa.

Kwa hakika katika kosa tulilofanya Watanzania mwaka 2015 ni kumchagua mtu kuwa rais wetu ambaye hakujiandaa kuwa rais, sideeffects zake ndizo hizi tunazohangaika nazo leo na kwa sasa kila.mtu analia kama sio kwa sauti basi analilia tumboni.

Kwa sasa tuna rais ( Waziri wa ujenzi na miondombinu) ambaye ameshindwa kutuongoza na tayari watanzania wengi wamelitambua hilo, miaka 3 tu ya utawala wake, tayari tumeanza kuwaza replacement yake 2020 tofauti kabisa na awamu zilizopita.

Katika wale wawili wa 2015 waliokuwa wamejiandaa kushika nafasi ya urais, ni mmoja ambaye bado yupo na sifa zaidi ya kushika nafasi ya urais 2020 na kutuvusha Watanzania, huyu ni Bernard Kamilius Membe.

Watanzania, tuna miaka 2 ya kujipima na kutafakari na kuamua ma hatimae 2020 tufanye maamuzi sahihi , tusifanye makosa tena ya 2015.

Ni mimi Mwl Ukweli kutoka Ushetu.
 
Yaani wenye kuweza kufanya mabadiliko ya urais katika nchi hii ni CCM tu. Huo ukweli unajulikana japo watu tumekuwa wagumu kuukubali.

Kwa tume ipi ya uchaguzi itakayompa madaraka mpinzani hata kama atashinda?

Msijifanye hamjui hii nchi!




Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom