mie pia navaa kama urembo na wala si vinginevyo! kingine kuna baadh ya makabila kam wamasai wanavaa kabisa zile shanga zao miguuni! na wanapendeza kwelikweliii
charty,
Ni ukweli uyasemayo kuwa uwa ni urembo tu na si vinginevyo.
Lakini ningependa kukwambia kuwa mtazamo wa watu katika jamii yetu una shinikizo kubwa katika maamuzi yetu.
Mfano, kama tayari 'vikuku' vimeonekana kuwa ni aina ya ishara kwa wanawake kutoa kotekote. Je, ukienda kwa watu unao waheshimu wao watakufikiria vipi?
Mfano mwingine ni wanaume kusuka; jamii ya kimasai ni sehemu ya mila zao, lakini vijana wa mujini wakisuka jamii inawachulia vipi? unadhani ukitoa mfano wa wamasai wanamme kusuka ndio utaeleweka? Sidhani.
Binafsi nilimshauri mchumba wangu asivae kikuku maana ilikuwa ikiniweka kwenye mazingira magumu pindi nikiwa nae na alikubali.
Last edited by a moderator: