“Ratiba ya mchakato wa kumpata wagombea wa CCM wa Urais Tanzania inaanza June 15,2020 hadi June 30,2020 ambapo Watu watachukua na kurejesha fomu kisha baada ya hapo vikao vya uchujaji vitaanza” -POLEPOLE
•
“July 09, 2020 kitaketi kikao cha Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM ambayo itatoa mapendekezo kwa Halmashauri Kuu ya Taifa juu ya majina ya wanachama waisozidi watano wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”-POLEPOLE
•
“July 10, 2020 kitaketi kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa ya Chama chetu ambacho kitakuwa na kazi ya kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, majina yasiyozidi matatu ya wanaoomba dhamana ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”-POLEPOLE
•
“July 11 hadi July 12 ,2020 utaketi Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ambao utakuwa na kazi ya kuchagua jina moja la Mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa Urais kwa tiketi ya CCM”-POLEPOLE