Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Aisee ilinisumbua hiyo kitu na kutokana na vipimo vyao walisema ninayo na wakanipa dawa hizo hizo ulizotumia lakini wapi ugonjwa unaisha baada ya wiki2 unarudi nikaenda pale Shekilango kuna maabara pale Legho nikafanyiwa vipimo vya damu jina limenitoka na mkojo wakakuta kunaugonjwa wa madini ya Culcium yamezidi na ndio yanasababisha maumivu ya tumbo 24/7 Vipimo vilitoka nina Culciumoex +++ ila dose yake ujipange mkuu sio chini ya elfu 50
 
Aisee ilinisumbua hiyo kitu na kutokana na vipimo vyao walisema ninayo na wakanipa dawa hizo hizo ulizotumia lakini wapi ugonjwa unaisha baada ya wiki2 unarudi nikaenda pale Shekilango kuna maabara pale Legho nikafanyiwa vipimo vya damu jina limenitoka na mkojo wakakuta kunaugonjwa wa madini ya Culcium yamezidi na ndio yanasababisha maumivu ya tumbo 24/7 Vipimo vilitoka nina Culciumoex +++ ila dose yake ujipange mkuu sio chini ya elfu 50

nashukuru kwa msaada wako
 
Ndugu WanaJF mimi ninasumbuliwa na ugonjwa wa UTI baada ya kuthibitishwa na daktari. ilinianza mwezi wa nane,nikatibiwa nikapona lakini baada ya wiki mbili ikarudi tena, nikarudi tena kwa daktari nikatibiwa na baadae ikarudi tena. yaani nimechoka na sielewi nifanyeje. dawa nlizotumia ni hizi Ciprobody,Doxin (nimekopi kama ilivyoandikwa kwnye cheti ila huenda nikakosea baadhi ya spelling). Naombeni Ushauri Kwa Wanaojua Na Mnielekeze Dawa Nzuri Zakununua. Asanteni

Pamoja na kutumia dawa, mara nyingi sindano inatibu kwa urahisi zaidi. Gharama yake ni 12,000 hivi.

Kujirudia rudia kwa ugonjwa, inatokana na nature ya maambukizo. Ugonjwa huu hutokana na bacteria wakaao katika njia ya haja kubwa. Huko hawaleti madhara yoyote. Mara waingiapo njia ya mkojo huleta maambukizi.

Hivyo, kama upo nyumba ya kupanga acha kabisa kutumia maji/kopo kwa kuchangia, beba lako.

Epuka choo cha kukaa, bora upande juu kivunjike.

Kama ni mtu wa kilaji, chunga sana sink za kukojolea bar, kwani nyingine zipo juu usawa wa kikojoleo na wakati mwingine inagusa hapo au matone kurukia.

Kama hujaoa, haja zako unamalizia gest, basi epuka gest za uswazi na zaidi taulo, na sabuni zilizobakizwa na mteja mwingine hata kama ni hotel.

Mwisho, 'Use a condom every time you have sex'
 
Mkuu kama una mwenzio unayekuwa naye faragha mara kwa mara naye hajawahi kutibiwa UTI basi labda ndio sababu kila ukipona ugonjwa hurudia tena baada ya muda mfupi. Kama unaye basi inabidi naye atibiwe ili kuhakikisha ugonjwa unapotea kabisa. Kila la heri.
 
Unatakiwa uwe mwangalifu na msafi hasa maliwatoni,kunywa na jisafishe kwa maji ya kutosha..kama una patna hakikisha nae anapata doz na msikutane kimwili mpaka mpime tena na kuonekana mpo salama,ila kama unakunywa dawa na still mnascrew kupona itakuwa ni ndoto,pole sana
 
Pamoja na kutumia dawa, mara nyingi sindano inatibu kwa urahisi zaidi. Gharama yake ni 12,000 hivi.

Kujirudia rudia kwa ugonjwa, inatokana na nature ya maambukizo. Ugonjwa huu hutokana na bacteria wakaao katika njia ya haja kubwa. Huko hawaleti madhara yoyote. Mara waingiapo njia ya mkojo huleta maambukizi.

Hivyo, kama upo nyumba ya kupanga acha kabisa kutumia maji/kopo kwa kuchangia, beba lako.

Epuka choo cha kukaa, bora upande juu kivunjike.

Kama ni mtu wa kilaji, chunga sana sink za kukojolea bar, kwani nyingine zipo juu usawa wa kikojoleo na wakati mwingine inagusa hapo au matone kurukia.

