Ushirombomoya
Member
- May 11, 2021
- 77
- 143
Binafsi ni mdau wa makazi yaliyopangwa na kupewa matumizi kulingana na mpango wa eneo husika.
Kifupi uwa ninahisi kero kupita sehemu ambazo zina ujenzi holela, kwa mantiki hiyo nimekuwa nashawishika kununua maeneo yaliyopimwa. Nilifanikiwa kununua eneo Dodoma (mtumba) na kufanya malipo kikamilifu.
Baada kufanya malipo kikamilifu nikajaribu kufuatialia hati kwenye mfumo wa e ardhi nako ikaonekana taarifa za kiwanja hazisomani hii ni ajabu, muuzaji ni serikali na mfumo ni wa serikali tena wizara husika ambao wanajinadi kuwa maombi tufanye kupitia mtandao wao ila unakutana na changamoto hii!
Basi baada ya kushindwa kutuma maombi ya hati kwa mfumo wa e ardhi kutokana na changamoto tajwa hapo juu, ikabidi nifunge safari hadi Dodoma.
Nikafika Dodoma salama na kwenda moja kwa moja ofisi ya ardhi, hapo ndipo nikajua Nchi hii kuna miungu watu, siku ya ijumaa kumuona afisa ardhi ni kama umepata bahati ya kushinda mchezo wa kubahatisha.
Nikauliza ila nikapewa majibu ya kuwa siku ya ijumaa ofisi ya ardhi haifanyi kazi, kichwani nikajiuliza je nipo nchi nyingine! Ila nimeshuhudia watu wengine wakipewa huduma licha ya maneno na maelekezo ya ofisi ya kitengo cha ardhi kuwa ijumaa hawafanyi kazi za nje.
Japo najua watumishi wa serikali wanatakiwa kufanya kazi hadi ijumaa, sawa wao wamepanga kufanya hivyo je wametupa taarifa wadau wote?
Kwa hali nchi hii haiwezi kuepukana na makazi holela, maana maafisa ardhi wamekuwa miungu watu. Gharama tunalipia, kodi tunalipa kwa serikali ila hatuna maana, nchi hii ni ngumu kupiga hatua ya maana kwa utendaji huu.