Habari za Mwisho wa wiki wana jamaa...
Napenda kuwasalimu nyote, na kila mmoja katika imani yake...
Baada ya salamu naomba niende moja kwa moja kwenye mada kama inavyojieleza.
Imekua kama fasheni kukuta wadada wametupia zigo la shanga kwenya mauno yao, sasa huwa najiuliza je wanafahamu kua wazee wetu walizitumia kuwasiliana na wenza wao??
Nilikua najua niurembo tu ila siku moja mzee mmoja katika maongezi walipita wadada hatareeee... shanga kiunoni kama mzinga wa nyuki, story zikaanzia hapo.
Mzee: Ulishawahi kukutana na mwanamke mwenye shanga na unajua nini maana yake?
Mimi: Hapana mzaa, (huku nikiwa na shahuku ya kujua) kwani zinamaana gani?
Mzee: Zamani izo zilikua zinavaliwa kwa sababu maalum na kwa njia ya kuwasiliana, wamama walivaa shanga za aino tofauti kutoa ujumbe tofauti kwa waume zao.
Mimi: Inakuaje hapo? Walikua wanatumiaje?
Mzee: Kwa mfano; Mwanamke akiwa hedhi, alivaa shanga NYEKUNDU na hapo mumewe alikua anajua kua leo hakuna mchezo.
Mimi: Mmhm...
Mzee: NJANO zilikua zinaashiria huko kwenye kumaliza safe zone na kukaribia hedhi
KIJANI zilimaanisha yuko tayari kupata mtoto... (Fertilization)
NYEUPE alikua anamaanisha kua anahamu ya kufanya tendo kwa kuenjoy za kwa mda zaid.
NYEUSI ilikua inamwambia mwanaume asijaribu kuomba game japo yupo safe zone
Hizi zilitumika kutokana na HESHIMA waliyokua nayo wazee wetu ilikutotumia maneno tofauti na kizazi cha sasa ambapo watoto wa miaka 12 kuongelea swala la ngono ni jambo la kawaida kabisa..
"Sasa nini nikawanajiuliza, hizi dada zetu wa leo, Je mnafahamu haya? Au Mzee aliniambia tuu sababu sikua na ufahamu wa hili jambo"
Wajuzi wa mabo naombeni maono yenu katika hili na pia mtujuze zaidi...
Ahsanteni.