Urais 2025 kwa tiketi ya CCM ni mtifuano hasa

Urais 2025 kwa tiketi ya CCM ni mtifuano hasa

Ni hivi mnajadili CCM 2025, lakini ukweli ni kua wabongo wamechoka sana na hili li chama na wako tayari sasa hivi kuupa upinzani nchi.
Wapinzani wajipange tu 2025 wanaichukua nchi kirahisi sana,hatuwezi kuongozwa na mzanzibar wakati bongo ina watu milioni 60 na uchafu. kwanza nchi imeshamshinda huyu mama ni gender tu inayomlinda kwa sasa na genge la Msoga. 2025 nchi ni ya wapinzani hii.
Kapata jina jipya "Mama Tozo"
 
Hii ni dhana tu unayoitunga hapa.

Huyo mama angeonyesha uwezo wa kuongoza dhana yako isingekuwepo. Mama hana uwezo wa uongozi, sio tu kwa sababu yeye ni mwanamke.
Nchi yetu imejaa wapigaji na wajanjawajanja wengi,kuongoza mwanamke ni ngumu Sana.
Sanasana wanaokula mezani kwake ndo watapinga ukweli.

Mwendazake pamoja na ukali wake aliendelea kutumbua watendaji mpaka alipoitwa na Israel.
Hi miaka anayomalizia mama ahakikishe Mambo yote ya wazanzibari yamekaa sawa,wasije kumlaumu.

Maana hiyo 5 ni fumbo,naogopa historia maana inatabia ya kujirudia.Yaliyotokea kwa Joyce Banda yasije jirudia.
 
Mkuu samahani mm sio Ngosha na wala siko upande ule ila nayaona yanayoratibiwa na wao. Ni suala la muda Tu nawe utagundua jambo Lao.
Labda mwenyewe awe hana Nia ya kugombea 2025. Nguvu za Mwenyekiti wa CCM kwa wanachama wake ni nyingi kuliko nguvu Rais wa Tanzania kwa wananchi. Mwenyekiti anaweza akaanzisha zengwe la kukufuta kama Magufuli alivyo mfuta Benard Membe na asiulizwe na mtu.

Sana sana wenye kuutaka Urais inabidi wajikombe vizuri kwake ili mwaka 2030 awaunge mkono.
 
Kama vipi mama apindue meza, amalizie 4 aliyorithi kwa JPM. Halaf aanze na mikumi yakwake hadi 2035, amwachie Doroth Gwajima.
Sisi wanaume tumeshatawala sana toka uhuru, sasa ni zama ya wa kina mama.
Wanawake hoyeeeeee
 
Kama vipi mama apindue meza, amalizie 4 aliyorithi kwa JPM. Halaf aanze na mikumi yakwake hadi 2035, amwachie Doroth Gwajima.
Sisi wanaume tumeshatawala sana toka uhuru, sasa ni zama ya wa kina mama.
Wanawake hoyeeeeee
Hahaha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji2996]

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Naomba Gwajima kama mnamawasiliano nae mumwambie achukue fomu awe na timu ya watu wawili Polepole na Jerry slaa.
Wengine anaweza kuongezea
 
Mama yupi Mkuu? Huyu huyu au mwingine? Kawekewa mtego na tayari keshanaswa. Hana pakupumulia tena. "Wasukuma Wanaamini kuwa ng'ombe wanaoswagwa na mwanamke kamwe hawafiki mnadani" . Dalili tayari ziko wazi.
Kule kanda ya ziwa wataupiga mwingi sana kwenye uchaguzi ujao, waswahili wana msemo wa usitukane mamba ungali hujavuka mto. Sina uhakika kama ushawishi wa boyz2men utakuwa na nguvu safari hii huko kanda ya ziwa, akina ngosha wanawasoma tu.
 
Wewe inaonyesha ni mbumbu wa katiba hii ni awamu ya sita kwa hiyo 2025 CCM anachukua form mtu mmoja tu rais aliyepo madarakani mtifuano utakuwa mwaka 2030. Soma katiba zote mbili ya CCM na ya jamhuri ya muungano. Mama hatoki mpaka awamu yake ya miaka 10 iishe


Nakubaliana na wewe asilimia zote, alivyo wavalisha watu barakoa na kutii hana mpinzani wasubirie 2030 tu.
 
