Kuna vitu hata havitakiwi kujadiliwa, ukitaka kufanya jambo kwa kudhamiria kuwafurahisha watu utapotea.
Hereni za masikioni wapo hawaziafiki, mwingine hasuki nywele, utakutana na asiyevaa suruali, yupo anavaa sketi fupi mwingine ndefu za kufunika miguu yote, hapo sijaongelea aliyetoboa pua, ulimi, kuweka kichuma juu ya jicho au kidevuni, wanaopigilia bangili...wote hao ukisema utafsiri wanamaanisha nini utaumia kichwa bila sababu.
Kama inakukera, mweleze mwenza wako lakini usilazimishe wengine kufuata unachokiamini wewe kuwa sahihi.