MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA
MKOJO (UTIs) YAFAHAMU NINI
CHANZO NA JINSI YA KUZUIA.
Maambukizi katika njia ya
mkojo au katika kibovu cha
mkojo, tatizo hili SI
miongoni mwa magonjwa
ya zinaa (STDs)
Mara nyingi tatizo hili
husababishwa na bacteria
anajukanae kama E.coli,
JINSI UNAVYOENEA
UTIs ni tatizo miongoni mwa
watu hasa wanawake hasa
wenye uke kwa sababu ya
uwazi wa urethra kuwa
karibu sana uke na tundu la
haja kubwa.
Kuna bacteria hatari kutoka
tumboni na kuingia katika
njia ya mkojo urethra kwa
kuwafuta au kuwapangusa
kutoka kwenye huo uwazi
wa uke na tundu la haja
kubwa.
Vile vile watu wenye uke
(wanawake) wana mrija
mfupi sana wa urethra
(mrija wa mkojo) hivyo kwa
sababu hiyo ni rahisi kwa
bacteria kusafiri na kuingia
kwenye kibovu cha mkojo na
kusababisha maambukizi.
Kibofu cha mkojo (bladder)
ni kiungo ambacho hutunza
mkojo kabla ya mkojo
kuingizwa kwenye mrija
urethra wake ili utoke
njekwa njia ya kukojoa.
NINI DALILI ZAKE
Dalili za maambukizi katika
njia ya mkojo (UTIs) kama
yafuatayo;
Kukojoa mara kwa mara
kusiko kawaida;
Maumivu kama ya kuwaka
moto wakati wa kukojoa
(kama unaunguzwa na
mkojo);
Mkojo kutoa harufu isiyo ya
kawaida;
Mkojo kuwa na hali ya damu
ndani yake;
maumivu ya tumbo la chini
mara nyingine;
Pia homa.
JINSI UCHUNGUZI
UNAVYOFANYIKA.
Mara zingine uchunguzi wa
haya Maambukizi katika njia
ya Mkojo yana unaweza
kufanyika kwa kuchunguza
dalili hizo nilizo taja hapo
juu.
Vile vile huweza kufanyika
kwa kupima Mkojo, mkojo
kupelekwa Maabara kwa
uchunguzi zaidi ambapo
huchunguzwa kwa kupima
kuwepo kwa Bacteria
wasababishao maambukizi
hayo (E.coli)
NINI MATATIZO YAKE.
Endapo kama maambukizi
haya ya njia ya mkojo
hayatotibiwa mapema na
kimamilifu, maambukizi
yanaweza kusambaa mpaka
kwenye mfumo wa mkojo
wa juu (kwenye kibofu na
figo kuathirika),
Na inapofikia hali hiyo ya
maambukizi basi inaweza
kupelekea kulazwa
hospitalini.
Pia, maumivu yanapokuwa
ya hali ya juu, hasa maumivu
ya tumbo la chini, mkojo
kuwa na damu, haraka sana
mwone mhudumu wa afya
iwezekanavyo.
JINSI INAVYOTIBIWA.
Maambukizi katika njia ya
mkojo (UTIs)
Tiba yake ni rahisi tu
ambapo ANTIBIOTICS tu
hutumika, (ni vizuri dawa
hizo majina yake uende
moja kwa moja hospital
ukaandikiwe na daktari
kulingana na kiwango cha
maambukizi kilivyo na
sababu zingine utakazokuwa
nazo ndio maana sijaandika
ni aina gani ya ANTIBIOTICS
zinazotakiwa).
Ni muhimu sana kumaliza
dozi uliyopangiwa hata
kama dalili zote zimekwisha
ni lazima umalize dozi hiyo.
Kama dalili ulizokuwa nazo
hazikuisha mpaka dozi
inakwisha basi tambua ya
kuwa, kuna uwezekano
kuwa bacteria wamekuwa
sugu kwenye hiyo aina ya
dawa uliyotumia.
Na utashauriwa
kuchunguzwa upya na
kutibiwa upya.
Habari gani kuhusu Mpenzi
wako ama mwenza wako
endapo wewe unapata
Maambukizi kwenye njia ya
mkojo (UTIs)?
Maambukizi kwenye njia ya
mkojo (UTIs) sio ugonjwa wa
zinaa .
Lakini kujishughulisha na
Ngono kunaweza kupelekea
maambukizi haya na
kumbuka mpenzi au
mwenza wako hahitaji
kutibiwa.
KUZUIA MAAMBUKIZI
KWENYE NJIA YA MKOJO.
Unaweza kuzuia (sio kutibu)
Kwa kufanya yafuatayo;
Kunywa mpaka glass sita za
maji kwa siku;
Kunywa kwa wingi juisi
chachu ya Cranberry (jamii
ya matunda Damu)
Kojoa mara kwa mara kadiri
iwezekavyo.
Kojoa kabla na Baada ya
tendo la ngono/ndoa
Jipanguse/jisafishe kwa
kutoka mbele kwenda
nyuma mara baada ya kuoga
au baada ya kujisaidia.
(namaana wakati wa
kuchamba basi ni vyema
ukajisafisha kwa kupeleka
nyuma na sio mbele upande
wa uke ilipo urethra)
Vaa chupi au nguo za ndani
zisizo bana sana na hasa si
vizuri kuvaa nguo za jamii
ya nailoni, ni vizuri kuvaa
nguzo za ndani jamii ya
pamba ni nzuri zaidi.
Oga Mara kwa Mara
Pia, kama unajua una
Maambukizi katika njia ya
mkojo basi fanya haya;
Jizuie au acha kunywa chai,
kahawa, bia, mvinyo na vitu
kama hivyo vyenye jamii ya
alkali ndani yake.
Jihadhari na juisi ya
machungwa kwa sababu
vyote hivyo hubadilika na
kuwa alkali ndani ya mwili
ambayo huchangia bacteria
kukua ndani ya mwili
asababishae UTIs.
Tumia vitamin C kama
kichochezi asilia cha kufanya
ukojoe mara kwa mara.
Kitu kingine cha muhimu cha
kuzingatia ni kuzuia kutumia
vimiminika/vinywaji.
Makala hii inalenga kukupa
mwanga nini juu ya
ugonjwa huu wa
maambukizi katika njia ya
mkojo ili uweze kujua ni
namna gani ya kukabiliana
nayo.
Endapo hali inakuwa tofauti
basi wahi kituo cha afya kwa
uchunguzi zaidi.
CHANZO!
ManyandaHealthy: MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO (UTIs) YAFAHAMU NINI CHANZO NA JINSI YA KUZUIA.