Urais CCM: Mchakato wa wagombea Urais ndani ya chama kuanza Juni 15- Juni 30

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,421
Ratiba ya mchakato wa kumpata wagombea wa CCM wa Urais Tanzania inaanza June 15,2020 hadi June 30,2020 ambapo Watu watachukua na kurejesha fomu kisha baada ya hapo vikao vya uchujaji vitaanza.

July 09, 2020 kitaketi kikao cha Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM ambayo itatoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu ya Taifa juu ya majina ya wanachama waisozidi watano wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

July 10, 2020 kitaketi kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa ya Chama chetu ambacho kitakuwa na kazi ya kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, majina yasiyozidi matatu ya wanaoomba dhamana ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

July 11 hadi July 12 ,2020 utaketi Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambao utakuwa na kazi ya kuchagua jina moja la Mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Urais kwa tiketi ya CCM.
 
Vip kuna ambao wataruhusiwa kuchukua fomu au ule utamaduni unaendelea?
 
Ni vizuri,,ila mi nashauri tuendelea na ile desturi yetu
 
Wabunge na madiwani wenyewe bado waendelee kusubiria, au mchakato unaenda concurently-?
 
Ratiba ya mchakato wa kumpata wagombea wa CCM wa Urais Tanzania inaanza June 15,2020 hadi June 30,2020 ambapo Watu watachukua na kurejesha fomu kisha baada ya hapo vikao vya uchujaji vitaanza.

July 09, 2020 kitaketi kikao cha Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM ambayo itatoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu ya Taifa juu ya majina ya wanachama waisozidi watano wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

July 10, 2020 kitaketi kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa ya Chama chetu ambacho kitakuwa na kazi ya kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, majina yasiyozidi matatu ya wanaoomba dhamana ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

July 11 hadi July 12 ,2020 utaketi Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambao utakuwa na kazi ya kuchagua jina moja la Mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Urais kwa tiketi ya CCM.
Najiandaa kwenda kuchukua form ya kugombea urais kwa tiketi ya ccm. Sijui watanipa hiyo form bila mizengwe
 
Back
Top Bottom