Kama hujaoa, haja zako unamalizia gest, basi epuka gest za uswazi na zaidi taulo, na sabuni zilizobakizwa na mteja mwingine hata kama ni hotel.

Mwisho, 'Use a condom every time you have sex'

Nakushukuru sana ndugu nimefaidika na mengi mno.mungu akulipe
 
Unatakiwa uwe mwangalifu na msafi hasa maliwatoni,kunywa na jisafishe kwa maji ya kutosha..kama una patna hakikisha nae anapata doz na msikutane kimwili mpaka mpime tena na kuonekana mpo salama,ila kama unakunywa dawa na still mnascrew kupona itakuwa ni ndoto,pole sana

nashukuru ndugu chocs
 
Hivi UTI na STD kuna tofauti gani?samahani lakini nataka kujua.
 
Hivi UTI na STD kuna tofauti gani?samahani lakini nataka kujua.

Navyofaham mimi kuna tofauti cz u.t.i inatokana na maambukizi kwa njia ya mkojo na hayo mengine kwa njia ya kujamiiana. Ingawa u.t.i ikikomaa sana inaweza sababisha kupata ugonjwa wa zinaa pia.
 
Navyofaham mimi kuna tofauti cz u.t.i inatokana na maambukizi kwa njia ya mkojo na hayo mengine kwa njia ya kujamiiana. Ingawa u.t.i ikikomaa sana inaweza sababisha kupata ugonjwa wa zinaa pia.

Thanks Mkuu!
 
MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA
MKOJO (UTI’s) YAFAHAMU NINI
CHANZO NA JINSI YA KUZUIA.
Maambukizi katika njia ya
mkojo au katika kibovu cha
mkojo, tatizo hili SI
miongoni mwa magonjwa
ya zinaa (STDs)
Mara nyingi tatizo hili
husababishwa na bacteria
anajukanae kama E.coli,
JINSI UNAVYOENEA
UTIs ni tatizo miongoni mwa
watu hasa wanawake hasa
wenye uke kwa sababu ya
uwazi wa urethra kuwa
karibu sana uke na tundu la
haja kubwa.
Kuna bacteria hatari kutoka
tumboni na kuingia katika
njia ya mkojo urethra kwa
kuwafuta au kuwapangusa
kutoka kwenye huo uwazi
wa uke na tundu la haja
kubwa.
Vile vile watu wenye uke
(wanawake) wana mrija
mfupi sana wa urethra
(mrija wa mkojo) hivyo kwa
sababu hiyo ni rahisi kwa
bacteria kusafiri na kuingia
kwenye kibovu cha mkojo na
kusababisha maambukizi.
Kibofu cha mkojo (bladder)
ni kiungo ambacho hutunza
mkojo kabla ya mkojo
kuingizwa kwenye mrija
urethra wake ili utoke
njekwa njia ya kukojoa.
NINI DALILI ZAKE
Dalili za maambukizi katika
njia ya mkojo (UTIs) kama
yafuatayo;
Kukojoa mara kwa mara
kusiko kawaida;
Maumivu kama ya kuwaka
moto wakati wa kukojoa
(kama unaunguzwa na
mkojo);
Mkojo kutoa harufu isiyo ya
kawaida;
Mkojo kuwa na hali ya damu
ndani yake;
maumivu ya tumbo la chini
mara nyingine;
Pia homa.
JINSI UCHUNGUZI
UNAVYOFANYIKA.
Mara zingine uchunguzi wa
haya Maambukizi katika njia
ya Mkojo yana unaweza
kufanyika kwa kuchunguza
dalili hizo nilizo taja hapo
juu.
Vile vile huweza kufanyika
kwa kupima Mkojo, mkojo
kupelekwa Maabara kwa
uchunguzi zaidi ambapo
huchunguzwa kwa kupima
kuwepo kwa Bacteria
wasababishao maambukizi
hayo (E.coli)
NINI MATATIZO YAKE.
Endapo kama maambukizi
haya ya njia ya mkojo
hayatotibiwa mapema na
kimamilifu, maambukizi
yanaweza kusambaa mpaka
kwenye mfumo wa mkojo
wa juu (kwenye kibofu na
figo kuathirika),
Na inapofikia hali hiyo ya
maambukizi basi inaweza
kupelekea kulazwa
hospitalini.
Pia, maumivu yanapokuwa
ya hali ya juu, hasa maumivu
ya tumbo la chini, mkojo
kuwa na damu, haraka sana
mwone mhudumu wa afya
iwezekanavyo.
JINSI INAVYOTIBIWA.
Maambukizi katika njia ya
mkojo (UTIs)
Tiba yake ni rahisi tu
ambapo ANTIBIOTICS tu
hutumika, (ni vizuri dawa
hizo majina yake uende
moja kwa moja hospital
ukaandikiwe na daktari
kulingana na kiwango cha
maambukizi kilivyo na
sababu zingine utakazokuwa
nazo ndio maana sijaandika
ni aina gani ya ANTIBIOTICS
zinazotakiwa).
Ni muhimu sana kumaliza
dozi uliyopangiwa hata
kama dalili zote zimekwisha
ni lazima umalize dozi hiyo.
Kama dalili ulizokuwa nazo
hazikuisha mpaka dozi
inakwisha basi tambua ya
kuwa, kuna uwezekano
kuwa bacteria wamekuwa
sugu kwenye hiyo aina ya
dawa uliyotumia.
Na utashauriwa
kuchunguzwa upya na
kutibiwa upya.
Habari gani kuhusu Mpenzi
wako ama mwenza wako
endapo wewe unapata
Maambukizi kwenye njia ya
mkojo (UTIs)?
Maambukizi kwenye njia ya
mkojo (UTIs) sio ugonjwa wa
zinaa .
Lakini kujishughulisha na
Ngono kunaweza kupelekea
maambukizi haya na
kumbuka mpenzi au
mwenza wako hahitaji
kutibiwa.
KUZUIA MAAMBUKIZI
KWENYE NJIA YA MKOJO.
Unaweza kuzuia (sio kutibu)
Kwa kufanya yafuatayo;
Kunywa mpaka glass sita za
maji kwa siku;
Kunywa kwa wingi juisi
chachu ya Cranberry (jamii
ya matunda Damu)
Kojoa mara kwa mara kadiri
iwezekavyo.
Kojoa kabla na Baada ya
tendo la ngono/ndoa
Jipanguse/jisafishe kwa
kutoka mbele kwenda
nyuma mara baada ya kuoga
au baada ya kujisaidia.
(namaana wakati wa
kuchamba basi ni vyema
ukajisafisha kwa kupeleka
nyuma na sio mbele upande
wa uke ilipo urethra)
Vaa chupi au nguo za ndani
zisizo bana sana na hasa si
vizuri kuvaa nguo za jamii
ya nailoni, ni vizuri kuvaa
nguzo za ndani jamii ya
pamba ni nzuri zaidi.
Oga Mara kwa Mara
Pia, kama unajua una
Maambukizi katika njia ya
mkojo basi fanya haya;
Jizuie au acha kunywa chai,
kahawa, bia, mvinyo na vitu
kama hivyo vyenye jamii ya
alkali ndani yake.
Jihadhari na juisi ya
machungwa kwa sababu
vyote hivyo hubadilika na
kuwa alkali ndani ya mwili
ambayo huchangia bacteria
kukua ndani ya mwili
asababishae UTIs.
Tumia vitamin C kama
kichochezi asilia cha kufanya
ukojoe mara kwa mara.
Kitu kingine cha muhimu cha
kuzingatia ni kuzuia kutumia
vimiminika/vinywaji.
Makala hii inalenga kukupa
mwanga nini juu ya
ugonjwa huu wa
maambukizi katika njia ya
mkojo ili uweze kujua ni
namna gani ya kukabiliana
nayo.
Endapo hali inakuwa tofauti
basi wahi kituo cha afya kwa
uchunguzi zaidi.
CHANZO!
ManyandaHealthy: MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO (UTI's) YAFAHAMU NINI CHANZO NA JINSI YA KUZUIA.
 
MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA
MKOJO (UTI’s) YAFAHAMU NINI
CHANZO NA JINSI YA KUZUIA.
Maambukizi katika njia ya
mkojo au katika kibovu cha
mkojo, tatizo hili SI
miongoni mwa magonjwa
ya zinaa (STDs)
Mara nyingi tatizo hili
husababishwa na bacteria
anajukanae kama E.coli,
JINSI UNAVYOENEA
UTIs ni tatizo miongoni mwa
watu hasa wanawake hasa
wenye uke kwa sababu ya
uwazi wa urethra kuwa
karibu sana uke na tundu la
haja kubwa.
Kuna bacteria hatari kutoka
tumboni na kuingia katika
njia ya mkojo urethra kwa
kuwafuta au kuwapangusa
kutoka kwenye huo uwazi
wa uke na tundu la haja
kubwa.
Vile vile watu wenye uke
(wanawake) wana mrija
mfupi sana wa urethra
(mrija wa mkojo) hivyo kwa
sababu hiyo ni rahisi kwa
bacteria kusafiri na kuingia
kwenye kibovu cha mkojo na
kusababisha maambukizi.
Kibofu cha mkojo (bladder)
ni kiungo ambacho hutunza
mkojo kabla ya mkojo
kuingizwa kwenye mrija
urethra wake ili utoke
njekwa njia ya kukojoa.
NINI DALILI ZAKE
Dalili za maambukizi katika
njia ya mkojo (UTIs) kama
yafuatayo;
Kukojoa mara kwa mara
kusiko kawaida;
Maumivu kama ya kuwaka
moto wakati wa kukojoa
(kama unaunguzwa na
mkojo);
Mkojo kutoa harufu isiyo ya
kawaida;
Mkojo kuwa na hali ya damu
ndani yake;
maumivu ya tumbo la chini
mara nyingine;
Pia homa.
JINSI UCHUNGUZI
UNAVYOFANYIKA.
Mara zingine uchunguzi wa
haya Maambukizi katika njia
ya Mkojo yana unaweza
kufanyika kwa kuchunguza
dalili hizo nilizo taja hapo
juu.
Vile vile huweza kufanyika
kwa kupima Mkojo, mkojo
kupelekwa Maabara kwa
uchunguzi zaidi ambapo
huchunguzwa kwa kupima
kuwepo kwa Bacteria
wasababishao maambukizi
hayo (E.coli)
NINI MATATIZO YAKE.
Endapo kama maambukizi
haya ya njia ya mkojo
hayatotibiwa mapema na
kimamilifu, maambukizi
yanaweza kusambaa mpaka
kwenye mfumo wa mkojo
wa juu (kwenye kibofu na
figo kuathirika),
Na inapofikia hali hiyo ya
maambukizi basi inaweza
kupelekea kulazwa
hospitalini.
Pia, maumivu yanapokuwa
ya hali ya juu, hasa maumivu
ya tumbo la chini, mkojo
kuwa na damu, haraka sana
mwone mhudumu wa afya
iwezekanavyo.
JINSI INAVYOTIBIWA.
Maambukizi katika njia ya
mkojo (UTIs)
Tiba yake ni rahisi tu
ambapo ANTIBIOTICS tu
hutumika, (ni vizuri dawa
hizo majina yake uende
moja kwa moja hospital
ukaandikiwe na daktari
kulingana na kiwango cha
maambukizi kilivyo na
sababu zingine utakazokuwa
nazo ndio maana sijaandika
ni aina gani ya ANTIBIOTICS
zinazotakiwa).
Ni muhimu sana kumaliza
dozi uliyopangiwa hata
kama dalili zote zimekwisha
ni lazima umalize dozi hiyo.
Kama dalili ulizokuwa nazo
hazikuisha mpaka dozi
inakwisha basi tambua ya
kuwa, kuna uwezekano
kuwa bacteria wamekuwa
sugu kwenye hiyo aina ya
dawa uliyotumia.
Na utashauriwa
kuchunguzwa upya na
kutibiwa upya.
Habari gani kuhusu Mpenzi
wako ama mwenza wako
endapo wewe unapata
Maambukizi kwenye njia ya
mkojo (UTIs)?
Maambukizi kwenye njia ya
mkojo (UTIs) sio ugonjwa wa
zinaa .
Lakini kujishughulisha na
Ngono kunaweza kupelekea
maambukizi haya na
kumbuka mpenzi au
mwenza wako hahitaji
kutibiwa.
KUZUIA MAAMBUKIZI
KWENYE NJIA YA MKOJO.
Unaweza kuzuia (sio kutibu)
Kwa kufanya yafuatayo;
Kunywa mpaka glass sita za
maji kwa siku;
Kunywa kwa wingi juisi
chachu ya Cranberry (jamii
ya matunda Damu)
Kojoa mara kwa mara kadiri
iwezekavyo.
Kojoa kabla na Baada ya
tendo la ngono/ndoa
Jipanguse/jisafishe kwa
kutoka mbele kwenda
nyuma mara baada ya kuoga
au baada ya kujisaidia.
(namaana wakati wa
kuchamba basi ni vyema
ukajisafisha kwa kupeleka
nyuma na sio mbele upande
wa uke ilipo urethra)
Vaa chupi au nguo za ndani
zisizo bana sana na hasa si
vizuri kuvaa nguo za jamii
ya nailoni, ni vizuri kuvaa
nguzo za ndani jamii ya
pamba ni nzuri zaidi.
Oga Mara kwa Mara
Pia, kama unajua una
Maambukizi katika njia ya
mkojo basi fanya haya;
Jizuie au acha kunywa chai,
kahawa, bia, mvinyo na vitu
kama hivyo vyenye jamii ya
alkali ndani yake.
Jihadhari na juisi ya
machungwa kwa sababu
vyote hivyo hubadilika na
kuwa alkali ndani ya mwili
ambayo huchangia bacteria
kukua ndani ya mwili
asababishae UTIs.
Tumia vitamin C kama
kichochezi asilia cha kufanya
ukojoe mara kwa mara.
Kitu kingine cha muhimu cha
kuzingatia ni kuzuia kutumia
vimiminika/vinywaji.
Makala hii inalenga kukupa
mwanga nini juu ya
ugonjwa huu wa
maambukizi katika njia ya
mkojo ili uweze kujua ni
namna gani ya kukabiliana
nayo.
Endapo hali inakuwa tofauti
basi wahi kituo cha afya kwa
uchunguzi zaidi.
CHANZO!
ManyandaHealthy: MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO (UTI’s) YAFAHAMU NINI CHANZO NA JINSI YA KUZUIA.