Namna pekee ya kumzuia mwenyekiti wa CCM wa sasa asipeperushe bendera yao come 2025 ni either (1)Aaamue mwenyewe bila shinikizo kutokuchukau form au (2) afe/auawe. Otherwise hawana cha kumfanya kwa kuwa Katiba yao ipo wazi na mtu mwingine yeyote serious hatopewa form.

Msijitoe ufahamu
 
Samia hatakua na mpinzani ndani ya chama 2025 mark my words….

Mchezo wa Samia kukaa hapo alipo ulisukwa kwa ustadi mkubwa sana…

Ilikua either Samia, Asha rose au Mary Nagu….2015

Trust me Samia is there until the mission accomplished!!

Hii nchi Boys2men wanazichezea siasa zake kwa akili ya juu sana!

Ulipowataja Asharose Migiro na Mary Nagu hoja yako ikapata ulemavu. Huwezi kuwa na running mate anayetoka upande uleule wa Muungano anaotoka presidential candidate!
 
Tafadhalini tusipewe tema Msukumamizigo.
Bado wana ushamba flani kama alivyotamka Napelepe.
Wa kujilinganisha na mungu Dogani.
 
Kuna kila dalili ndani ya chama mfumo dume umetamalaki na una mizizi mirefu sana. Kuna kundi kubwa huko haliamini katika uwezo wa mwanamke kushika nafasi kuu kwenye utawala/uongozi wa nchi. Wengine ni kutokana na tamaduni mila na desturi zao. Na wengine ni kutokana na unyanyapaa tu na silika za mfumodume zilizojengeka miongoni wao. Ni kati yao hawa wote tayari wanapiga jalamba kuelekea 2025.

Hakuna anayetaka kuharibu lakini kila mmoja anaomba mwenzake aharibikiwe

Kila mmoja ana timu zake zinazodukua na kutafuta taarifa za wengine. Kila mmoja ana wapambe wake, wapiga filimbi wake, chawa wake nknk.. Ni mwendo wa kutafutana kimya kimya!

Vinara front liners au front contenders ni wale wale vijana wetu ndani ya chama wanaotaka kuwapiga chini wazee
Waziri wa fedha
Aliyewahi kuwa waziri wa mazingira
Aliyewahi kuwa waziri wa afya na utalii pia
Kuna pia yule waziri mwenye asili mbili
Na wengineo

Wote wanajiweka vizuri kielimu.. Tayari wawili wana PhD. Wote kwa nyakati tofauti walipiga pesa ndefu za chama na serikali pia. Wanafahamiana vizuri tu nani alipata ngapi kwenye nini..wote wana miradi mingi na wanaingiza vipato vya kutosha sana

Wote wana ushindani mkubwa sana. Wanataka kuoneshana ubabe wao kwa wao. Huyu waziri wa sasa wa kibubu amepata pa kupigia kiulaiiini sana na ni wazi wenzake wanaona gere kupitiliza, lakini naye hana hakika kama atadumu kwenye hiyo nafasi mpaka 2025 kwahiyo sasa ni mwendo wa chukua chako mapemaaa

Common sharing iliyopo kati ya wote hawa ni moja, hawataki katiba mpya wanajua hicho ni kitanzi cha ndoto zao...! Hi yo basi tutarajie drama za kila aina

Drama za tozo na miamala
Drama za wapingao chanjo
Drama za bidhaa kupanda bei
Drama za usalama nknk

Vitu vidogo vidogo vitakuzwa na kuhakikisha vinabaki midomoni mwa watu kwa muda mrefu. Mama atakimbizwa kimbizwa sana ili wenye mipango yao wajipange vema.

Ni mchakamchaka kuelekea 2025[emoji2996][emoji2996][emoji2996][emoji2996]

Sio kwa Bongo yetu; labda Mama aamue kujiweka pembeni mwenyewe. Otherwise, atakayetaka kushindana na kiti ataambulia kuzittokabweiwa tu!
 
Back
Top Bottom