Mwaka 2015 , Tanzania ilikuwa na uchaguzi mkuu wa madiwani, ubunge na urais.
Nitajikita zaidi kuzungumzia chama cha Mapinduz, chama tawala kwa zaidi ya miaka 23, kimekuwa kikishika dola na kupata nafasi ya kuunda serikali,
Niweke wazi mapema, mimi ni mwanachama wa chama cha CHAUMA.
Mwaka 2015 katika mchakato wao wa kupata mgombea wa urais kupitia chama chao hicho, kulikuwa na mtifuano na mnyukano wa hali ya juu sana hasa kwa watu wawili waliojiandaa kikamilifu kuwa rais wa Tanzania, Benard Kamilius Membe na Edward Ngoyai Lowasa.
Hawa watu wawili walijiandaa kushika nafasi hiyo kubwa kabisa ya uongozi wa nchi, Kwa bahati mbaya na sababu wazijuazo ccm wakampitisha Dr John Magufuli kuwa mgombea wao , ambae pia ndiye rais wetu kwa sasa.
Kwa hakika katika kosa tulilofanya Watanzania mwaka 2015 ni kumchagua mtu kuwa rais wetu ambaye hakujiandaa kuwa rais, sideeffects zake ndizo hizi tunazohangaika nazo leo na kwa sasa kila.mtu analia kama sio kwa sauti basi analilia tumboni.
Kwa sasa tuna rais ( Waziri wa ujenzi na miondombinu) ambaye ameshindwa kutuongoza na tayari watanzania wengi wamelitambua hilo, miaka 3 tu ya utawala wake, tayari tumeanza kuwaza replacement yake 2020 tofauti kabisa na awamu zilizopita.
Katika wale wawili wa 2015 waliokuwa wamejiandaa kushika nafasi ya urais, ni mmoja ambaye bado yupo na sifa zaidi ya kushika nafasi ya urais 2020 na kutuvusha Watanzania, huyu ni Bernard Kamilius Membe.
Watanzania, tuna miaka 2 ya kujipima na kutafakari na kuamua ma hatimae 2020 tufanye maamuzi sahihi , tusifanye makosa tena ya 2015.
Ni mimi Mwl Ukweli kutoka Ushetu.