Ahsante sana Mkuu!
 
Habari wana JF na wenye ufahamu na Mambo ya kitabibu.

Nimechelewa mno kugundua tatizo la mkojo mchafu kwa mwanangu wa miezi tisa.

Alianza kwa kujishikashika nyeti zake kama miezi miwili nyuma, sasa labda kwa kukosa uzoefu kwa Kuwa ndiye mtoto wangu wa kwanza sikugundua kuwa linaweza kuwa Ni tatizo, sasa mpaka tunashtuka mimi na mama yake mtoto anakojoa damu.

Tulimkimbiza haraka hospitali kariakoo kwa dk Hameer ma ametupa dawa fulani hivi ya unga ya kuchanganya ma maji ambayo anatumia siku ya pili sasa,
Ila mtoto anapata taabu sana akojoapo yaani ni kilio hatulali wala mchana hatupumziki kabisa!

Je, hii hali itakwisha kweli maana tunakosa raha kwa kweli tunapomwona mtoto wetu pekee anapata taabu namna hii.

Ana siku ya pili anatumia dawa, mtoto wetu ni wa kiume.
 
Habari wana jf na wenye ufahamu na Mambo ya kitabibu.
Nimechelewa mno kugundua tatizo la mkojo mchafu kwa mwanangu wa miezi tisa,
Alianza kwa kujishikashika nyeti zake kama miezi miwili nyuma, sasa labda kwa kukosa uzoefu kwa Kuwa ndiye mtoto wangu wa kwanza sikugundua kuwa linaweza kuwa Ni tatizo, sasa mpaka tunashtuka mimi na mama yake mtoto anakojoa damu,
Tulimkimbiza haraka hospitali kariakoo kwa dk Hameer ma ametupa dawa fulani hivi ya unga ya kuchanganya ma maji ambayo anatumia siku ya pili sasa,
Ila mtoto anapata taabu sana akojoapo yaani ni kilio hatulali wala mchana hatupumziki kabisa!

je hii hali itakwisha kweli maana tunakosa raha kwa kweli tunapomwona mtoto wetu pekee anapata taabu namna hii.
ana siku ya pili anatumia dawa, mtoto wetu ni wa kiume.

Hili tatizo la UTI kwa watoto wa kiume wanatahiriwa kwa lazima kupunguza maambukizi ya UTI
 
dalili kubwa huwa ni homa me navyo jua though bado sijapata mtoto. watakuja wataalamu zaidi
 
Akipona tu tafadhali sana atahiriwe na pia acha kumvalisha nepi mchana, hata usiku ni bora muwe mnamuasha kumkojolesha. Pia akioga hakikisha anasuuzwa mwili na maji masafi yasiyo na sabuni, pia msisafishe mzee wake na sabuni hata kidogo.
 
Akipona tu tafadhali sana atahiriwe na pia acha kumvalisha nepi mchana, hata usiku ni bora muwe mnamuasha kumkojolesha. Pia akioga hakikisha anasuuzwa mwili na maji masafi yasiyo na sabuni, pia msisafishe mzee wake na sabuni hata kidogo.

Ahsante kwa ushauri, mengine ndio tunajifuza maana sisi ni walezi wachanga,
Ndio mtoto wetu wa kwanza.
 
Back
Top Bottom