Mi nikijua zinakaa kiunoni?😱
Huku kwetu ukivaa hivo vicheni na.vikuku maana ake unauza 0713.....
Tena muguu yote maana ake halis unatoa kote kote ukivaa mmoja pekee unatoa nyuma pekee
Hahahah....mi kwa kweli watu wanaovaa cheni mguuni daah sijui huwa nawaonaje
Ahhha me wananiboa na wale wanaovaa pete kidole.cha mguuu
Hadi ww mtoto wa kitanga....mbona nasikia ninyi kwa kujipamba ndio wenyewe
Nasikia binamuyo ana majaaliwa hadi mtu waweza pagawa...
Sosi ni yeye mwenyewe hapo juu kanambia...
Suala la urembo kwa sisi wanawake linjumuisha mambo mengi sana kuanzia mavazi na hereni, vishaufu bangili vidani na makochokocho mengine.
Siku za karibuni kumeibuka mtindo wa wanawake kuvaa vikuku yaani cheni za miguuni. jambo hilo limekuwa likipigiwa kelele na baadhi ya watu wenye mrengo tofauti wakihusisha jambo hilo na tabia zisizofaa.
Lakini cha kushangaza nimewahi kuona baadhi ya wabunge wanawake na viongozi wa kike serikalini tena wenye mamlaka makubwa wakiwa wamevaa vikuku tena wengine walipata hata fursa ya kupiga picha na mkuu wetu na vikuku vyao.
Ninachofahamu mimi, bungeni ni mahali ambapo mavazi yanazingatiwa sana, na ninaamini wengi wetu tumewahi kushuhudia baadhi wabunge wakitolewa nje kwa sababu ya mavazi yao kuonekana kwenda kinyume na matakwa ya bunge, lakini pamoja na jamii huku nje kuwahukumu wanawake wanaovaa vikuku kama watu waliopotoka kimaadili, lakini kwenye eneo hilo la bunge inaonekana jambo hilo limepewa Baraka.
Sasa kwa kuwa suala la urembo kwa wanawake linaenda na wakati, hivi sasa tumerudi Kiafrika Zaidi, na sasa urembo wa shanga umechukua nafasi. licha ya shanga kutumika kama chachandu ya kunogesha mapenzi kwa kuvaliwa kiunoni na wanawake, lakini kwa miaka mingi urembo wa shanga umekuwa ukitumiwa na waafrika wake kwa waume katika kujipamba.
Mfano mzuri ni kwa Wamasai ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakijipamba kwa shanga wake kwa waume na wamekuwa wakipendeza haswa.
Sasa miye hivi karibuni nimeamua kujipamba Kiafrika Zaidi kwa kutupia urembo wa shanga mwilini kiunoni hadi mguuni.
Sasa sijui wenzangu mtanionaje?
CC:
miss chagga, miss neddy, miss strong, Karucee, MankaM, DEMBA, Munkari, tinna cute, Tina, Paloma, sister, Ennie, Arabela, Preta, farkhina, Asprin, Mentor, watu8, charminglady, mwekundu, Fixed Point, Ruttashobolwa utafiti, Tyta, Kaunga, Neylu[/
binafsi siwezi kuvaa vikuku