Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada

Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada

nliwahi kuuliza hl swali nkajibiwa nkikua ntajua, sa cjui ntakuwa lini.
 
Wengi tunajua tunawaonaje wanawake wanaovaa vikuku, sisi tunawaza mengine, wao wanasema ni urembo tuu.

LEO FUNGUKENI HAPA, KWANINI MNAVAA VIKUKU?
 
Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu urembo huu wa kuvaa cheni za miguuni. Wengi wamekuwa wakisema kuwa cheni hizo zinamaanisha kwamba mvaaji anaonyesha kwamba yeye anaweza mapenzi ya kinyume na maumbile, au analika pande zote tetesi hizi zimeleta mchanganyiko kidogo kwenye urembo huu.

Watu wengine wamediriki hata kukataza kabisa wapenzi wao wasivae urembo huo, mimi binafsi siwezi kuongozana na mtu amevaa kitu kama hicho.

Haya sasa kazi kwako mdau, wewe unaonaje ni sawa urembo huo kutumika, na je mwenza wako akivaa urembo huo, utaafiki?
 
Watu walitiririka sana kuhusu jambo hilo, itafute hiyo mada, ilishajadiliwa humu.
 
Kuna vitu hata havitakiwi kujadiliwa, ukitaka kufanya jambo kwa kudhamiria kuwafurahisha watu utapotea.

Hereni za masikioni wapo hawaziafiki, mwingine hasuki nywele, utakutana na asiyevaa suruali, yupo anavaa sketi fupi mwingine ndefu za kufunika miguu yote, hapo sijaongelea aliyetoboa pua, ulimi, kuweka kichuma juu ya jicho au kidevuni, wanaopigilia bangili...wote hao ukisema utafsiri wanamaanisha nini utaumia kichwa bila sababu.

Kama inakukera, mweleze mwenza wako lakini usilazimishe wengine kufuata unachokiamini wewe kuwa sahihi.
 
Poleni na msiba wa kipenzi chetu sisi wanyonge!

Ebana, mimi nina mtazamo hasi kwa wanawake wanaovaa vikuku miguuni, huwa nawaona most of them kama malaya tu.

Sasa sijui ndio ushamba wangu wa kikurya au ndio uzee unanisumbua.

Nimeambatanisha picha chini hapo ili kwa wale wasiovijua vikuku wasinisumbue kwa maswali.

FB_IMG_1616646269382.jpg
 
Back
Top Bottom